Uchaguzi 2020 Kauli ya Jaji Kaijage na yanayopangwa kufanywa na NEC kwa wagombea Urais

Hivi akietaka uchaguzi uhailishwe alikuwa Nani? Na Mh Raid ndiyo alisema kipindi Korona amebamba Tanzania kuwa uchaguzi lazima ufanyike na Chadema ndiyo hamkutaka uchaguzi ufanyike

Hoja yako ni nini hapa?
 
Uongozi wa juu uliopo hautaki kabisa kampeni hasa kwenye nafasi ya juu ya uongozi. Wangependa kubaki na akina shibuda na lipumba ili kampeni zisiwe na msisimko.
Hili liko wazi na halina ubishi, kweli nchi hii tumefikia vibaya sana sana.
 
Hakuna haja yakurisha watu. Uchaguzi ni mchakato wa kisheria na kanuni. Ukikiuka sheria zinakuondoa tu, wala si Tume. Vyama inapaswa kufuata sheria na kanuni sio hisia.
Sawa , lakini je kazi ya kutafsiri sheria hizo kikatiba ni ya nani ? Tume au mahakama ?
 
Magufuli tunafaham tangu akiwa mbunge anataka apite bila kupingwa, lakini awamu hii hata akipita apite lakini dunia nzima itafaham amepitaje na inawezekana ikawa ndio mwisho wa ccm. Tundulisu msifikiri ni kondoo kama LOWASA.
Lissu ni mwepesi mno! Alafu usije unafikiri Magu anahofu na huu uchaguzi? Hana ata chembe ya hofu
 
Mbona hamjiamini? Tatizo la upinzani kupeleka makapi yaliyo toka CCM, na watu wasio na maadili wasaliti wa nchi kama kina TL, kwa nini hamjifunzi? Watu wazuri kama kina Dr Slaa mkawatupa kapuni kisa tamaa ya pesa, sasa hivi mnajambajamba tu! Kuwapa nchi wapinzani bado saaaaaana!
 
Wajumbe Wa tume ya taifa ya uchaguzi wote Ni wanaccm, wajiondoe Mara moja
Njaa Mbaya Sana,hasa inapoanzia kwenye ubongo.CCM wanadhani wana hati miliki ya Tanzania, wameweka refa wao,washika vibendera,kamisaa na bado wanatamani kupanga lineups za timu upinzani?
Huo ni mchezo katika nchi ya marehemu wasio na utashi wowote.Mnatuchukulia poa?
 
Asante kwa taarifa muhimu 'but there is no short cut in life'
 
Tanzania tuna shida ya siasa za ushabiki. Yanga ikiifunga Simba kesho maisha hayabadiliki lakini tukipata viongozi wabovu wasiojali maisha yetu,tutapata shida na hata kupoteza maisha..Tuwe makini. Tumepanda tulichovuna miaka hii 5...Ni miaka 5 mingine Mwenyenzi Mungu katupa fursa ya kuchagua tutakachovuna...Hayeni
 
Tuko tayari kuingia barabara ni kama mkoloni CCM anataka kutuchagulia mgombea Urais.
Jamani heeee hawa kina Jdg Kaijage, Jdg Mtungi & Co watatuletea baraa nchi hii.
Tuliachiwa nchi nzuri yenye upendo na maelewano sasa Ma CCM wanataka kuleta baraa!!
Uchaguzi serikali za mitaa watu walinyamaza ila sasa kwa hili sijui kama watavumilia!!
Tunaomba plse kina Maraisi wastaafu na viongozi wenye ushawishi tusaidie tusitumbukie kwenye baraa!!
 
Sawa , lakini je kazi ya kutafsiri sheria hizo kikatiba ni ya nani ? Tume au mahakama ?
Kazi ya kutafsiri na kusimamia sheria ni ya mahakama na vyombo vingine vilivyowekwa kisheria. Jukumu la kusimamia sheria ya Uchaguzi ni ya NEC. NEC itaendelea kutimiza jukumu hili mpaka pale sheria itakapo badilishwa au kutafsiriwa vinginevyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…