Nadhani ameshangazwa na umakini wa shahidi mshitakiwa. Kama shahidi mashitakiwa kaamua kusema ukweli anaoujua yeye, ni lazima wenye hila wajiulize kwanini yuko na mtiririko huo!!
Kinachoshangaza kwa sisi maamuma wa sheria ni kama kuna ushahidi usiokuwa na mashaka kuwa mashitaka yatathibishwa - kina haja gani ya mshitaki kuweka pingamizi la kutaka mshitakiwa asijieleze??!!
Ajabu zaidi sababu wanazotumia kupinga upatikanaji wa document ya shahidi wa mashitaka (mpaka ikapelekea kuhoji kama mahakama imewasiliana na mshitaki kinyume cha taratibu) ndio wanazotumumia kuhoji barua anayotaka kuwasilishwa imemfikiaje mahabusu asiyekuwa huru!! Wanasisitiza hata kuhusu chain of custody ni shida, jambo ambalo hawakuonesha ni shida upande wao.
Leo wanasema Kibatala ni wakili wa mshitakiwa wa nne (Mbowe) hivo hakupaswa kuandika barua. Anasahau mawakili hawa hawajiwakilishi bali kampuni zao kama wao wasiviwakilisha isipokuwa serikali! Wanasahau hawajapinga Kibatala kuhoji mashahidi wao ambao walikuwa wanatoa ushahidi kuhusu walivowakata washitakiwa 1-2 na wala sio hata 3.
Mawakili wa serikali wameshindwa hata kutambua kuwa hata wao hawana mawakili dhidi ya mshitakiwa mmoja mmoja. Wamesahau washitakiwa wote wako katika kesi moja 16/2020 na wote wanashitakiwa kwa makosa yanayofanana isipokuwa mmoja kuhusu silaha na risasa!!