Kauli ya CDF mstaafu kuhusu waliotaka kupindisha katiba ili Rais Samia asiapishwe inanipa picha halisi ya kwanini Bashiru na wenzake walitenguliwa

Mkuu kama labda hujawahi kufanya kazi kwenye taasisi yeyote..!!lakini katika watu 3 viongozi lazima wawili watajikata na kuwa wasiri na kumtenga 1...na ndo ilivyokuwa kwa jpm...MAMA hakuwahi kuaminiwa hata siku moja
Na Makamba Jr alisema kuna watu hata kuwasalimia (wakati huo akiwa waziri katika ofisi ya Makamu wa rais) tu ilikuwa ngumu.
 
Unaposema Magufuli hakuwa mtu wa kumuamini kiongozi wake unamaanisha nini na wakati mwenyewe ndio aliemchagua tena 2020 awe mgombea mwenza, huku Magufuli mwenyewe akiwa ndio mwenyekiti wa chama na raisi wa nchi?
Swala la dini na ukizimkazi hilo halina mantiki yoyote, maana hata baraza lake la mawaziri lilikuwa na 90% ya mawaziri wasiokuwa waislam na bado hakuna aliemletea tatizo au kushindwa kumchagua.

Pia makamu alikuwa na power kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi, labda wewe unazungumzia power ya kunyanyua mavyuma au ile ya kufokea fokea watu hovyo ndo ionekane una power kwa wale unaowafokea fokea.
Kuhusu Majaliwa kuwadanganya hilo ni kawaida kwa 85% ya watanzania kuwa waongo. Au umesahau kashfa ya fisadi papa Lowasa aliyovikwa na viongozi wote wa chadema, lkn baadae ikaja kudhihirika kuwa waliudanganya umma wa watanzania? Je na wao walikufanya mtoto mdogo?
 
Nakumbuka, lakini alisema alikuwa na machaguo mawili. Hata hivyo kama hakuja kumpenda, 2020 alikuwa na nafasi ya kubadilisha kwakuwa hakuwepo wa kumzuia.
Hakuwa na chagua tayari alikuwa na chaguo lake lakini akashauriwa ( na kwa kutofahamu hila akakubali) na badala yake akawa Sa100.

Haya mambo hayahitaji Phd kuyadadavua ni kuunganisha dots tu.

Hivyo akiwa hoi akaona nchi yarudi kulekule na kwa kutaka kuyaendeleza aloyaanza akasahau kwamba kuna katiba na akataka BHR (yaani kiaina kuwe na serikali ya muda)awe makamu na ndipo zogo lilipoanza.

Zogo lilikuwa ni kubwa kwelikweli na kulikuwa na patashika nguo kuchanika.

Kwa hilo CFD alitekeleza jukumu lake la kusimamia katiba.

Ila kiukweli kwenye nchi yenye mfumo wa Kleptokrasia ni lazima wababe aka wapigaji wangeshinda.
 
Watu wanamsifia mobeyo ila kwa wachache tuliosomea Cuba tunaona hata yy alikua kwenye Dillema, na nahisi anajilaumu
 
Ile kiini macho tu ili kubalance ishu za dini na jinsia ,ila magu hakumkubali huyo mama ndo maana mambo mengi alipiga mwenyewe.
Hilo wala halina mashiko. Kama ni jinsia mbona angeweza kuchagua mwanamke mungine kutoka Zanzibar, inamaana Zanzibar nzima mwanamke alikuwa ni huyo huyo mama Samia?

Pia hakuna wanawake wengine waislam kule Zanzibar?
 
Una hoja
 
Hawawezi kumtaarifu kwa sbb hakuwa sehemu ya kamati ya ulizi na usalama.Kumbuka hiyo kamati ingeamua kuchukua nchi kulikuwa hakuna jinsi
 
Nakumbuka, lakini alisema alikuwa na machaguo mawili. Hata hivyo kama hakuja kumpenda, 2020 alikuwa na nafasi ya kubadilisha kwakuwa hakuwepo wa kumzuia.
Asante sana kwa comment hii. Hata na mimi nilimueleza jamaa hapo juu namna hivi hivi ulivyoandika.
 
Nadhani upo sahihi mkuu
Hata hii clip ukijuliza Why? na kutafakari kwa makini utaona kuna ujumbe na pengine majuto pia. Sikilizeni kwa makini na mjiulize kwa nini yamesemwa yaliyosemwa na aliyesema
 
Jiulize kama alijua makamu ndie second kwa nn wamuite waziri mkuu kwanza? Je na yy alikua anaingiwa na kile kishawishi cha kina bashiru?

Ningekua Mobeyo ningekaa kimya tu, nikala benefit of the doubt
Yeye alijua katiba inasema makamu anakuwa Rais so huwezi kumtaarifu haraka sbb kiusalamanhuwezi kujua kama issue ya kumuondoa jiwe ilikuwa imeandaliwa na kuratibiwa na makamu kwa manufaa yake hivyo unamuweka pembeni ili kupata taarifa za usalama zaidi za nchi la sivyo mkienda kifala nchi inaweza vamiwa na wao wangeuawa na group jingine,,so ni strategy Bora amabyo mabeyo wliifanya
 
Sababu mojawapo nimeshaizungumzia pale kwenye comment yangu ya kwanza mkuu, it is up to you to take it or leave it, Mabeyo alitumia sababu ile ile ya siku zote na utaratibu ule ule wa ma CDF kustaafu

Lakini nyuma ya pazia hiyo haikuwa sababu kubwa, 'Wahusika' wanadai yeye na Magufuli walishapanga mwaka atakaostaafu, (endapo angeendelea kuwa hai) ambapo haikutakiwa kuwa 2022

Na CDF mpya alikuwa ameshaandaliwa Major General Charles Mbuge, ambaye naye alikuwa ni pro Magufuli, ndio maana kustaafu kwa Mabeyo kuliibua maswali kwa waliokuwa wanajua kinachoendelea
 
Jiulize kama alijua makamu ndie second kwa nn wamuite waziri mkuu kwanza? Je na yy alikua anaingiwa na kile kishawishi cha kina bashiru?

Ningekua Mobeyo ningekaa kimya tu, nikala benefit of the doubt
C'moon wadhani alikuwa hafahamu kweli?

Ni uchu wa madaraka ulikuwa katika "despetare state".

Ni pale usemapo kuna vita katika viambaza vya utawala, "desperate measures in desperate times".

Na si kwambani yeyeapewe sifa kwa kutuliza hali bali ni kufikia muafaka baina ya makundi mawili yenye malengo tofauti.

Ni dhahiri kundi lenye nguvu kwa kila kitu ndilo loloshinda.
 
Pengine Wewe kuna kitu unakijua wengine hawakijui, hivyo ni vigumu mkawa sawa kimtazamo. Pengine potezea tu kwani hivyo waaminivyo ndivyo inapaswa iwe hivyo ili mambo yaende.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…