Kauli ya Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma ni vema ikajadiliwa' ni kuhusu Mitandao ya Kijamii

Kwani jaji yeye ni nani mpaka asisemwe vibaya mitandaoni?

Mbona majaji walipokuwa wakisemwa vizuri mitandaoni hakuja kukemea hiyo hali?

Ni lini kumtaja jaji jina mitandaoni, kuonyesha picha yake au kutaja mahali anapoishi kulikuwa ni kosa?

Kwani maisha ya majaji ni siri zisizopaswa kusemwa hadharani?

Wanasheria wa upande wa pili ni wakina nani hao, maana kikawaida mahakamani kuna wanasheria wa pande mbili zinazokinzana, sasa ukimtaja mwanasheria yoyote maana yake umetaja upande upi?
 
Huyu mzee anatakiwa afungwe kabisa

Ana ulinzi wa uhakika kwa sasa kwakuwa anasimamia uovu kwa maagizo ya watawala. Hivyo anatoa vitisho kwa wataka haki ili udhaifu wa Muhimili anaousimamia usiendelee kupuuzwa. Hapo alipo ana hukumu ya rais dhidi ya Mbowe, hivyo anaweka vitisho ili watu waogope siku hukumu ya kihuni ikitoka.
 
Wananchi na binadamu kwa ujumla hujua haki ilipo kwa asilimia kubwa bila hata kusoma sheria.
Majaji au mahakimu wakitoa haki hawashambuliwi. Mashabulizi huanza pale ambapo Imani ya haki inapokosekana.
Majaji wanatakiwa wasisitize kuwa watatoa haki na ionekane kuwa imetendeka.
 
Tutamalizana naye hata kwa waganga wa kienyeji
 
Kwa hii kauli ya jaji hivi punde mtaanza kusikia tena watu wasiojulikana
 
Kwani huyo Jaji Mkuu wapi yeye kama yeye kaonyesha kasoma na sisi raia tukaona Taaluma kwenye matendo yake??? Asiwatishe watu wazima kama yeye kama vile school's Kids.
 
Yaap nimeona nchi ya jirani hapo kwa uhuru nyeusi inaitwa nyeusi nadhani jaji anapaswa kuwanyoshea vidole hao majaji wake kwanza bahati nzuri hii kesi ya mchongo inawaaibisha mno
Una uhakika hawanyooshei kwa utaratibu rasmi? Hiyo ni mahakama mzee, hakuna kukosoana kwa style za Mtaka na Ummy hadi umma usikie. Unaweza kumkosoa mtu bila kumdhalilisha.
 
Kulingana na maadili ya uwakili hutakiwi kwenda kumshambulia Jaji kwenye mitandao au sehemu yoyote ile. Kama ametoa uamuzi ambao hujaupenda au amekufanyia kitu chochote ambacho hakipo sawa kuna sehemu za kupeleka malalamiko yako na siyo kwenye mitandao.

Kiukweli naona Jaji mkuu wetu yupo sahihi kabisa kuhusu mambo yanayofanywa na baadhi ya Mawakili. Naomba tu Jaji mkuu aendelee kuwashughulikia mawakili wote wanaoenda kinyume na maadili yao.
 
Anaposema siku zao zimekwisha ana maana watawapiga risasi kama walivyofanya kwa Tundu Lissu?

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…