Kauli ya Julius Malema kuhusu kifo cha Malkia Elizabeth inasikitisha na kuhuzunisha

Sure.. Utumwa ni kuhoteana, kila race iliwai hotea race nyingine katika wakati fulani... shida ni kwamba race zingine zote zimeshamove on ila sisi ndiyo bado tunalia kila siku tunasahau kuwa na sisi tuliwai wahotea wakati fulan.
Leta hicho kitabu uliposoma haya unayosema
 
Ungejua madhira ambayo wazungu wametupa na Sasa Hawa vibaraka wao anyway ni neema ya Mungu kwamba Afrika bado inahimili vishindo
 
Namsifu Malema kwa kusema ukweli,na wengi wenu ukweli hua hampendi kuusikia
 
Nimesema Julius Malema amezaliwa 1981 ila anavyojinadi km kazaliwa 1502

Anatia hasira **** yule
Kumbuka pia SA imepata Uhuru 1994 . Pia malema kuzaliwa 1981 hakumfanyia yeye kutokujua mateso ya Babu na Bibi zake walio fanyiwa na Dictators Royal family ya UK
 
Umeelewa alichosema malema?
 
Malema yupo sahihi kwa waafrika wenye mtizamo wa kimapinduzi na Waafrika wanafiki wenye kupenda umagharibi au undumilakuwili nao wapo sahihi pia kuomboleza kifo cha Malkia Elizabeth!
 
Mawazo ya sampuli yake ni sawa mtu kuwa nayo, lakini kuyaleta wakati huu ni kutafuta umaarufu usiokuwa na maana, kwangu siku zote kuipiga teke maiti ni upungufu wa akili kwa yule anayeipiga.
Malema anatafuta umaarufu au tayari ni Maarufu 🤣🤣
 
Hakuna mwanasiasa msafi kama pamba, ila angalau watu 'vocal' wa aina hiyo ni muhimu sana. Hapa amezungumzia madhila waliyoyapata chini ya uangalizi wa Malkia na si habari ya Wazulu. Halafu mkuu unataka Kiongozi aishi 'Manzese' ya South Afrika! ili aonekane anawajali Watu. Lakini kuhusu wageni kushambuliwa Malema alitoa statement ya kulaani hilo tena waziwazi

Malema is well-known for his controversial politics; however, the EFF commander preached a simple message of love and unity when it came to this difficult topic. The EFF politician affectionately known as ‘Juju’ drove one particular point home when it came to xenophobia in SA: “Africa is for all of us…”
 
Ni hao hao wazungu unao wasifia ndio walio walea viongozi wetu unao waponda,tunayo ita misaada ni zao la raslimali zetu walizo ingia mikataba na viongozi walio wasimika. Hao hao wazungu ndio wanatufitinisha na neno lao "demokrasia"... Ni wanafiki kwa maslahi yao.
Kama tunajiamini na kuchagua mema kutoka kwa wazungu, basi,tujichagulie viongozi wetu kwa mfumo wa asili yetu,inawezekana kabisa matokeo yasipite kwenye wizi.
 
Kwangu ni mnafiki na hana tofauti kabisa na politicians wengi wa hapa Africa, anajifanya yupo very vocal kumbe ni kwa ajili ya maslahi yake binafsi, anazungumzia demokrasi wakati ndani ya chama chake anakiongoza kwa iron rule, kuna baadhi ya municipalities alishinda why ameogopa kuziongoza?kulalama on the side ni tofauti kabisa na kuwa in the mix, EFF hawana respect na angalia walivyoligeuza bunge la SA kuwa kama kijiwe cha kahawa, EFF hawana uwezo wa ku uphold rule of laws, hata mimi kama unaingia kwangu kwa kuruka dirishani wakati mlango upo definitely Nita deal na wewe maana ur undermine me,mfano wa malema kuishi na watu anaowapigania nimeutoa ili ujue unafiki wake, bankrollers wake ni crocodiles 🐊, mchana anajifanya anawachana giza likings anaingia kwa kunyenyekea kwenye security estates zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…