Kauli ya CDF mstaafu kuhusu waliotaka kupindisha katiba ili Rais Samia asiapishwe inanipa picha halisi ya kwanini Bashiru na wenzake walitenguliwa

Wacheni lawama za Kijinga kama umemsikiliza vizuri alitumia approach za concesus na mwishoni yeye na Kamati Yake ya ulinzi ndiyo waliyekuwa wanaamua kikatiba!

Wanasiasa huwa wanaweka interests wakiongozwa na wakina Ndugai! Unafikiri ni kazi rahisi mbele ya wafia dini wa Amirata na Sukumagang ya wakina Ndugai, Bashiru na Polepole?
 
Hizo ni hearsay mkuu,kwa hali aliyokuwa nayo ninani alikuwa anamuhudumia?
 
Sio lazima CDF ajue kila kitu kuhusu katiba. Na kwakuwa hakuwa anajua katiba inasemaje, alitumia busara kubwa kurejea na kuangalia katiba inasemaje kulingana na hali na mazingira yalivyokuwa.

Hakuna mtu anayejua kila kitu. Msijifanye much know.Shame on you!
 
Hearsay ni mambo ya maisha binafsi unayosema wewe
Nilijua utasema hivyo.Ndiyo maana sikutaka kujikita huko.

Na wewe umefanya kosa la kuita hearsay kitu ambacho hata hujakisikia. Yani kabla mimi sijasema hayo mambo ya maisha binafsi ni yapi, wewe ushayaita hearsay. Umeonesha bias yako tu.

If you know, you know. Sina haja ya kubishana kwenye hayo.
 
Haya mambo yalijulikana na tuliyajadili hapa.

Mabeyo kaja kuweka rekodi wazi tu na hata hiyo kaweka kwa summary tu. Kuna mengi sana hajasema.

Kitabu kizima kikitoka mtastuka sana.
Nchi hii ina mengi yaliojificha aisee.
 
Kauli ya kwamba familia pia ilikuwa haijui inafikirisha sana, yaani mke wake Mama Janeth hakuwa karibu na mumewe kumuhudumia....... mpaka anafariki??
Kuna hali fulan ya mgonjwa ikifikia, basi ni madaktari tu ndo wanatakiwa wawe karibu na mgonjwa ili kuwapa nguvu ya kupambania maisha yake.

Muda huo mgonjwa anatakiwa awe katika sehem yenye utulivu huku akiwa chini ya uangalizi wa karibu mno na wa mara kwa mara wa madaktari. Yani hata hao viongozi wa vyombo vya usalama wanakuwa hapo kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa mgonjwa na hasa kiongozi wa nchi.
 
Hapana! Mabeyo hakuliangalia hili unalolisema wewe!

Mabeyo alitazama mbele athari ya kupindua mamlaka ukiyaruhusu tu hata kwa mara moja watu wataona ni mchezo wa kawaida na usalama wa nchi utakuwa kwenye hatari zaidi. Kuna mambo ya kusigina lakini mambo ya kupindua utawala wa mwenzako si jambo dogo kwa usalama wa nchi.

Na kaweka msingi bora ya kuwa nafasi ya jeshi kwa usalama wa nchi ni ipi na nafasi ya wanasiasa na mamluki ni ipi!
 
Kipande hiki chote ni maneno ya hisia, tuhuma na kuokoteza tu.
Weka ushahidi japo kidogo umetoa wapi n.k.
 
Hilo wala halina mashiko. Kama ni jinsia mbona angeweza kuchagua mwanamke mungine kutoka Zanzibar, inamaana Zanzibar nzima mwanamke alikuwa ni huyo huyo mama Samia?

Pia hakuna wanawake wengine waislam kule Zanzibar?
Nitajie mwanamke mwenye ushawishi zanzibar unayemjua kwenye siasa 2015/2020.
 
Naona ni maneno tu yasiyo na uthibitisho wowote ule.

Haina shida, hata hivyo. Ni haki ya watu kusema, iwe uzushi au la!
Yeah mkuu siyo kila mjadala unahitaji uthibitisho kama ile ya "thibitisha mungu yupo na ukishindwa basi hayupo", kuna mambo unaweza ukawa unambishia mtu kumbe kuna kitu anakijua ambacho wewe hukijui ila tu hawezi kukisema hadharani, kwahiyo mambo mengine ni kuacha tu watu waamini wanachokiamini kwa sababu ni 'siri za kambi' na haiwezekani kuthibitisha ila si kwamba hayapo
 
Kipande hiki chote ni maneno ya hisia, tuhuma na kuokoteza tu.
Weka ushahidi japo kidogo umetoa wapi n.k.
 

Hivi unajisikia lakini? CDF asijue katiba na sio lazima ajue? Unajisikia? Tuna safari kubwa sana kama Taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…