Kauli ya Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma ni vema ikajadiliwa' ni kuhusu Mitandao ya Kijamii

Kauli ya Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma ni vema ikajadiliwa' ni kuhusu Mitandao ya Kijamii

Halafu watu wanashangaa kwanini cdm hawakwenda mahakamani baada ya uchafuzi Mkuu wa 2020. Jaji mkuu ndio huyo anatishia watu kuongea mtazamo wao kwenye uhuni unaoendelea mahakamani. Bila machafuko na kuonyeshana makali, sioni mifumo yetu ikirudi kwenye njia sahihi.
Hamkuwa na ushahidi wowote zilikuwa propanganda tupu! Mlishindwa kihalali tu.

Hivi nyinyi mkishinda uchaguzi mtafuta kila mtu kwenye utumishi wa umma? Kwa sababu mmegombana na watu wote kuanzia vyombo vya dola, mahakama, bunge na wananchi wakawaida kila siku mnawaita wajinga sasa mtatawala wanyama au? Ndiyo maana tunasema nyinyi kutawala TZ labda baada ya miaka 3,000.
 
Hayo unayoyaona na kuyasikia hakika jua nyakati zimekaribia.
 
Haya maneno kama kweli yametoka kwa msimamizi wa haki BASI tunahitaji kuwa na msimamizi wa haki mwingine huyu hatufai!
Ni kweli hafai kuwa msimamizi wa haki! Anaongea kama IGP!

Eti hata majina yao ya bandia tunayafahamu. Hivi ni kazi ya jaji mkuu kufanya upelelezi?

Kama ni mkweli na mwenye kufahamu taaluma yake vyema, asingethubutu kuongea hayo maneno.

Very sad indeed. Inaonekana wengi wa hao majaji wamechomekwachomekwa tu kwa maslahi ya watawala na siyo kwa weledi wao.

What a hopeless statement!
 
MwanaHalisi Digital imemnukuu Jaji Mkuu wa Tanzania akikemea vikali tabia ya baadhi ya watu wakiwemo wanasheria ya kumkosoa Jaji au mwanasheria wa upande mwingine kiasi cha kumtaja kwa jina na picha yake, na wakati mwingine kutaja hadi mahali anakokaa.

Amekwenda mbali hadi kufikia kusema , wote wanaofanya hivyo wanafahamika na kwamba siku zao zimekwisha.

Hii ni kauli kali mno kutolewa na Jaji Mkuu, ambayo bila shaka imechagizwa na jazba, mimi nilidhani Mh Jaji Mkuu angejaribu kuangalia kufuatilia kisa cha majaji kushutumiwa mitandaoni badala ya kuwapiga mikwara watoa shutuma.

View attachment 2039314

======

JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma amekubali na kuwasajili mawakili wapya 313 katika sherehe ya 65 ya kuwakubali na kuwasajili mawakili wapya iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mawakili hao wanahusisha wanawake 170 na wanaume 143 ambao sasa wafanya idadi ya mawakili kufikia 10,749 kutoka 10,436 mwezi Juni mwaka huu katika orodha ya mawakili nchini.

Tukio hilo limefanyika leo Ijumaa, Desemba 10, 2021 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam ambapo Prof. Ibrahimu Juma amewataka Mawakili hao kuwa na nidhamu na kufikiria mbali zaidi kuliko kusubiri ajira.

Maadili na viwango, hatupaswi kuwa na mawakili wasiokuwa na maadili, kosa moja la wakili linaweza kuzungushwa mitandaoni na kutuchafua na kuchukuliwa kama Tanzania nzima hatuna maadili. Endeleeni kupambana na mawakili vishoka.

Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma amesema, ndani ya mwezi mmoja, baada ya kuanza kazi Kituo Jumuishi cha Temeke, asilimia 38 ya mashauri yaliyofunguliwa na mawakili, “yalirejeshwa kwao, makosa kama kutaja kifungu cha sheria. Majaji tuangalia la kufanya ili tusiwe tunawarudishia tu.”

Huko mitandaoni nawajua mawakili, hata majina yenu ya bandia nayajua na wengine wako ndani ya mahakama, wanamshambulia jaji kwa jina na picha au wakili wa upande wa pili. Tunawafahamu. Siku zao zimekwisha- Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma

Kukosoa hukumu hakuna tatizo. Nitafurahi hukumu zangu kama zitakosolewe, nitajifunza. Lakini saizi mawakili wanawakosoa majaji, mahakimu kwa majina na picha zao, mara anaishi wapi, hii haikubaliki na mawakili wa aina hiyo hawafai kuwa mawakili- Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma

Masikini wenzangu🏃🏃🏃🏃🏃🏃
 
Sasa hivi wanasiasa wamewazidi nguvu watumishi wa serikali kiasi cha kwamba wako tayari kujiabisha ili kuwafurahisha wanasiasa.Mfano kesi ya Mbowe ni aibu sana kwa viongozi wa JWTZ.
 
Ni kweli hafai kuwa msimamizi wa haki! Anaongea kama IGP!

Eti hata majina yao ya bandia tunayafahamu. Hivi ni kazi ya jaji mkuu kufanya upelelezi?

Kama ni mkweli na mwenye kufahamu taaluma yake vyema, asingethubutu kuongea hayo maneno.

Very sad indeed. Inaonekana wengi wa hao majaji wamechomekwachomekwa tu kwa maslahi ya watawala na siyo kwa weledi wao.

What a hopeless statement!
Vipi mkuu wewe ni mmoja wao waliotajwa na Jaji Mkuu nini? Mbona mapovu mengi sana?
 
Halafu watu wanashangaa kwanini cdm hawakwenda mahakamani baada ya uchafuzi Mkuu wa 2020. Jaji mkuu ndio huyo anatishia watu kuongea mtazamo wao kwenye uhuni unaoendelea mahakamani. Bila machafuko na kuonyeshana makali, sioni mifumo yetu ikirudi kwenye njia sahihi.
Kwani mbaya wenu si akiondolewa na mungu wenu bila kumwaga damu?
 
AIgmal.jpg
 
Hamkuwa na ushahidi wowote zilikuwa propanganda tupu! Mlishindwa kihalali tu.

Hivi nyinyi mkishinda uchaguzi mtafuta kila mtu kwenye utumishi wa umma? Kwa sababu mmegombana na watu wote kuanzia vyombo vya dola, mahakama, bunge na wananchi wakawaida kila siku mnawaita wajinga sasa mtatawala wanyama au? Ndiyo maana tunasema nyinyi kutawala TZ labda baada ya miaka 3,000.
Wewe cio mzima. Kama haya ndiyo mawazo yako unatakiwa kuombewa. Mtu anawaambia wasimamizi wa uchaguzi kuwa ole wenu muwatangaze wapinzani mtaniona halafu kwa mazingira kama hayo inaendaje mahakamani.
 
Back
Top Bottom