MwanaHalisi Digital imemnukuu Jaji Mkuu wa Tanzania akikemea vikali tabia ya baadhi ya watu wakiwemo wanasheria ya kumkosoa Jaji au mwanasheria wa upande mwingine kiasi cha kumtaja kwa jina na picha yake, na wakati mwingine kutaja hadi mahali anakokaa.
Amekwenda mbali hadi kufikia kusema , wote wanaofanya hivyo wanafahamika na kwamba siku zao zimekwisha.
Hii ni kauli kali mno kutolewa na Jaji Mkuu, ambayo bila shaka imechagizwa na jazba, mimi nilidhani Mh Jaji Mkuu angejaribu kuangalia kufuatilia kisa cha majaji kushutumiwa mitandaoni badala ya kuwapiga mikwara watoa shutuma
View attachment 2039314
======
Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma amesema, ndani ya mwezi mmoja, baada ya kuanza kazi Kituo Jumuishi cha Temeke, asilimia 38 ya mashauri yaliyofunguliwa na mawakili, “yalirejeshwa kwao, makosa kama kutaja kifungu cha sheria. Majaji tuangalia la kufanya ili tusiwe tunawarudishia tu.”
Huko mitandaoni nawajua mawakili, hata majina yenu ya bandia nayajua na wengine wako ndani ya mahakama, wanamshambulia jaji kwa jina na picha au wakili wa upande wa pili. Tunawafahamu. Siku zao zimekwisha- Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma
Kukosoa hukumu hakuna tatizo. Nitafurahi hukumu zangu kama zitakosolewe, nitajifunza. Lakini saizi mawakili wanawakosoa majaji, mahakimu kwa majina na picha zao, mara anaishi wapi, hii haikubaliki na mawakili wa aina hiyo hawafai kuwa mawakili- Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma
View attachment 2039391