Kauli ya CDF mstaafu kuhusu waliotaka kupindisha katiba ili Rais Samia asiapishwe inanipa picha halisi ya kwanini Bashiru na wenzake walitenguliwa

Kauli ya CDF mstaafu kuhusu waliotaka kupindisha katiba ili Rais Samia asiapishwe inanipa picha halisi ya kwanini Bashiru na wenzake walitenguliwa

Hilo hata mimi limenishangaza. Lkn hata kama alikuwa hajui hilo, ina maana alishindwa kuwa na mwanasheria ambae angemwambia ni nani mwenye jukumu la kutangaza kifo cha raisi au kiongozi mkuu wa serikali.

Toka lini kifo cha mkuu wa nchi kikatangazwa na katibu mkuu kiongozi au waziri mkuu huku makamu wa raisi akiwa nchini!
Wacheni lawama za Kijinga kama umemsikiliza vizuri alitumia approach za concesus na mwishoni yeye na Kamati Yake ya ulinzi ndiyo waliyekuwa wanaamua kikatiba!

Wanasiasa huwa wanaweka interests wakiongozwa na wakina Ndugai! Unafikiri ni kazi rahisi mbele ya wafia dini wa Amirata na Sukumagang ya wakina Ndugai, Bashiru na Polepole?
 
Hiyo yote inaonekana ni kwa amri kutoka juu, amri yake mwenyewe Magufuli.

Magufuli angetaka mkewe aende Kwa Mzena angetoa amri moja tu, hata kwa helikopta angeweza kupelekwa, mbona aliamrisha mpaka Kardinali Pengo aende?

Stories za Magufuli alivyokuwa anaiendesha familia yake zikija kutoka watu watamuangalia Magufuli tofauti.
Hizo ni hearsay mkuu,kwa hali aliyokuwa nayo ninani alikuwa anamuhudumia?
 
Hilo hata mimi limenishangaza. Lkn hata kama alikuwa hajui hilo, ina maana alishindwa kuwa na mwanasheria ambae angemwambia ni nani mwenye jukumu la kutangaza kifo cha raisi au kiongozi mkuu wa serikali.

Toka lini kifo cha mkuu wa nchi kikatangazwa na katibu mkuu kiongozi au waziri mkuu huku makamu wa raisi akiwa nchini!
Sio lazima CDF ajue kila kitu kuhusu katiba. Na kwakuwa hakuwa anajua katiba inasemaje, alitumia busara kubwa kurejea na kuangalia katiba inasemaje kulingana na hali na mazingira yalivyokuwa.

Hakuna mtu anayejua kila kitu. Msijifanye much know.Shame on you!
 
Hearsay ni mambo ya maisha binafsi unayosema wewe
Nilijua utasema hivyo.Ndiyo maana sikutaka kujikita huko.

Na wewe umefanya kosa la kuita hearsay kitu ambacho hata hujakisikia. Yani kabla mimi sijasema hayo mambo ya maisha binafsi ni yapi, wewe ushayaita hearsay. Umeonesha bias yako tu.

If you know, you know. Sina haja ya kubishana kwenye hayo.
 
Haya mambo yalijulikana na tuliyajadili hapa.

Mabeyo kaja kuweka rekodi wazi tu na hata hiyo kaweka kwa summary tu. Kuna mengi sana hajasema.

Kitabu kizima kikitoka mtastuka sana.
Nchi hii ina mengi yaliojificha aisee.
 
Kauli ya kwamba familia pia ilikuwa haijui inafikirisha sana, yaani mke wake Mama Janeth hakuwa karibu na mumewe kumuhudumia....... mpaka anafariki??
Kuna hali fulan ya mgonjwa ikifikia, basi ni madaktari tu ndo wanatakiwa wawe karibu na mgonjwa ili kuwapa nguvu ya kupambania maisha yake.

Muda huo mgonjwa anatakiwa awe katika sehem yenye utulivu huku akiwa chini ya uangalizi wa karibu mno na wa mara kwa mara wa madaktari. Yani hata hao viongozi wa vyombo vya usalama wanakuwa hapo kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa mgonjwa na hasa kiongozi wa nchi.
 
Mabeyo kwenye hii ishu alitumika tu sidhani kama he saw what was coming, Mabeyo ni pro Magufuli na ndio maana baada ya mwaka tu alipoona mambo yanaanza kuenda mrama, akatangaza kustaafu bila sababu za msingi

Ni wazi pro Magufulis kina Bashiru and co hawakumtaka Mama, maana since day one alishaonesha dalili kuwa ni pandikizi la Godfather ndio maana walitaka kupindisha katiba, ila Godfather akaingilia kati akaamua kumtumia Mabeyo hapo

Akamuambia kwamba waambie hao kina Bashiru and co kuwa tumeshitukia mchezo wao, hivyo waambie wamuapishe huyo Mama haraka iwezekanavyo, kwahiyo ni kama Godfather alitumia advantage ya katiba kwa maslahi yake na genge lake
Hapana! Mabeyo hakuliangalia hili unalolisema wewe!

Mabeyo alitazama mbele athari ya kupindua mamlaka ukiyaruhusu tu hata kwa mara moja watu wataona ni mchezo wa kawaida na usalama wa nchi utakuwa kwenye hatari zaidi. Kuna mambo ya kusigina lakini mambo ya kupindua utawala wa mwenzako si jambo dogo kwa usalama wa nchi.

Na kaweka msingi bora ya kuwa nafasi ya jeshi kwa usalama wa nchi ni ipi na nafasi ya wanasiasa na mamluki ni ipi!
 
Lakini nyuma ya pazia hiyo haikuwa sababu kubwa, 'Wahusika' wanadai yeye na Magufuli walishapanga mwaka atakaostaafu, (endapo angeendelea kuwa hai) ambapo haikutakiwa kuwa 2022

Na CDF mpya alikuwa ameshaandaliwa Major General Charles Mbuge, ambaye naye alikuwa ni pro Magufuli, ndio maana kustaafu kwa Mabeyo kuliibua maswali kwa waliokuwa wanajua kinachoendelea
Kipande hiki chote ni maneno ya hisia, tuhuma na kuokoteza tu.
Weka ushahidi japo kidogo umetoa wapi n.k.
 
Hilo wala halina mashiko. Kama ni jinsia mbona angeweza kuchagua mwanamke mungine kutoka Zanzibar, inamaana Zanzibar nzima mwanamke alikuwa ni huyo huyo mama Samia?

Pia hakuna wanawake wengine waislam kule Zanzibar?
Nitajie mwanamke mwenye ushawishi zanzibar unayemjua kwenye siasa 2015/2020.
 
Naona ni maneno tu yasiyo na uthibitisho wowote ule.

Haina shida, hata hivyo. Ni haki ya watu kusema, iwe uzushi au la!
Yeah mkuu siyo kila mjadala unahitaji uthibitisho kama ile ya "thibitisha mungu yupo na ukishindwa basi hayupo", kuna mambo unaweza ukawa unambishia mtu kumbe kuna kitu anakijua ambacho wewe hukijui ila tu hawezi kukisema hadharani, kwahiyo mambo mengine ni kuacha tu watu waamini wanachokiamini kwa sababu ni 'siri za kambi' na haiwezekani kuthibitisha ila si kwamba hayapo
 
Kipande hiki chote ni maneno ya hisia, tuhuma na kuokoteza tu.
Weka ushahidi japo kidogo umetoa wapi n.k.
Yeah mkuu siyo kila mjadala unahitaji uthibitisho kama ile ya "thibitisha mungu yupo na ukishindwa basi hayupo", kuna mambo unaweza ukawa unambishia mtu kumbe kuna kitu anakijua ambacho wewe hukijui ila tu hawezi kukisema hadharani, kwahiyo mambo mengine ni kuacha tu watu waamini wanachokiamini kwa sababu ni 'siri za kambi' na haiwezekani kuthibitisha ila si kwamba hayapo
 
Sio lazima CDF ajue kila kitu kuhusu katiba. Na kwakuwa hakuwa anajua katiba inasemaje, alitumia busara kubwa kurejea na kuangalia katiba inasemaje kulingana na hali na mazingira yalivyokuwa.

Hakuna mtu anayejua kila kitu. Msijifanye much know.Shame on you!

Hivi unajisikia lakini? CDF asijue katiba na sio lazima ajue? Unajisikia? Tuna safari kubwa sana kama Taifa.
 
Back
Top Bottom