Kauli ya Heche kukosoa Congo kuwekeza Tanzania ina ufinyu wa uelewa

Kauli ya Heche kukosoa Congo kuwekeza Tanzania ina ufinyu wa uelewa

Kwao kuna mto na bahari na nchi isiyokosa mvua na madini yote ya thamani kwa nini waje kuwekeza Tanzania na sio kwao kwenye fursa na soko kubwa saba?
Jicho la biashara haliko namna hiyo, la msingi ni fursa ambayo mtu anaiona. Huo mtazamo ndiyo umefanya Wachagga wanatuzidi sana makabila mengi Tanzania.
 
View attachment 3653552

Kauli ya Heche inaleta dharau isiyostahili kwa viongozi wa Taifa. Kuwaambia “hakuna watu wenye akili na maarifa” si hoja, ni matusi yanayodhalilisha taifa badala ya kujenga. Uongozi una majukumu magumu; kukosoa kwa lugha ya kejeli hudhoofisha heshima ya nchi.

Kwa uwekezaji wa kutoka nje, teknolojia ni mojawapo tu. Mtaji ndiyo msingi mkuu, bila pesa hakuna kitu. Soko kubwa, utulivu wa kisiasa, sera nzuri, miundombinu, na motisha ya kodi ni muhimu zaidi. Mwekezaji wa Congo anaweza kuleta mtaji wake na kununua au kuleta teknolojia. Congo ina madini mengi na idadi kubwa ya watu, soko linalokaribiana nasi. Kuwaalika katika kilimo, uvuvi na madini kunafungua milango ya biashara ya pande zote, si kudhoofisha.

Kushughulikia bandari ni jambo zuri, lakini si kisingizio cha kukataa ushirikiano mbalimbali. Ushirikiano wa kikanda unajenga nguvu pamoja. Kukosoa bila kuona fursa ni kudumaza maendeleo. Hoja yake inakosa uelewa wa biashara za kimataifa na inaonekana zaidi kama siasa kuliko uchambuzi wa kiuchumi.
Wakongo wanashindwa kutumia ardhi yao yenye rutuba, ni Tz kweli?
 
Back
Top Bottom