Kauli ya kuitwa 'wanyonge' ndio silaha hatari wanayoitumia viongozi ili wananchi wasitoke nje ya boksi

Kauli ya kuitwa 'wanyonge' ndio silaha hatari wanayoitumia viongozi ili wananchi wasitoke nje ya boksi

Masikini wa akili ambao wengi ni wana CCM.
Wakazi wa maeneo anayopenda kutembelea
 
Myonge ni kabwela,hana pa kukimbilia au hana pa kusemea akasikilizwa na ndio walio wengi.
 
Aisee! Kumbe kundi la wanyonge ndiyo hilo!!
Wana nguvu kazi, Vijana bado lakini wanalelewa kama walionyongwa na maisha. Wanachoweza kufanya ni kutandika bidhaa kwenye barabara za miji, vibaraza,miti bila kubughudhiwa. Bidhaa zenyewe pipi na matochi ya mchina! Bila aibu nao wanashangilia kuitqa wanyonge ilhali ni ni Vijana na nguvu na akili zao!
 
Kwahiyo alikuwa anaomba Kura kwa ajili ya wanyonge na siyo watanzania!! Kazi ipo lakini tutafika
 
Mada hii imeanzishwa na mtu mwenye uwelewa wa hali ya juu. Na mpaka sasa imechangiwa na watu wenye uwelewa wa hali ya juu.
Muanzilishi na wachangiaji wa uzi huu si wanyonge. Wanyonge ni watu wananipigia kura ccm.
 
Wanyonge wenyewe..
IMG-20171029-WA0011.jpg
 
Kwa hiyo ukitoa wanyonge waliobaki hawana viongozi wa kuwatetea? au hawakupiga kura katika uchaguzi. ni lazima uwe kiongozi wa wote na utengeneze mazingira ili kila mtu apige hatua mbele yule mnyonge apate na aliyekuwa nacho apate zaidi ndio kukuwa kwa uchumi. lakini sio hawa uwapandishe na wengine uwashushe. uchumi imara haujengwi na kauli za kisiasa ili upate kuongoza ila ni policy nzuri kuwawezesha watu wote nafasi sawa kusonga mbele kwa kadri ya uwezo wa mtu. mfanya biashara mtaani atafanya zaidi biashara ikiwa kazungukwa na majirani ambao hali zao za kiuchumi zinaimarika kila siku ila kama watu ni maskini hausaidii kukua kwa biashara. sote tukiweza kusonga mbele kila mtu atafaidika sasa tuache kaulli hizi mimi kiongozi wa wanyonge je hawa wasio kuwa wanyonge nani kiongozi wao?
 
Ni vizuri kama katiba ingetamka haya madaraja ya Watanzania kama vile wanyonge n.k ili kila mmoja ajue kundi lake...ni wazo langu tu hilo
 
Hapo kwa usemi wa wanyonge basi watz wengi huku kijijini wapo hoi kwa kuupenda msemo huuu Ila nami nashangazwa Sana maana duuuh nishida xo nazimia kwenye gia kwani sinamkojo wa kupimwa kwa Sasa maana nilikuwa toilet
 
Back
Top Bottom