Imeandikwa kuwa wanyonge hawatouona ufalme wa Mungu, lakini pia kiumbe dhaifu na mnyonge amejikatia moto wa milele.
Leo mlemavu wa miguu au macho au mikono, nenda kamwite "we kilema", halafu uone kama atafurahia jina hilo, japo kweli ni kilema.
Albino kumwita zeruzeru nayo japo si kosa na kweli kwa kiswahili tunamwita hivyo, ila ni kama dhihaka, hawapendi kuitwa hivyo.
Sasa mmeamua sisi tusio na ajira, maskini, wamachinga, bodaboda nk. Kutuita wanyonge.
Najua dhana na lengo lenu, kweli tujione wanyonge tusioweza kitu au jambo na mwisho mtutumie tu.
Kuanzia leo iwe mwisho kutuita wanyonge, kwani mbona nyie mlikuwa "wenye nguvu", "wezi" kunachuki?
Basi tuheshimiane, iwe mwisho