Veta Kuna Kozi nyingi.
Kwani.
Kwani kuendesha basi la Mwendo Kasi unaweza kuipata chuo kikuu.?
Kuendesha mitambo kule migodini, kuendesha madumper na exavetor,ni kazi zenye maslahi mazuri kuliko kukaa na Cheti Cha digrii bila ujuzi Wowote ZAIDI ya theories tu na kukariri hotuba za watu mashuhuri tu. Umejaza kichwani hotuba na falsafa za Pilato ambazo hazina Mchango Wowote kwenye uzalishaji unapokosa Ajira.
Veta Kuna Kozi nyingi ambazo msomi Wa chuo Kikuu angeweza kuzipata angeweza kuajiri watu wengine kutokana na KUWA na Upeo Mkubwa ZAIDI .
Mfano ufundi Wa kuchomelea mageti na kutengeneza vitanda n.k . Ni Ajira KUBWA sana na imeajiri watu wengi tatizo unafanywa Kienyeji sana ,uchochoroni, hakuna ofisi za maana n.k lakini wasomi wangeteka fani hizo zinagekua na ushindani na kuua vitu dhaifu kutoka nje.
Hivi unategemea viatu kutoka itali vinatengenezwa na watu wasio na Elimu kubwa ?
Wasomi ni wakati Sasa wa kujiajiri bila kuchagua kazi.
Nenda Moshi Kuna madereva na makondakta Wana digrii. Hata ukiwaangalia wanavyojiheshimu utaona tofauti na wengine. Wana Bima ya Afya ,NSSF ,free lunch n.k. Madereva Wengi Sasa Wana miliki fuso zao. Wasomi wanaona kusafrisha abiria au mizigo Kwa Ndege au Meli ni jambo la hadhi sana kuliko magari lakini vyote ni vyombo vya usafririshaji. Mmoja ameitwa rubani ,Mwingine Dereva ,Mwingine nahodha au captain .
Wasomi wengi wa vyuo vikuu vya Tanzania wanataka pesa za haraka haraka ndio maana wengi wamekimbilia kwenye bodaboda.