Kauli ya CDF mstaafu kuhusu waliotaka kupindisha katiba ili Rais Samia asiapishwe inanipa picha halisi ya kwanini Bashiru na wenzake walitenguliwa

Nani sasa alimwambia kuwa makamu ndiyo anastahili kutangaza kifo Cha Rais?
Baada ya mashauriano marefu ndo ikaonekana kuwa ni makamu wa raisi pekee ndo mwenye mamlaka ya kutangaza kifo cha kiongozi mkuu yoyote wa serikali, na sio KM kiongozi wala Prime minister. Hivyo makamu akaapewa taarifa na baadae akatangaza kifo hicho.
 
Kweli kabisa kaka.
 
Ni ajabu sana kwamba siku za mwisho hadi Pombe anazidiwa kiasi hicho, VP alifichwa sinema nzima. Ningetegemea awe na taarifa kuhusu maendeleo ya matibabu ya boss wake. Kwa nini wamfiche mtu ambae kikatiba alitakiwa kuchukua madaraka baada ya Pombe kuzima?
 
MZee kaeleza kisomi sana kwa mtu mwenyr Ufahamu ataelewa na ataweza kuconnect kwanini hata alikuwa anasema kuwa Hakukuwa na connection ya Moja kwa moja kwa makamu na yeye zaidi ya Rais labda kwenye occasion maalumu...

Ni wazi Kuwa wote hawakumtaka sa100 na ndo maana hata taarifa wakitoa kwanza Dodoma...
Na ndo maana nikisoma uzi wa Yoga nikisililiza na story ya Mobeyo napata sana mawazo
 
Huwa nakaa chini najiuliza.
Taarifa aina hii za yaliyopita na kufa huko zinapokuwa public debate. je zinasaidia kukwamua mkwamo wa inflationa na ombwe la kiuongozi tulilo nalo leo?

Tulishaona panga pangua za kutosha na sisi tulishasema huko awali kwamba hao waliotenguliwa wana fununu za kutaka kupindua meza. Yalishapita hukooo.

Hatutakaa tupige hatua za maendeleo kama nchi endapo tunaendekeza hizi tabia za maneno maneno yasiyo na impact kwa hali ya nchi inayopitia kwa sasa
 
Babu ndo ujue ninkuongeza nyama kwenye 2025
 
Raisi mwenyewe mbona uwa anagusia hilo tukio mara kadhaa. Juzi tu alipokuwa Dar kupongezwa siku ya wanawake kaliongelea tena kuna watu walikuwa wanaulizana ataweza kweli kabla kuapishwa kwake.
Waliokuwa wanaulizana kama ataweza, ndio hao waliotupwa nje muda mfupi baada ya msiba kuisha.
 
Babu ndo ujue ninkuongeza nyama kwenye 2025
Hahahah
Katika tafakuri nawaza labda mtoa hoja angeweka maswali yenye kuibua fikra tunduizi kwenye kufahamu kwa nini CDF, IGP na DGIS walikuwa ndiyo wamekizunguka kitanda alicholazwa Rais badala ya watu walioainishwa kwenye Katiba kuwa ndiyo waratibu wa kila hatua?

Je, nchi inaendeshwa kwa mujibu wa mwongozo wa Kijeshi? Maana tunaunga nukta kuhusu ushiriki wa Mfumo na Polisi kwenye mchakato wa uchaguzi na kupiga kura.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…