Kauli ya CDF mstaafu kuhusu waliotaka kupindisha katiba ili Rais Samia asiapishwe inanipa picha halisi ya kwanini Bashiru na wenzake walitenguliwa

#Weak points,
Katiba ndio Muongozo wetu,mlipo mchagua Mama awe makamu wa Raisi hamkuwa na wasiwasi hawezi, yaliyo tokea yametokea Uraisi ni Taasisi , hizo kenge zilizo taka kupindisha Katiba ningekuwa mshauri wa mama wote kwenye system wangekuwa nje wanacheza na vijukuu nyumbani,Tuheshimu Katiba yetu hayo hawezi au ana weza mkenjipanga kabla ya kumpa Umakamo wa Raisi.
 
Mim naona lawama apewe magufuli tu maana yeye ndio alimchagua awe mgombea mwenza.
 
Mabeyo alitangaza tu kustaafu bila sababu za msingi? Seriously? Are you that ignorant?

Hujui kuwa jeshini ma CDF hustaafu kwa mujibu wa sheria muda wao ukifika?

Kwani Davis Mwamunyange na Robert Mbona walistaafu kwa sababu gani za msingi? By the way, hao nao walikuwa ma CDF.

Goodness gracious 🤣.
 

Nawafahamu CDFs wote mkuu ila kustaafu kwa Mabeyo kuliibua maswali kadhaa kwa waliokuwa wanajua kinachoendelea, ila mwisho wa siku Jibu likawa tu "amestaafu kwa mujibu wa sheria", na wengi kama wewe waliamini kuwa kweli Mabeyo alistaafu kwa mujibu wa sheria, hivyo nilitegemea comment kama hii wala sishangai, ila acha ibaki hivyo hivyo mkuu
 
Yale mahojiano pengine yamefanywa kwa wema ila yameniacha na maswali mengi sana juu ya uongozi wa nchi yetu na hatma ya Katiba yetu.

Ina maana wakati wote wa ugonjwa hadi rais hawezi tena kuongea, nani alikuwa anaongoza nchi?
 
Wataka kusema Sa100 alikwenda Tanga na kukaa kule bila kufahamu kinoendelea?
 
Yale mahojiano pengine yamefanywa kwa wema ila yameniacha na maswali mengi sana juu ya uongozi wa nchi yetu na hatma ya Katiba yetu.

Ina maana wakati wote wa ugonjwa hadi rais hawezi tena kuongea, nani alikuwa anaongoza nchi?
Sikiliza tena alokisema Mabeyo ametumia misamiati kadhaa kukujulisha ni nani walikuwa wasimamizi wa shughuli nzima.

Yeye alibaki kama mtazamaji au tuseme mwamuzi wa mpira au VAR.
 
Umesema alistaafu bila sababu za msingi. Sawa….sababu za msingi za CDF kustaafu ni zipi?

David Musuguri, Ernest Kiaro, Robert Mboma, George Waitara, na Davis Mwamunyange walistaafu kwa ‘sababu’ gani ‘za msingi’ zilizo tofauti na sababu za Mabeyo kustaafu?

Nataka tu kujua hizo sababu za msingi kwa lengo la kujifunza. Nitashukuru ukinifahamisha maana yawezekana mimi sizijui. Napenda kujifunza mambo mapya.
 
Kama nchi, tujitafakari sana namna ya kupata Makamu wa Rais.
Nimewahi kusema tena humu, kwasababu ya ubinafsi wa watu wanaoteuliwa kugombea urais hasa ndani ya CCM, huwa wamekuwa na utaratibu wa kuteua wagombea wenza wenye ushawishi mdogo ndani ya chama na hata kwa wananchi.

Kwa lugha nyepesi ni kwamba, marais wamekuwa wakipenda makamu wa rais ambao hawawezi kuwafunika. Si unaona hata Rais wa sasa alimteua mtu gani kuwa makamu wake?

Upatikanaji wa makamu wa rais unapaswa kuzingatia kwamba, huyu mtu muda wowote anaweza kuwa Rais wa nchi!
 
Ww ndio umetoa most weak point
 
Lakini umesahau JPM alisema yeye alimtaka nani awe makamu ( na sio Sa100) wake na alisema hiyo ilikuwa ni siri ila msukuma akaisema hadharani.
 
Sikiliza tena alokisema Mabeyo ametumia misamiati kadhaa kukujulisha ni nani walikuwa wasimamizi wa shughuli nzima.

Yeye alibaki kama mtazamaji au tuseme mwamuzi wa mpira au VAR.
Mkuu, nimefuatilia labda kama kuna kipanda nimekosa unisaidie kufafanua.

Kama tunafuata Katiba, Makamu wa rais ni mtu wa pili kimamlaka katika nchi yetu. Rais anapokuwa mgonjwa, usukani anatakiwa kuwa nao makamu wa rais mpaka rais akae sawa na aweze kutekeleza majukumu yake. Wakati wote wa matibabu, wanaomtibu Rais wanapaswa kutoa taarifa na maendeleo ya afya yake kwa Makamu wa rais kama mtu wa pili kimamlaka katika nchi.

Itoshe tu kusema, simulizi yote ya Rtd CDF wetu imenijuza nisichojua mimi Mfugaji wa huku kijijini kando kando ya Tanzania!
 
Mkuu kama labda hujawahi kufanya kazi kwenye taasisi yeyote..!!lakini katika watu 3 viongozi lazima wawili watajikata na kuwa wasiri na kumtenga 1...na ndo ilivyokuwa kwa jpm...MAMA hakuwahi kuaminiwa hata siku moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…