Kauli ya Chongolo ni ufedhuli kwa wasomi wa vyuo vikuu. Ipingwe!

Kauli ya Chongolo ni ufedhuli kwa wasomi wa vyuo vikuu. Ipingwe!

yuko sahihi , ila kuna wakati nashangaa kwa nini serikali inashindwa kuajiri walimu hasa shule za kata unakuta shule mwalimu wa hesabu mmoja shule nzima au fizikia.
 
Kwani unadhani wanaotoa ushauri kuhusiana na unyanyasaji wa kijinsia pamoja na kusaidia jamii namna bora ya kfungua na kuanzisha miradi ya kujikwamua kama vile kuanzisha vikundi, namna ya kupata mikopo kwa ajili ya makundi, kuandika andiko ili waweze kusajiliwa, kuandika katiba pamoja na kujisajili.

kazi ni nyingi sana...sema mnajua kazi za ki ufundi.
Sasa why mfungui hizo ofisi ili muwe mmejiajiri?.
 
Kama ndio hivyo hawa vijana wa sasa walio kidato cha nne na cha sita washauriwe wakimaliza shule waende VETA kwanza kabla ya kujiunga na vyuo vikuu.
Kama Chongolo anaona nchi imeshindwa kutengeneza ajira za vijana wanaotoka vyuo vikuu katika taaluma za Bcom, Social Sciences, Engineering, Medicine n.k aseme wazi tu na aeende kwenye mzizi wa matatizo badala ya kusubiria wamemaliza vyuo vikuu ndo anawaambia warudi chini kujifunza ufundi bomba na useremala tena. Hii ni kuwapoteza pesa na muda.
Kweli wa JKT waende na VETA waende iyo miezi 3 na cheti juu .
 
Elimu ni ujuzi au maarifa unayopewa ili upambane na mazingira yako,

Kama umefika huko panapoitwa Chuo na ukahitimu labda Shahada ya Uchumi lakini miaka 3 au 4 baada ya kuhitimu ukakosa ajira ya kujiajiri au kuajiriwa,ukaona ngoja uende Veta ukapate mafunzo ya Udereva na Ufundi Makanika mbona utakuwa umejiongezea kitu muhimu katika maisha yako na tena unaweza ukapata ajira kupitia mafunzo ya Veta kwa haraka kuliko hilo li karatasi lako la Chuo,
Vijana wa Kitanzania mliopo Vyuo acheni Upumbavu wa kujiona nyinyi ni kundi muhimu sana kuliko mtu yoyote,kufika Chuo haimaanishi huwezi kuwa Fundi Mwashi,Mchomeleaji au Seremala.

Nchi zilizoendelea mtu mmoja unamkuta ana Shahada na bado ana vyeti vidogo hata 10 vya kazi za mikono,hapa Tanzania mtu ukifika tu Chuo basi wewe ni Elon Musk,

Chongolo yupo sahihi,wanachuo acheni ulonyolonyo nendeni Veta!
 
Mjumbe anatapika halafu anayala tena. Chongolo kasema nenda VETA jifunze umekanika ujiajiri. Wewe una BSc Mechanical Engineering unajisikia vibaya kuambiwa kwenda VETA? Ni kwa sababu digrii yako ni feki. Mtu mwenye digrii ya kweli ya umekanika hawezi kwenda VETA vile yote yaliyoko VETA anayajua. Shida ni kiburi kuwa ni msomi na kutojituma. Kuna imani potofu kuwa Jamii inatakiwa ikupe kazi. Serkali haina ajira zaidi ya watumishi wake wachache, haina gereji, shamba, nini kinakufanya udhani kuwa inawajibika kukuajiri? Vijana wapuuzi wanadanganywa na CHADEMA kuitukana CCM mbowe kasema tatizo ni tumehuru. Si nendeni kutafuta tumehuru iwape ajira kwenye gereji ya tume?
Poyoyo.
Nchi ipo chini ya CCM Alafu Mnajitekenya nakucheka wenyewe
 
Mtoa mada nahisi uelewa wako ni mdogo na unapenda kukurupuka.Punguza mhemko na papara.Bandiko lako lote limekosa mantiki.

Kupata ajira kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa changamoto karibu dunia nzima!!!!!!!!!!Kwa utamaduni wa elimu yetu humuandaa mwanafunzi kuajiriwa, kwamba ukimaliza masomo yako utakutana na ajira!!!!!!!!!! Hizi zama zimepita na hazitarudi tena!!!!!!!!!!!

Ajira zimekuwa ngumu lakini shughuli za kufanya ziko nyingi!!!!!!!!!!!!!!! Huko vyuo vikuu asilimia kubwa ya mafunzo hasa wanaochukua masomo ya sanaa na hata sayansi hakuna ujuzi wa mikono unaofundishwa zaidi ya kukariri vitini!!!!!!!!!!!!!

Huyu mhitimu akitoka huko hatakuwa na uwezo mkubwa wa kujishughulisha na shughuli mbalimbali ambazo nyingi hutumia ujuzi wa mikono!!!!!!!!!!!

Veta kuna mafunzo mbalimbali ya muda mfupi sana na muda mrefu ambayo kwa kiasi kikubwa hutumia ujuzi wa mikono ambao haupatikani kwa wanafunzi wengi huko vyuoni. Mfano wa mafunzo hayo ni:

Masonry & Bricklaying (MB)

Carpentry & Joinery (CJ)

Road Construction & Maintenance (RCM)

Civil Draughting (CD)

Painting & Sign writing (PS)

Welding & Fabrication (WF)

Fitter Mechanics (FM)

Meat Processing Technology (MPT)

Electronics (ELEC)

Motor Vehicle Mechanics (MVM)

Electrical Installation (EL)

Food Production (FP)

Food & Beverage Services & Sales (FBSS)

Front Office Operations (FO)

Plumbing & Pipe fitting (PPF).

Ukipata haya mafunzo ambayo huchukua muda mfupi utakuwa na uwanda mpana wa kujishughulisha wakati unasubiria muujiza wa ajira!!!!!!!!!!!

Nb 1: Zama zimebadilika. Tujifunze kubadilika!!!!!!!!!

Nb 2: Maarifa ya darasani hutumika kidogo sana mtaani!!!!!!!!!!!!!!

Nb 3: Mtaa una kanuni, sheria na taratibu zake ambazo hutafundishwa chuoni!!!!!!!!!!

Ni mtazamo!!!!!!!!!!!!!!!!
Ipi afadhali, VETA au tumehuru? According to Mr Tundu all these problems of ajira and ugumu wa maisha na bei kupanda, jibu lake ni tumehuru.
 
Weka ushabiki wa kivyama pembeni, utaona mantiki halisi ya aliyoysema Katibu Mkuu huyo.

Kuwa na digrii si hoja, hoja ni kuwa na uwezo wa kujiajiri.

Mtu mwenye ujuzi wake toka Veta wa kuunganisha mabomba ya maji taka, na mtu aliye na digrii ya political sayansi ni yupi aliye na urahisi wa kujiajiri mwenyewe?

Na itanoga zaidi, kama huyu msomi wa political sayansi akawa na ujuzi wa kutengeneza vitu na kuitumia kwa upana zaidi hiyo digrii yake, badala ya kukaa nayo tu akiilea huku akiwa tegemezi kwa wengine.

Digrii kwa siku hizi siyo nyenzo tena ya kupatia kazi.
Kwahiyo Chongolo anataka vijana wote wa vyuo vikuu wawe mafundi mchundo ??

Muwe mnaangalia mantiki ya hoja iliyotolewa kwanza kabla ya kukimbilia kuunga mkono hoja mfu.

Daniel Chongolo anapowaambia vijana wa vyuo vikuu waende veta wawe na uwezo wa kujiajiri maana yake elimu yao ya chuo kikuu haina maana yoyote isipokuwa elimu ya veta na kwamba chuo kikuu wamepoteza muda wao bure.

Kuna la maana hapo ??
 
Vitendo katika fani ipi?Anayesomea maendeleo ya jamii anaweza fanya mafunzo ya vitendo vipi ili mtaani ajiajiri?.
Kuna fani zilipaswa kufutwa vyuoni Kama tungekuwa serious. Kama ccm inajua fani hizi hazina practical application mitaani kwann zifundishwa?? CCM ni wangese
 
Isomi wako usio na Tija una manufaa gani Kwako na jamii zaidi ya kuwa mzigo?
Aliyesababaisha niwe mzigo ni ccm. Walipaswa wawekeze vya kutosha ktk vyuo vikuu ili wanafunzi wasome kwa vitendo na siyo kuhubiriwa na kupewa notes tu darasani. Chongolo anapaswa kuwajibika ktk hili.
 
Msomi ndiyo ulipaswa utengeneze PRIVATE SECTOR ndani ya nchi na nje ya nchi,lakini eti wewe unawaza watu waje toka nje ya nchi ndiyo wa anzishe PRIVATE SECTOR ndiyo wewe uajiriwe!.Aisee!Hii ni aibu kwa msomi kuwa na mawazo ya aina hii.
Kwani Singapore wasomi ndo walitengeneza Google?
Sera nzuri ya Serikali ya Singapore iliwaruhusu Google kuja kufungua ofisi nchini kwao na kutengeneza ajira.
 
Mkuu siyo kwamba ni yeye hataki tu kufanya bali ni hajui kabisa kutenda.Mimi nimefanya kazi na wahandisi wa umeme miaka ya 2000 huko,yaani muhandi hajua jinsi ya kubadili ballistic chock katika tubelight flame!?.
Mwengini alishindwa kupima ufanisi wa three phase earthing katika project yake.Baada ya kangaika kwa muda mrefu bila mafanikio,ndiyo akaelekezwa kuja katika ofisi yetu ili kumpa msaada.
Kifipu mambo bado ni magumu kwa wasome wetu.
Kuna shida tu kwenye uandishi wako na unataka utuaminishe ulichokiandika?
 
Mfumo mbovu kwani ni mfumo unique au ndio mifumo ya Dunia?
We mjinga sikiliza. Vyuo vikuu kutoa degree za mahubiri bila vitendo siyo mfumo wa dunia. Nenda kasmea hata diploma tu huko nje utaiona tofauti.

Tatizo lako umesoma chekechea mpk kidoto cha 6 huko Matipwinyo Nanguruwe. Halafu ukaenda kuchukua "digrii" Tandabui University
 
Chongolo amewataka wasomi wa vyuo vikuu kwenda veta ili wakapate uwezo wa kujiajiri.

Kauli hii inatoa tafsiri hasi nyingi sana dhidi ya wasomi wa vyuo vikuu na vyuo vikuu vyenyewe.

Mosi, inatoa tafsiri kwamba elimu ya vyuo vikuu ni dhaifu ukilinganisha na ile ya veta. Kama hivi ndivyo. Je, malengo ya utoaji wa elimu ya vyuo vikuu yamefikiwa? Ikiwa bado hayajafikiwa ni nani wa kulaumiwa, kama siyo CCM na wanaccm?

Pili, inatoa tafsiri kwamba waliohitimu veta wana uwezo wa kujiajiri kuliko waliohitimu vyuo vikuul. Binafsi naona kuwa haya ni madhara ya kusema kabla ya kufanya utafiti. Huku mitaani tunaona watu wengi waliojiri ni wale ambao hawajaenda veta wala vyuo vikuu.

Sasa Chongolo atuambie hawa waliupata wapi uwezo huu? Je, ni shule ya msingi? Kama ndivyo atoe kauli nyingine.

Natoa wito kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vyote nchini kuandaa maandamano kupinga kauli hii inayotweza na kuidhalilisha elimu ya daraja la juu kabisa duniani. Mkikaa kimya CCM haikawii kuwafanya muonekane kama wahitimu wa darasa la saba.

Yaani Chongolo anawafanya ninyi wasomi wenye madigrii kuwa ni mbumbumbu kuliko kijana wa darasa la nne aliyehitimu ufundi uashi?

MSIKUBALI!
Kasema kweli, shida ni kwamba Serikali imewekeza saba kwenye vyuo vikuu badala ya vyuo ya kati, VETA vilitaliwa kuwa ni vyuo vyenye kupata fund ndefu sana kutoka Serikalini lakini sio hivyo
 
Kasema kweli, shida ni kwamba Serikali imewekeza sana kwenye vyuo vikuu badala ya vyuo ya kati, VETA vilitaliwa kuwa ni vyuo vyenye kupata fund ndefu sana kutoka Serikalini lakini sio hivyo
Unajua maana ya kuwekeza Sana?? Ingekuwa imewekeza Sana wanafunzi wangekuwa wanasoma kwa vitendo zaidi kuliko kuhubiriwa.
 
We mjinga sikiliza. Vyuo vikuu kutoa degree za mahubiri bila vitendo siyo mfumo wa dunia. Nenda kasmea hata diploma tu huko nje utaiona tofauti.

Tatizo lako umesoma chekechea mpk kidoto cha 6 huko Matipwinyo Nanguruwe. Halafu ukaenda kuchukua "digrii" Tandabui University
Toa upumbavu wako hapa wewe fala,watu wangapi wamesoma vyo vya Nje na ni jobless hapa Tanzania?
 
Back
Top Bottom