Kauli ya Chongolo ni ufedhuli kwa wasomi wa vyuo vikuu. Ipingwe!

Mimi ningeshauri serikali kwa vile vyuo vyetu vingi havina sehemu za kufanyia tafiti (research centers) basi watu waliokaa kwenye kazi (field) kwa muda mrefu sana ndo warusishwe vyuoni wakafundishe siyo mtu amebakishwa tutorial..within 5years tayari ni lecture kisa amechukua masters na phd tayari. mfano. Akina Kibatara and likes wakatoe elimu ya sheria huko chuo kikuu..

Wale wataalam wanaotengeneza mitambo ya gesi pale kinyerezi na waotengeneza and the likes wakafundishe chuo kikuu.

Wale wahasibu wabobezi warudi wakafundishe.
Wale wataalam wa mabarabara na ujenzi walioko kwenye field muda mrefu wakafundishe.

Wale miners wabobezi kule GGM na Nyamongo warudishwe wakafundishe...

Tuachaneni na Hao wahadhiri ambao vichwa vyao vimeota kutu na hawafanyi vitu kwa vitendo kwasababu hawaoni vitu katika uhalisia...tuchukue watu waliopo kwenye field. Haiwezekani mwanafunzi amemaliza chuo lakini akipewa mtihani kwa vitendo anaonekana kichekesho..
 
Mwalimu wa VETA ANAFUNDISHWA NA VETA CHUO KIPO MOROGORO acha kupotosha na hili uwe mwalimu wa veta lazima usome ufundi au fani usika kwa miaka mitatu level 3 then una enda Morogoro miaka miwili kusomea ualimu wa ufundi
 
Nainga kauli yake mkono. Hatujuwi kazi nyingine wasomi hii ni hatari. We will die masikini sana
 
Yaani Chongolo anawafanya ninyi wasomi wenye madigrii kuwa ni mbumbumbu kuliko kijana wa darasa la nne aliyehitimu ufundi uashi?
Hatari na nusu basi vyuo vifungwe watu waende veta wakimaliza la 7
 
Ndio Maana wameambiwa wakasome VETA Ili wajifunze mbinu za uzalishaji.
Kuna mafunzo ya kusindika vyakula. Ufundi Wa Simu, Kushona viatu, Kushona nguo. Hiví msomi akiamua Kushona suti Kwa kiwango Cha kushindana na suti Toka China hawezi kuendesha MAISHA yake na akatoka. Suti zinauzwa mpaka laki Saba.

Kuna Kozi nyingi za uzalishaji hazifundishwi vyuo vikuu.
Vyuo vikuu vinatengeneza wataalam waelekezaji au wasimamizi hivyo wakikosa Ajira inabidi wajifunze kujiajiri na kujiongoza na kujisimamia katika uzalishaji.
 
Nainga kauli yake mkono. Hatujuwi kazi nyingine wasomi hii ni hatari. We will die masikini sana
Nani kakuongopea? Kuna kazi hazihitaji ujuzi km zile za kujaza makaratasi ya wahudhuliaji, zinahitaji ujuzi upi record management kwan hawafundishwi chuoni?
 
Kama zipi zitaje au unazungumzia ufundi bomba, kuchomelea mageti na kupaka rangi ukuta?
 
Wew? Nani kasema huwezi kujiajiri?
 
Mwalimu wa VETA ANAFUNDISHWA NA VETA CHUO KIPO MOROGORO acha kupotosha na hili uwe mwalimu wa veta lazima usome ufundi au fani usika kwa miaka mitatu level 3 then una enda Morogoro miaka miwili kusomea ualimu wa ufundi
Umeshaoma matangazo ya Utumishi kuhusina na walimu wa kwenda kufundisha VETA?
 
Unataka mtu aliyesoma Political science, Medicine, au Accounting akafanye kazi za fundi bomba au fundi ujenzi?
 
Chongolo ameshiba sana
 
Sasa si angesema tu watu waache kwenda vyuo vikuu kusomea masomo ya sanaa na sayansi kwa sababu hakuna ajira zake badala yake wakimaliza kidato cha nne wa veta moja kwa moja?!
Kuna haja gani ya kupoteza mamilioni au kuwafanya watu waingie katika madeni makubwa ya mkopo wa chuo kikuu wakati lengo kuu kwa wote ni kurudi kuja kufanya "kazi za mikono" za fundi bomba, ujenzi na useremala??
 
Sasa kwanin wasibadili mitaala ili mtu akimaliza chuo kikuu awe full package kuliko kusoma chuo miaka mi 4 halafu arudi asome tena veta nawadogo zake
 
Kwa kauli yake ni kwamba hakuna sababu yakuwa na vyuo vikuu. Huwezi kumwambia Mwanachuo aende vyeta ili aweze kujiajiri.
Kwa lugha nyepesi CCM imeshindwa kujenga Taifa Linaloenda na Wakati.Haifai Kuendelea Kuongoza.
 
Huko vyuo vikuu asilimia kubwa ya mafunzo hasa wanaochukua masomo ya sanaa na hata sayansi hakuna ujuzi wa mikono unaofundishwa zaidi ya kukariri vitini!!!!!!!!!!!!!
Nani mwenye wajibu wa kuhwkikisha wanafunzi wanafanya masomo ya vyuo vikuu kwa vitendo? Chongolo na ccm yake ndiyo wameiharibu elimu ya chuo kikuu kwa kuifanya isiwe tofauti na ile ya sekondari.


Alichoikiongea Chongolo ni upuuzi. Duniani kote bunifu na tafiti za kitaslamu hufangwa na wahitimu wa vyuo vikuu. Kwann iwe tofauti hapa kwetu? CCM wamelikoroga Sasa hawataki kulinywa wanalikimbia
 
Mjumbe anatapika halafu anayala tena. Chongolo kasema nenda VETA jifunze umekanika ujiajiri. Wewe una BSc Mechanical Engineering unajisikia vibaya kuambiwa kwenda VETA? Ni kwa sababu digrii yako ni feki. Mtu mwenye digrii ya kweli ya umekanika hawezi kwenda VETA vile yote yaliyoko VETA anayajua. Shida ni kiburi kuwa ni msomi na kutojituma. Kuna imani potofu kuwa Jamii inatakiwa ikupe kazi. Serkali haina ajira zaidi ya watumishi wake wachache, haina gereji, shamba, nini kinakufanya udhani kuwa inawajibika kukuajiri? Vijana wapuuzi wanadanganywa na CHADEMA kuitukana CCM mbowe kasema tatizo ni tumehuru. Si nendeni kutafuta tumehuru iwape ajira kwenye gereji ya tume?
 
Kama zipi zitaje au unazungumzia ufundi bomba, kuchomelea mageti na kupaka rangi ukuta?
Veta Kuna Kozi nyingi.
Kwani.

Kwani kuendesha basi la Mwendo Kasi unaweza kuipata chuo kikuu.?

Kuendesha mitambo kule migodini, kuendesha madumper na exavetor,ni kazi zenye maslahi mazuri kuliko kukaa na Cheti Cha digrii bila ujuzi Wowote ZAIDI ya theories tu na kukariri hotuba za watu mashuhuri tu. Umejaza kichwani hotuba na falsafa za Pilato ambazo hazina Mchango Wowote kwenye uzalishaji unapokosa Ajira.

Veta Kuna Kozi nyingi ambazo msomi Wa chuo Kikuu angeweza kuzipata angeweza kuajiri watu wengine kutokana na KUWA na Upeo Mkubwa ZAIDI .
Mfano ufundi Wa kuchomelea mageti na kutengeneza vitanda n.k . Ni Ajira KUBWA sana na imeajiri watu wengi tatizo unafanywa Kienyeji sana ,uchochoroni, hakuna ofisi za maana n.k lakini wasomi wangeteka fani hizo zinagekua na ushindani na kuua vitu dhaifu kutoka nje.

Hivi unategemea viatu kutoka itali vinatengenezwa na watu wasio na Elimu kubwa ?
Wasomi ni wakati Sasa wa kujiajiri bila kuchagua kazi.

Nenda Moshi Kuna madereva na makondakta Wana digrii. Hata ukiwaangalia wanavyojiheshimu utaona tofauti na wengine. Wana Bima ya Afya ,NSSF ,free lunch n.k. Madereva Wengi Sasa Wana miliki fuso zao. Wasomi wanaona kusafrisha abiria au mizigo Kwa Ndege au Meli ni jambo la hadhi sana kuliko magari lakini vyote ni vyombo vya usafririshaji. Mmoja ameitwa rubani ,Mwingine Dereva ,Mwingine nahodha au captain .

Wasomi wengi wa vyuo vikuu vya Tanzania wanataka pesa za haraka haraka ndio maana wengi wamekimbilia kwenye bodaboda.
 
Kama ndio hivyo hawa vijana wa sasa walio kidato cha nne na cha sita washauriwe wakimaliza shule waende VETA kwanza kabla ya kujiunga na vyuo vikuu.
Kama Chongolo anaona nchi imeshindwa kutengeneza ajira za vijana wanaotoka vyuo vikuu katika taaluma za Bcom, Social Sciences, Engineering, Medicine n.k aseme wazi tu na aeende kwenye mzizi wa matatizo badala ya kusubiria wamemaliza vyuo vikuu ndo anawaambia warudi chini kujifunza ufundi bomba na useremala tena. Hii ni kuwapoteza pesa na muda.
Yuko sahihi
Kusoma VETA sio dhambi.
Wala Uhalifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…