Hili jina limeanza awamu hii ya tano, huko nyuma tuliitana ndugu..."ndugu wananchi". Lkn awamu ya tano tunaitwa "wanyonge".
Wanyonge ni watu ambao hawana cha kuwafanya wenye nguvu (watawala). Katiba inasema mamlaka yote yatatoka kwa wananchi. Iweje huyu tuliyemweka atuite wanyonge?
Maneno huumba ati! Ukiitwa zoba na ukakubali unakuwa zoba kweli.
Sasa ktk awamu hii ya tano tumeona hili jina linatufanya wananchi tunaonesha unyonge halisi. Mifano:-
- wafanyakazi hawapandishiwi mishahara yao kwa kuwa hawana la kuwafanya watawala (ni wanyonge).
..wakulima wanalima wanafanya kila kitu kwa hela na nguvu zao lkn baadaye wanawekewa masharti, eti wasiuze nje ya nchi (ni wanyonge).
...Tumebomolewa majumba wakati vibali vya kujenga vilitolewa na wao (unyonge)..
..Tunaondolewa kazini eti tuna vyeti fake wakati ajira walitupatia wao (unyonge).
..katiba inaruhusu vyama vingi, watu wanachagua vyama vyao na kushiriki uchaguzi kupitia huko. Wanajiandikisha na kupiga kampeni, kisha wanapiga kura halafu kwasabb ya unyonge tu mazing-zong yanajitokeza.
Hili jina "wanyonge" lipigwe marufuku kutumika.