Kauli ya kuitwa 'wanyonge' ndio silaha hatari wanayoitumia viongozi ili wananchi wasitoke nje ya boksi

Uchaguzi umeisha nitakusemea kwa litundulissu likushitaki kwa kughushi ilani yake. Ila lenyewe lilisema "huyu magufuli mtakatifu wetu anayejiita mtetezi wa wanyonge". Huu usemi ni wa kawaida, hulka ya Watanzania, sioni kama una shida yoyote. Ukimwita sugu mheshimiwa au pter msigwa mchungaji haina maana kwamba ni mheshimiwa au ni mchungaji; ndivyo tu tulivyo Watanzania. Kamanda, na wewe tafuta kibwagizo chako huru usipoteze muda wetu.
Nimetoa maoni yangu mkuu. Au siko huru kutoa maoni yangu?
 
Ukweli ni kwamba watanzania wengi ni wanyonge.Kwa mujibu wa kamusi hiyo.
Kuitwa mnyonge ni tusi kubwa Sana. Kwa mujibu wa kamusi.

Mnyonge ni mtu hoe hae asiye na mbele. A futureless person. Hawa ndio mtaji wa wanasiasa na ndio uamua hatma ya maisha ya watu wote katika nchi.
 
Wakuu

Hivi inaingia akilini raia mtanzania ambaye ni mpiga kura, ambaye ni mlipakodi kwa nchi yake na ambaye ni mwajiri mkuu wa viongozi wetu kwa kuwapa dhamana ili watuongoze wanasimama mchana kweupe na kutuita wanyonge haya ni matusi ya reja reja.

Wakati huo huo mtu anasema sisi ni matajiri na wakati huohuo sisi hao hao ni wanyonge huku anasahau neema zote na raha zote hadi V8 na kiyoyozi anavotumia ni kodi yetu.

Wananchi tupewe heshima yetu ni afadhali watuite “ Hawa Watanzania “ AU “ Hawa Walipa Kodi “ mambo ya unyonge nayo hatutaki kuyasikia tena sio heshima na nikutukosea adabu Mimi binafsi sio Mnyonge ni mtanzania shujaa tena mlipakodi kwa nchi yangu Tanzania na napenda niitwe kama mtanzania na sio mnyonge maana mnyonge hua hana haki na ni mtu dhaifu.
 
Kwanza nani anawanyonga?
Pili kwanini wasianze na hao wanaowanyonga wananchi?
Wanapopigana watu wawili, wakumshika ni yule anayepiga siyo anayepigwa
 
Kwa sababu wanatuibia na kutukandamiza na bado uchaguzi ukija wanajitangaza washindi! Hapo lazima watuone wanyonge...
 
Hakuna wanyonge bali kuna wajasiriamali JASIRI.
Wapambanaji.
 
Wakuu
Hivi inaingia akilini raia mtanzania ambaye ni mpiga kura, ambaye ni mlipakodi kwa nchi yake na ambaye ni mwajiri mkuu wa viongozi wetu kwa kuwapa dhamana ili watuongoze wanasimama mchana kweupe na kutuita wanyonge haya ni matusi ya reja reja.
Wakati huo huo mtu anasema sisi ni matajiri na wakati huohuo sisi hao hao ni wanyonge huku anasahau neema zote na raha zote hadi V8 na kiyoyozi anavotumia ni kodi yetu.
Wananchi tupewe heshima yetu ni afadhali watuite “ Hawa Watanzania “ AU “ Hawa Walipa Kodi “ mambo ya unyonge nayo hatutaki kuyasikia tena sio heshima na nikutukosea adabu Mimi binafsi sio Mnyonge ni mtanzania shujaa tena mlipakodi kwa nchi yangu Tanzania na napenda niitwe kama mtanzania na sio mnyonge maana mnyonge hua hana haki na ni mtu dhaifu.
Watanzania ni wanyonge ndio sababu wenye mamlaka wanaudhubutu wa kuwapora haki zao na wasiweze kufanya lolote !!
 
Ni wanyonge kweli ikiwa kila ripoti tunapigwa tuu na ripoti zikitoka mpaka CAG anafukuzwa kazi ili kurahisisha upigaji wao kwa nini wewe usiitwe mnyonge...
Achana na io na ile ya uchaguz ndio kes kabisa ile no wanyonge kwel kwel mm sijawah kwenda kupiga kura
 
Bandika bango hapo kwako kuwa unayo pesa na maisha mazuri kiasi vha kwamba hauhitaji utetezi wa kiongozi wako
 
Asee ukiitwa mnyonge pigana, mtu anatumbua 4bl anakaa nazo ndani tu. Hazina kazi tuseme. Hivi watu kama hawa rais wao ni yule yule wa wanyonge au rais wao mwingine?

Kumbe wanyonge tulikua mtaji kwa wababe, wenye nchi, wenye nguvu, wenye akili, wanasiasa 🤔🤔

4bl zinamilikiwa na mnyonge m1, je anastahili kuhitwa mnyonge kweli? Au wanyonge ni watu wa aina gani?
 
Asee ukiitwa mnyonge pigana, mtu anatumbua 4bl anakaa nazo ndani tu. Hazina kazi tuseme. Hivi watu kama hawa rais wao ni yule yule wa wanyonge au rais wao mwingine?

Kumbe wanyonge tulikua mtaji kwa wababe,wenye nchi, wenye nguvu,wenye akili, wanasiasa 🤔🤔

4bl zinamilikiwa na mnyonge m1,je anastahili kuhitwa mnyonge kweli? Au wanyonge ni watu wa aina gani?
Ona mcha Mungu na mnyenyekevu, mpenda wanyonge namna alivyokuwa anaongea na wanyonge kwa upendo.
 
Asee ukiitwa mnyonge pigana, mtu anatumbua 4bl anakaa nazo ndani tu. Hazina kazi tuseme. Hivi watu kama hawa rais wao ni yule yule wa wanyonge au rais wao mwingine?

Kumbe wanyonge tulikua mtaji kwa wababe,wenye nchi, wenye nguvu,wenye akili, wanasiasa 🤔🤔

4bl zinamilikiwa na mnyonge m1,je anastahili kuhitwa mnyonge kweli? Au wanyonge ni watu wa aina gani?
Wanyonge ni mtaji wa kisiasa
 
Back
Top Bottom