Kauli ya Julius Malema kuhusu kifo cha Malkia Elizabeth inasikitisha na kuhuzunisha

Alichoandika ni ukweli ila kwakuwa tunapenda unafiki basi sawa.
Ila Julius Malema anafaa kuendelea kuwa mwanaharakati siku akipewa uraisi ataiua S.A kabisa.
 
Bora hata huyo aliyeidhinisha mauaji ya kiongozi wa nje ya nchi yake kwa manufaa ya watu wake kiuchumi.
Angalia hawa wetu, Sept 7, 2017 kiongozi mmoja aliamuru kiongozi mwingine auwawe kwa risasi nyingi sababu anatetea maslahi ya watu wa nchi hiyohiyo kama Mbunge na anawaelimisha watambue haki zao.
Jaribio hilo likashindwa kwa mkono wa Mungu na akajeruhiwa vibaya mno. Bado kiongozi huyo akaagiza asigharamiwe matibabu yake na pia watu wa chama chake tawala marufuku kwenda kumuona hospitali, kukusanyika kumuombea wala kuvaa T shirt zenye ujumbe wa "Pona haraka".
Jee kuna kiongozi mnyama zaidi ya huyo? Hao ndio hata Mungu huwa anachukua maamuzi mwenyewe, kwamba hata uwe na afya njema kiasi cha kupiga push up 100 hadharani au kucheza mapanga shaa kama "wanaume Temeke" lazima apite naye kuwalinda watu wake.
 
Waafrika wenyewe kwa wenyewe mpaka sasa wanadhulumiana sana huku wakichekeana halafu wanajidai kuumizwa sana na wizi uliofanywa na wazungu huko karne ya 19
 
Bora ungekaa kimya.

Huna evidence ya blacks kuwauza wazungu utumwani
 
Ila ilikitokea akafariki kiongozi mwenye mrengo tofauti na wazungu huwa hawa mwandiki vizuri pia.
Fatilia Kuanzia Fidel Castro, Hugo Chavez na wengine hata salamu za rambi rambi huwa hawatoi.
Mkumbuke kuna watu wengine familia zao ziliguswa kabisa na tawala za kina Elizabeth.
 
Sisi tunapenda unafki, tuendelee na maisha yetu! Ya Kenya yametushinda itakua ya Malema?
 
Hawa jamaa wametutawala mpaka akili na tumekuwa kama mazuzu.
 
Ndio maana niliwahi sema humu sisi ni early version ya human being, version ya kiwango cha chini kabisa.
 
Waarabu asili yao ni watu weusi,ni baada ya kuoana na watumwa wa kizungu,wanawake wa kizungu wa mashariki,waliokuwa watumwa ndio kukapatikana waarabu weupe.Hakuna taifa duniani,halikuwahi kufanya wengine watuma,ni mataifa yote na makabila yote,yalifanyana watumwa.
 
Eliza hakuwepo wakati hayo yanafanyika.Eliza ndiye alikuwa kiongozi wakati wa kupata uhuru.Makosa ya Babu zake siyo yake.
 
Kwa waafrika wenye akili nzuri, hawahitaji kujipendekeza kwa wazungu na wengine wote waliowatesa mababu zetu na wanaendelea kunyonya Africa kwa namna moja au nyingine.
Umasikini wa fikra ni mbaya kuliko ule wa mali. Siyo kila hoja hujadiliwa.
Mazuri yzo mbona huyasemi? Wa.mewaletea shule hospitali na teknolojia kibao zinazowanufaisha lakini kutokana na upambqvu wenu bado mko kwenye lindi la umaskini wa kutupwa halafu unasinguzia wazungu!

Hao watumwq, mlikuwa mnakamatana wenyewe . Mikataba mibovu .mnayoingia inatokana na ujinga wenu halafu mnalaumu wazungu.

Hata leo hii ikipigwa kura kwa uwazi waafrika wengi watachagua kurudi kutawaliwa na wazungu.. wakoloni wameondoka zaidi ya miaka sitini lakini failure zenu bado mnawatupia wazungu.
 
Nani anapokea rambi rambi ya msiba wa malkia Elizabeth? Tujitahidi kuchangia, wasije wakashindwa kusafirisha na kuzika mwili wa mpendwa wao.wana JF.
 
Wewe ni MTUMWA, na u aibu kwa wanaojitambua. Sijui unajisikiaje kuandika hayo.
 
Najaribu kufikiria kama huko waendako wafu hukutana, sijui sasa hivi Mugabe atakuwa anampa kauli gani Elizabeth II
 
Wewe sikijana mwenzio anajuwa mengi waafrica tumetendewa mambo yakinyama sana na wazungu hata Mungu analijuwa hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…