Kauli ya Heche kukosoa Congo kuwekeza Tanzania ina ufinyu wa uelewa

Kauli ya Heche kukosoa Congo kuwekeza Tanzania ina ufinyu wa uelewa

View attachment 3653552

Kauli ya Heche inaleta dharau isiyostahili kwa viongozi wa Taifa. Kuwaambia “hakuna watu wenye akili na maarifa” si hoja, ni matusi yanayodhalilisha taifa badala ya kujenga. Uongozi una majukumu magumu; kukosoa kwa lugha ya kejeli hudhoofisha heshima ya nchi.

Kwa uwekezaji wa kutoka nje, teknolojia ni mojawapo tu. Mtaji ndiyo msingi mkuu, bila pesa hakuna kitu. Soko kubwa, utulivu wa kisiasa, sera nzuri, miundombinu, na motisha ya kodi ni muhimu zaidi. Mwekezaji wa Congo anaweza kuleta mtaji wake na kununua au kuleta teknolojia. Congo ina madini mengi na idadi kubwa ya watu, soko linalokaribiana nasi. Kuwaalika katika kilimo, uvuvi na madini kunafungua milango ya biashara ya pande zote, si kudhoofisha.

Kushughulikia bandari ni jambo zuri, lakini si kisingizio cha kukataa ushirikiano mbalimbali. Ushirikiano wa kikanda unajenga nguvu pamoja. Kukosoa bila kuona fursa ni kudumaza maendeleo. Hoja yake inakosa uelewa wa biashara za kimataifa na inaonekana zaidi kama siasa kuliko uchambuzi wa kiuchumi.
Mkuu uwezo wa Heche ni mdogo sana. Asikusumbue!
 
Congo hawo wanategemea mpaka nyanya kutoka kigoma ndio waje kuwekeza kwenye kilimo huku kwetu yaani tutakuwa tunachekesha kwakweli mkuu
Kutegemeana kitu cha kawaida, na sisi kuna vitu tunachukua kwao
 
Kongo watakuletea technologies gani ya kilimo na wewe!? Mambo mengine mnatetea hata bila kufikiri. Kongo hawa wenye ardhi nzuri na kubwa washindwe kwao halafu wawaletee nyie maarifa! Maarifa gani hayo. Muwakimbize wazungu mje mwendelezwe na walingara!!
Soma kwa kuelewa siyo kukimbilia ku comment tu. Mtaji wa fedha na masoko ndiyo bottomline katika uwekezaji. Suala la teknolojia ni secondary
 
Soma kwa kuelewa siyo kukimbilia ku comment tu. Mtaji wa fedha na masoko ndiyo bottomline katika uwekezaji. Suala la teknolojia ni secondary
Kwao kuna mto na bahari na nchi isiyokosa mvua na madini yote ya thamani kwa nini waje kuwekeza Tanzania na sio kwao kwenye fursa na soko kubwa saba?
 
..mimi nina mashaka sana na utaratibu wa kuleta wawekezaji kufanya kilimo na ufugaji Tanzania.
Mkuu sina shaka ! uwezo wa Viongozi wetu ni duni sana. Hivi BBT imeishia wapi? Mradi ule si ulilenga kuinua kilimo pesa zile zinarudishwa vipi!
..kama kuna sekta tuna uwezo nazo nadhani ni kilimo, uvuvi, na ufugaji.
Hizi ni sekta za Kilimo tunazopaswa kuzilinda haswa kwasababu watu wetu wana uwezo ila hatuwajengei mazingira mazuri.
..nilisikia kuna WARUSI wameletwa ili walime ndizi.
Kyela, Muleba, Machame ndizi zinaoza kwasababu hatuna mkakati wa kufikia walaji na kuendeleza Wakulima
..Sasa najiuliza hivi Watanzania hatuwezi kulima ndizi? Kwanini?
Ni aibu sana! miaka 60 tunatafuta mtu wa kutufundisha kulima ndizi
..Jana tena nimemsikia Waziri Prof.Mkumbo akisema Wasaudia wanakuja kufanya ufugaji.
Profesa!
..Hivi kweli Wasaudia wanajua ufugaji na mazingira yake kuliko jamii za Kitanzania?
Yaani Wasaudia wanajua zaidi ya Watanzania! Kwani yule SAS ni Msaudia. Kinachotakiwa ni elimu kidogo tu.
..Nafasi ya mkulima na mfugaji wa Kitanzania ni nini ktk mpango mzima wa kuleta Waarabu, na Warusi, kufanya kilimo na ufugaji?
Ni aibu sana!
Halafu watu hawa wanaofikiri namna hii wana bajeti ya Trilioni 1 ya vitafunio maofisini.
Kama hatutafanya mabadiliko tutafika wakati tunaagiza Wareno waje kutuchimbia matundu ya choo.
 
Ni aina ya watu waliopo Tanzania. Mwendokasi haiendeshwi na viongozi bali Watanzania wachache walioaminiwa. Sasa wanapoiba fedha za mradi au kuuza ticketi feki tuwalaumu viongozi?? Watu wanaiba mafuta na vipuri vya Mwendokasi bado tuwalaumu viongozibwa nchi kwa kuleta wawekezaji kwenye maeneo hayo?
Hao wezi wanateuliwa na nani! Mkuu wa TRL hakuchaguliwa kwa kura, aliteuliwa. Aliyemteua ni nani
Hao Watanzania wachache walioaminiwa, nani aliwapa madaraka!
 
Sema Mzala anatumia Lugha kali sana ila ni kweli DRC hawawezi kutushauri au kufanya uwekezaji wa aina yeyote ya chakula Tanzania labda walete mtaji sisi tulime kwao wanaagiza kila kitu kutoka Nje hapo Kasumbalesa truck ni za chakula,mafuta na copper zinazotoka kwao viongozi wengi DRC wanapelekewa chakula na hizo bus za kwenda Congo..
Ni sawa na wakazi wa temeke wamtume diwani aende masaki akawashauri kuhusu mipango miji na ujenzi bora wa makazi.
 
Labda wewe ndiyo umekatika vipande vipande
Wewe unaona DRC ni nzima? Kweli akili yako haipo mahali pazuri. Hata vitu vidogo huelewi pumbavu wewe umekalia uchawa. Unajifanya hujui kuwa Eastern CONGO ambapo ndipo penye utajiri wa natural resources ipo chini ya M23 na vikundi vidogo vidogo vingi?
 
Heche kakosea. Uwekezaji ni fursa zaidi kuliko asili. Mchaga anaweza acha ardhi kubwa ya urithi kilimanjaro akaenda morogoro kulima.
Wakongo kuwa na ardhi haimaanishi kwamba hawawezi kuja kuwekeza hapa.

Kuhusu Tech, It's not about nation abilities, it's about business opportunities kwa mtu mmoja mmoja.

Kuna mtu ana biashara kubwa China, ila ukiitazama China kiujumla imetuacha mbali, unaweza jiuliza Mtanzania atapeleka nini China? Kwa Tech gani aliyo nayo? Ila wapo Watanzania wamewekeza China.
Unaweza nitajia Mtanzania mmoja tu aliyewekeza china?
 
Back
Top Bottom