Kauli ya Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma ni vema ikajadiliwa' ni kuhusu Mitandao ya Kijamii

Kauli ya Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma ni vema ikajadiliwa' ni kuhusu Mitandao ya Kijamii

J

Jaji Mkuu yuko SAWA, hao WANAWASHAMBULIA hivyo na yeye anayo haki ya KUWASHAMBULIA kwa mkwara mzito na hata ikibidi KWA VITENDO. Kama wana hoja waende huko kwenye mfumo wao wa Mahakama waitafute haki yao. Siyo kufanya mambo kama watu ambao hawakusoma.
Kama ni hivyo basi aache washambuliane.
 
Kulingana na maadili ya uwakili hutakiwi kwenda kumshambulia Jaji kwenye mitandao au sehemu yoyote ile. Kama ametoa uamuzi ambao hujaupenda au amekufanyia kitu chochote ambacho hakipo sawa kuna sehemu za kupeleka malalamiko yako na siyo kwenye mitandao...
Naye àtashughulikiwa, Muulize Magufuli yuko wapi
 
MwanaHalisi Digital imemnukuu Jaji Mkuu wa Tanzania akikemea vikali tabia ya baadhi ya watu wakiwemo wanasheria ya kumkosoa Jaji au mwanasheria wa upande mwingine kiasi cha kumtaja kwa jina na picha yake, na wakati mwingine kutaja hadi mahali anakokaa...
Kesi ya Mbowe imewakalia vibaya sasa wameanza maandalizi ya kujihami na hukumu.
 
Tutegemee kuokota maiti zao kwenye sandarusi huko Coco beach

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Sasa ni zamu ya Mawakili kupotezwa. Enzi za Magufuli ilikuwa kosa mshtakiwa kuweka Wakili, ilionekana Mawakili hawana uzalendo wanatetea wahalifu. Sasa Jaji ameunga mkono kauli ya Polepole kwamba kuna wahuni walibaki hawakushughulikiwa na Magufuli.
 
Wewe Ni msimamizi Mkuu wa Haki Tanzania. Kauli kuwa "muda wao umekwisha" Ni ya kukandamiza haki ambayo umeapa kuilinda. Kama ulivyoshindwa kijizuia kutoa kauli ya bitisho, mbaya Kama hiyo, Basi na mawakili wako wameshindwa kijizuia.
Jitafakari nafasi uliyoishikilia.

Pili angalia usafi wa Majaji wako.
 
Kwenye maadili ya uwakili kuna kitu kinaitwa wajibu kwa wakili mwenzako na wajibu kwa mahakama, Jaji Mkuu alilrnga haya sana sana mawakili wamemuelewa vyema.

Wakili ni afisa wa mahakama na anawajibu kama afisa wa mahakama na pia ana wajibu kwa taaluma na wakili mwenzake.

Pale ni baba alikuwa anaongea na wanawe usimshangae akiwakemea.
Huwezi kutishia watu kwamba siku zao zina hesabika. Je akifa usiku huu??
Hakuna baba mpumbavu kama huyu.
 
Back
Top Bottom