Kauli ya CDF mstaafu kuhusu waliotaka kupindisha katiba ili Rais Samia asiapishwe inanipa picha halisi ya kwanini Bashiru na wenzake walitenguliwa

Kauli ya CDF mstaafu kuhusu waliotaka kupindisha katiba ili Rais Samia asiapishwe inanipa picha halisi ya kwanini Bashiru na wenzake walitenguliwa

Kwa uhaini huo huyo Bashiru hakutakiwa kuwa hai, achili huo Ubunge. Alikuwa na malengo gani na yenye maslahi ya kina nani?
Bashiru huyu aliyerudisha mali za CCM zilizowashinda vigogo wa chama asingekubali kutoa bure rasilimali za nchi. Wala Bashiru sio kilaza, hata kama humpendi utakubaliana na hilo.

Bashiru sio mtu wa kulalamika na kukosa maamuzi au asijue la kufanya. Wala asingesuasua kuendeleza miradi kama bwawa lingekuwa linazalisha umeme muda.

Hata Majaliwa angekuwa nafuu ya sasa. Yani mkuu wa usalama, PM, KM hawakukosea kwa pamoja kuwa na wasiwasi na huyu "kwa kudra za mwenyezi Mungu"
 
Yes ilikuwaje akamwita CDF dakika za mwisho badala ya makamo
Kijana hauelewi kinachojadiliwa hapa.

Huyo CDF alikuwa pale hospital muda wote wa kuugua kwa hayati Magufuli. Makamu yeye alikuwa Tanga kwa ziara maalum ya kiserikali.

Sasa ulitaka amwite mtu ambae yuko Tanga na kumuacha ambae yuko nae pale pale karibu na kitanda chake?
 
Hahahah
Katika tafakuri nawaza labda mtoa hoja angeweka maswali yenye kuibua fikra tunduizi kwenye kufahamu kwa nini CDF, IGP na DGIS walikuwa ndiyo wamekizunguka kitanda alicholazwa Rais badala ya watu walioainishwa kwenye Katiba kuwa ndiyo waratibu wa kila hatua?

Je, nchi inaendeshwa kwa mujibu wa mwongozo wa Kijeshi? Maana tunaunga nukta kuhusu ushiriki wa Mfumo na Polisi kwenye mchakato wa uchaguzi na kupiga kura.....
Kwahiyo ulitaka serikali isimame kuendelea na majukumu yake wakakae kumuuguza mgonjwa?

Mbona hata Lowasa alivyokuwa mahututi raisi aliagiza jeshi likawe karibu na mgonjwa mpaka msiba ulipomkuta. Huo ndio utaratibu wa kiuongozi kijana.
 
Kwahiyo ulitaka serikali isimame kuendelea na majukumu yake wakakae kumuuguza mgonjwa?

Mbona hata Lowasa alivyokuwa mahututi raisi aliagiza jeshi likawe karibu na mgonjwa mpaka msiba ulipomkuta. Huo ndio utaratibu wa kiuongozi kijana.
Ambatanisha hoja yako kwa kutumia sheria ama Ibara ya Katiba.

Kingine kuniita kijana ni kumkosea mke wangu ambaye anaamini mimi ni mzee tayari
 
Habari zenu wanaJF wenzangu, ama baada ya salam ningependa kuendelea na mada yangu hapa jukwaani.

Ndugu zangu kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Wakati raisi Samia alipoingia madarakani, haikupita hata

Bashiru Hakuchukua muda mrefu. Aliondolewa week moja au mbili baada ya mazishi.

Kwa jinsi alivyo Msemaji kabla na baada ya uteuzi... Kimya chake baada ya kutemwa kinafikirisha.
 
Mmeongea yote mmeshau kitu kimoja.
Mzee wa msoga=Samia
Magufuli hakuwa Mtu wa kumuamini kiongozi wake Kwa uharaka, NI dhahiri Kwa wakati ule makamu hakuwa na power yoyte zaidi ya cheo chake cha umakamu Tu, Samia naamini kuchaguliwa kwako haikua option ya Magu, Bali ilibidi iwe hivyo Kwanza ni muslimu, pia ni from kizimkazi, hivyo ilihitajika iwe balanced

Magu bila Shaka hakumuamini mama, hakumuamini Mzee wa msoga.
Aliamini Sana sukuma gang, mabeyo, bashiru n.k Hali iliyofanya taarifa zake binafsi zifichwe.

Kasimu majaliwa ametukosea Sana watanzania, katudanganya kama watoto, juzi tena hapa kwenye msiba WA lowasa katudanganya, kaficha uhalisia wa taarifa za marehemu, kasimu NI chawa yupo radhi afanye chochote kutetea ccm, kutetea cheo chake.
Hili nalo litapita.💔
 
..swali langu ni kwanini Mabeyo hakuwa akimpa taarifa Makamu wa Raisi / Kaimu Raisi.

..kwanini aliwataarifu Waziri Mkuu na Katibu Mkuu kiongozi kabla ya Makamu wa Rais ambaye kwa hali ya kiafya ya Rais alikuwa / alipaswa kuwa KAIMU RAISI?

..Suala la maradhi na kuugua kwa Raisi Magufuli ilikuwa ni jambo linalotakiwa kusimamiwa na Makamu wake.

Kwanza jiulize kwani Ni kazi ya CDF kutoa taarifa kwa viongozi wa kisiasa juu ya kuumwa kwa rais?.

Hapo mlaumu Makamu yeye mwenyewe kwa kushindwa kujisimamia na kuwa incharge.

Kama makamu alikuwa akikaimu madaraka ya rais kwa nini ashindwe kuwaita wahusika wote wampe taarifa juu ya hali ya mkuu wa nchi?

Sioni kosa kwa Mabeyo zaidi ya busara nyingi na uzalendo mkubwa uliotuvusha salama.
 
Kwanza jiulize kwani Ni kazi ya CDF kutoa taarifa kwa viongozi wa kisiasa juu ya kuumwa kwa rais?.

Hapo mlaumu Makamu yeye mwenyewe kwa kushindwa kujisimamia na kuwa incharge.

Kama makamu alikuwa akikaimu madaraka ya rais kwa nini ashindwe kuwaita wahusika wote wampe taarifa juu ya hali ya mkuu wa nchi?

Sioni kosa kwa Mabeyo zaidi ya busara nyingi na uzalendo mkubwa uliotuvusha salama.
Watu wanamlaumu Mabeyo bure tu!

Si ajabu wanataka hata kuona akiuliwa kwa firing squad kwa ‘makosa’ aliyoyafanya.

Given the circumstances, sioni alipokosea.

SMH!
 
..Mabeyo anastahili lawama.

..Kwanini MAKAMU WA RAIS hakuwa mtu wa kwanza kupewa taarifa kuwa Rais amefariki?

..Nimemsikia Mabeyo akisema eti kulikuwa na mjadala wa nani atangaze kifo cha Rais.

..Hivi Mabeyo na usomi wake, kutumikia jeshini kwa miongo kadhaa, na kutembelea nchi mbalimbali, hajui nani ana mamlaka ya kutangaza kifo cha Raisi? Kwamba walihitaji majadiliano?
We nawe kiazi sana,ina maana hujaelewa kwa nini Mobeyo kasema vile? dumb ass!!
 
Mabeyo kwenye hii ishu alitumika tu sidhani kama he saw what was coming, Mabeyo ni pro Magufuli na ndio maana baada ya mwaka tu alipoona mambo yanaanza kuenda mrama, akatangaza kustaafu bila sababu za msingi

Ni wazi pro Magufulis kina Bashiru and co hawakumtaka Mama, maana since day one alishaonesha dalili kuwa ni pandikizi la Godfather ndio maana walitaka kupindisha katiba, ila Godfather akaingilia kati akaamua kumtumia Mabeyo hapo

Akamuambia kwamba waambie hao kina Bashiru and co kuwa tumeshitukia mchezo wao, hivyo waambie wamuapishe huyo Mama haraka iwezekanavyo, kwahiyo ni kama Godfather alitumia advantage ya katiba kwa maslahi yake na genge lake
 
Back
Top Bottom