Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Kwani jaji yeye ni nani mpaka asisemwe vibaya mitandaoni?MwanaHalisi Digital imemnukuu Jaji Mkuu wa Tanzania akikemea vikali tabia ya baadhi ya watu wakiwemo wanasheria ya kumkosoa Jaji au mwanasheria wa upande mwingine kiasi cha kumtaja kwa jina na picha yake , na wakati mwingine kutaja hadi mahali anakokaa .
Amekwenda mbali hadi kufikia kusema , wote wanaofanya hivyo wanafahamika na kwamba siku zao zimekwisha .
View attachment 2039314
Hii ni kauli kali mno kutolewa na Jaji Mkuu , ambayo bila shaka imechagizwa na jazba , mimi nilidhani Mh Jaji Mkuu angejaribu kuangalia kufuatilia kisa cha majaji kushutumiwa mitandaoni badala ya kuwapiga mikwara watoa shutuma
Mbona majaji walipokuwa wakisemwa vizuri mitandaoni hakuja kukemea hiyo hali?
Ni lini kumtaja jaji jina mitandaoni, kuonyesha picha yake au kutaja mahali anapoishi kulikuwa ni kosa?
Kwani maisha ya majaji ni siri zisizopaswa kusemwa hadharani?
Wanasheria wa upande wa pili ni wakina nani hao, maana kikawaida mahakamani kuna wanasheria wa pande mbili zinazokinzana, sasa ukimtaja mwanasheria yoyote maana yake umetaja upande upi?