Lukonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 1,469
- 2,086
Nimejaribu kuifikiri na kuichambua kauli iliyotolewa na WHO Director General sijafika mwisho ila ni kauli inayofikirisha sana.
"COVID-19 not a priority: COVID-19 does not register as a priority for the millions of people affected by the conflict because of the myriad other threats they face, according to Tedros.
“It's not even their concern,” he said. “The chance of dying from all the issues… is really high. Compared to that, COVID is nothing."
Kauli hii ameitoa kwenye maelezo yake akiingolea jimbo lenye mgogoro la Tigrey huko Ethiopia.
MY TAKE
Kwanini watanzania tujilazimishe kuifanya Covid 19 a priority wakati tuna magonjwa yanayotumaliza sana?
Tatizo ni pale tulipoamua kuficha taarifa za vifo halisi vya Covid, lakini hata kwa machache yanayojulikana:
1: Ni janga lipi limetuchukulia viongozi wa juu wa nchi ndani ya kipindi kifupi?
2: Ni janga lipi limeondoka na wanasayansi/wasomi andamizi ambao nchi iliwekeza kuwasomesha kwa kipindi kirefu na wakaondoka ghafla?
3: Ni janga lipi limeondoka na wananchi wa kawaida kwa wingi ndani ya kipindi kifupi?
4: Ni janga lipi hapa kwetu limetatiza uchumi wa nchi kama Covid ndani ya muda mfupi?