Kauli ya Jaji Tiganga kwamba huenda Shahidi Ling'wenya alikuwa anapewa majibu ya maswali aliyoulizwa yawaibua Wadau

Halafu kuna kitu kimoja kimefanyika maksudi, leo ilikuwa mashtaka waje na shahidi, wakabadilikia kizimbani na kutaka utetezi waanze ili kuwashtukiza kwamba wawe hajajipanga, lakini jamaa wako smart, wamepeleka 'faya' hivyohivyo pamoja na kushtukizwa!
 
ukiwa umesimama kwenye ukweli inakua rahisi sana huna haja ya kujipanga maana licha ya kustukiza kwa kufunga ushahidi pia walikuja kwa kuchelewa sana lakini bado wakapigwa na kitu kwenye medula 🤣🤣
 
Hivi Lissu aliwahi kusemaje khs Majaji wa bongo.
2012 au 2013 wakati akitable hotuba ya makadirio ya bajeti kivuli ya Wizara ya katiba na sheria Lissu aliibua mazito juu ya teuzi za majaji na uwezo wao.

Nakumbuka hotuba hiyo mpaka iliibua tetesi za kuwepo kwa jaji mmoja kuwa hakuwa na LLB alikuwa na Diploma. Kuna jaji mwingine alitajwa kuwa toka ateuliwe hakuwahi kuandika wala kusoma hukumu mana hakuwa na uwezo wa kuandika kimombo. Ni madudu mengi yaliibuka juu ya majaji kutokana na hotuba ya Lissu. Nadhani pitia you tube unaweza ipata.

Kwa kifupi CCM imeharibu nchi hii in it's totality. Prof. Assad alikuwa sahihi aliposema 70 percent ya watu wanaoongoza taasisi hawana uwezo. Majaji ni kundi ambalo halijaachwa. Wengi wameteuliwa kwa malengo maalumu na wengi wakiwa hawana uwezo. Tiganga naona anafit kwenye kundi hili.
 
Kabla hamjajifunua, sheria zinasemaje kuhusu kauli ya jaji?

Kama sheria zinakataza, kwanini mawakili wa utetezi walikaa kimya?
walipuuza ndio maana wakili aliyekua anamwongoza akamwambia shahidi amwangalie jaji anapokua anajibu
 
Wewe na mmeo mlikenua sana Sabaya alipofungwa, sheria ni msumeno tulieni dawa iwaingie
Sijawahi kuona mwana ccm mwenye akili timam never, yaani hujitambui kichwa yako imejaa matope tu, kati ya sabaya na Mbowe nani alilalamikiwa toka mwanzo kuwa anafanya mambo ya hovyo? Yaani wewe unastahili matusi ya jumla "mpumbafu wa kutupwa wewe".
 
Kwa mtazamo wangu niliona ni kama aliridhika na namna shahidi wa kweli anavyotoa ushahidi wake, ilikuwa ni kama dhihaka wa mashahidi wa kubumba wa jamuhuri.
Mkuu; wewe umemwelea Jaji sawia! In short ameshangazwa jinsi shahidi aka mshtakiwa alivyonyoosha maelezo!

Dah; mwamba yule kanyoosha maneno hadi raha! Maandiko hayajakosea yanaposema ulimi wa kweli huthibitika milele tofauti na ule wa uongo ambao ni wa kitambo tu!
 
ukiwa umesimama kwenye ukweli inakua rahisi sana huna haja ya kujipanga maana licha ya kustukiza kwa kufunga ushahidi pia walikuja kwa kuchelewa sana lakini bado wakapigwa na kitu kwenye medula 🤣🤣
Ni kweli i see, the truth is always simple, ukweli hauna manjonjo mengi, ni umenyooka tu, wamepelekewa faya mbaya kabisa leo, yaani ni aibu!
 
Inategemea wakili alijitambulisha anamuwakilisha nani.Ikiwa alijitambulisha kumwakilisha mshitakiwa mmoja na ipo kwenye kumbukumbu wapo sawa.Lakini kama alijitambulisha mwanzo wa kesi kama anawakilisha watuhumiwa wote basi itakuwa ni makosa
 
Leo Jaji kaongea hayo maneno! Je wanasheria kwa uelewa wenu hayo maneno yanaweza kuja kutumika kukatiwa rufaa au kwa sasa hivi kumkataa Jaji?

View attachment 2023472
Huyo ni hakimu wa ngazi ya diploma,anapaswa kuendesha kesi za ugoni,wizi wa mifugo kwenye mahakama ya mwanzo..magu aliwapa ujudge mahakimu wajinga kma hawa ili wamsaidie kutoa hukumu za wapinzani
 
Sheria haina kitu inaitwa kupuuza!

Huoni aligundua kosa lake ndio maana akamlekebisha shahidi!
sawa tuchukue shahidi alikua anapewa majibu.
je yalikua yanatoka wapi na kwa nani
je kwa mazingra ya kotini inawezekana kupewa majibu bila watu wengine kuona aone jaji tu?
 
Amina Mkuu
 
Huyo Jaji Mungu anamwadhibu azidi kufanya vitu vya ajabu bila yeye kujua. Ni ktk njia ya kuiaibisha Jamhuri
 
Impartiality of a judge

It states that impartiality is essential to the proper exercise of the judicial office. Therefore a judge should make sure that his behaviour in court and in his private life maintains and enhances the public´s confidence in the impartiality of the judge and the judiciary. duties of his office.

Sasa Jana Jaji Tiganga amevunja kanuni hiyo kwa kusema kuwa shahidi wa utetezi anapewa majibu! Comment hiyo angelikaa nayo moyoni ingawa kimsingi hata moyoni mwake inabidi asiijenge dhana hiyo ispokuwa atakapokuwa anafanya analysis of evidence with strong reasons to believe so!
 
Ma judge ni watu wanaoheshimiwa sana na hawatakiwi kuwa na mazoea sana na watu wa nje mbali na familia na wafanya kazi wenzao.

Mahakamani huwa kuna canteens zina zinaandaa chakula chao. Kuanzia chai asubuhi, mchana na evening tea. Nyumbani wanakua na housekeepers chef, chauffeured car etc.

Haya yote wanafanyiwa ili watoe hukumu ya haki na wasionekane kirahisi kuweza kupokea rushwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…