Kauli ya kuitwa 'wanyonge' ndio silaha hatari wanayoitumia viongozi ili wananchi wasitoke nje ya boksi

Mwendazake aliwatumia Machinga kwa faida ya kujijenga kisiasa. Kwanza aliwaita wanyonge. Mnyonge naliona kama TUSI kwa Watanzania. Tafsiri yake hii hapa:

1.mtu dhaifu; mtu asiyekuwa na nguvu Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni (ms) Synonyms: mnyela
2. mtu mwenye tabia ya upole na ya kunyenyekea
3. mtu wa hali ya chini Mnyonge kupata haki ni mwenye nguvu kupenda (methali)

Binafsi silipendi hili neno, tupaze sauti sauti wana siasa wasituite sisi wanyonge, watumie neno wananchi au Watanzania, waache kutusanifu.
 
Tundu Lissu mwenyewe ameshakuwa mnyonge kwa mabeberu, na amekua akisema bila wao sisi hatuwezi kitu sasa wewe ukatae nuna ujanja gani?

Mzuie kwanza Lisu kuwaabudu wazungu na kuwa mnyonge wao kisha ndo uludi kwetu hapa.
acha kuhamisha upepo wa mada. mbinu ya kizamani sana.
wanyonge wanao semwa hapa ni wanyonge haswa waliopo tz.
 
Kukubali kuitwa mnyonge ni kuidhalilisha nafsi yako. Mungu aliumba binadamu mkamilifu mwenye nguvu za mwili na ubongo.

Yeyote akizitumia akili zake na nguvu zake vizuri ana uwezo wa kupiga hatua kiuchumi na kijamii.

Usikubali kuitwa Mnyonge, utapata LAANA kama aliyokndoka naye Mwendazake
 
Wasalaam

Kumekua na baadhi ya watu ambao wanapenda Sana kuenzi legacy ya awamu ya tano kwa kutumia neno lililoiburiwa awamu hiyo maarufu kama "WATANZANIA WANYONGE" bila aibu ingawa tuko awamu ya sita! Sijui Wana agenda gani??

Kuna mambo mengi ya kujiuliza juu ya uharisia wa kauli ya kuwatetea wanyonge huku wengi wao wakiona Kuna kasoro mahali wanapiga kelele eti Bora angekuwepo mtetezi wa wanyonge!!!

Mathalani, unasemaje unatetea wanyonge nakati wanyonge hao hao wamerundikana mitaani wakiwa ni majobless na hauna strategic plan ya kuwaokoa??
Unasemaje unatetea wanyonge nakati unatamani hata kile ambacho wako nacho mfukoni unakitaka kiingie kwenye system yako?
Sasa unatetea wanyonge gani?????

Haya mambo ya kauli ya unyonge wa watanzania yanapumbaza Sana, yanafunga uwezo wa kufikir na yanaleta utegemezi kwa Raisi, kwa hiyo kauli hii ya unyonge imepaswa kuachwa na kutokomezwa mara moja ili Kila mtu ajue anapambana na hali yake mwenyewe.
 
Wanaotumia neno hilo Wana agenda ficho nyuma unyonge unaozungumziwa.
 
Naunga mkono hoja, kuitwa wanyonge ni udhalilishaji kama mwingine.

CCM inatumia kauli mbiu hii ili kuwatawala
 
unataka tusiwe na huo msamiati kwenye lughayetu?
 
Wewe pambalu hebu tuondolee upuuzi wako wa Bavicha hapa!

Nchi hii ina wananchi masikini wengi ambao wako kwenye kipato chini ya kiwango!

"Watanzania wanyonge" ni jina halisi ambalo lilibeba dhana na malengo ya kuwainua na kushughulikia kero za wananchi wenye hali duni.

Hii ilienda sambamba na kuwajengea uwezo wa kiuchumi kama vile ujenzi wa hospitali, madawa, elimu bure, miundombinu, mikopo nk...
 
Kama unalipenda hilo jina litumie wewe na sii kwa watannzania,Watanzania no matajiri na utajiri kwa Kila mtu inawezekana
 
Bora mrundi katuachia nchi yetu!
Wakuu

Hivi inaingia akilini raia mtanzania ambaye ni mpiga kura, ambaye ni mlipakodi kwa nchi yake na ambaye ni mwajiri mkuu wa viongozi wetu kwa kuwapa dhamana ili watuongoze wanasimama mchana kweupe na kutuita wanyonge haya ni matusi ya reja reja.

Wakati huo huo mtu anasema sisi ni matajiri na wakati huohuo sisi hao hao ni wanyonge huku anasahau neema zote na raha zote hadi V8 na kiyoyozi anavotumia ni kodi yetu.

Wananchi tupewe heshima yetu ni afadhali watuite “ Hawa Watanzania “ AU “ Hawa Walipa Kodi “ mambo ya unyonge nayo hatutaki kuyasikia tena sio heshima na nikutukosea adabu Mimi binafsi sio Mnyonge ni mtanzania shujaa tena mlipakodi kwa nchi yangu Tanzania na napenda niitwe kama mtanzania na sio mnyonge maana mnyonge hua hana haki na ni mtu dhaifu.
 
Wewe pambalu hebu tuondolee upuuzi wako wa Bavicha hapa!

Nchi hii ina wananchi masikini wengi ambao wako kwenye kipato chini ya kiwango!

"Watanzania wanyonge" ni jina halisi ambalo lilibeba dhana na malengo ya kuwainua na kushughulikia kero za wananchi wenye hali duni.

Hii ilienda sambamba na kuwajengea uwezo wa kiuchumi kama vile ujenzi wa hospitali, madawa, elimu bure, miundombinu, mikopo nk...
Nyinyi si ndo mlikuwa mnapiga kelele za shangwe eti mmefikia level ya uchumi wa Kati??!
Sasa huo wingi wa wananchi maskini unatokea wapi??

Tatizo umekalili ndgu, hutaki kutumia utashi , we kazi yako kumeza unayomezeshwa, na nyie ndo wale wapambe wa legacy za mwenda!
BADILIKA
 
Huu wimbo siku hizi sisikii sana wana CCM wakiumba. Watanzania wanyonge wameisha!!??
 
Back
Top Bottom