"
Kwanza hiyo tafsiri yakohapo juu napingana nayo,viongozi wanaoitumia kauli hii wako sahihi na wanaitumia lugha hii kulingana na mahitaji ya wakati tulio nao.
Kiukweli nchi ya Tanzania kipindi kilichopita ilitengeneza matabaka ya walionacho na wasiokuanacho, dhulma ilitamalaki,uonevu,kukosekana huduma za haki za kisheria,huduma za afya zilitolewa kibaguzi,
wananchi kupokwa haki ardhi kwa kua tu hawana nguvu za kiuchumi,
Hali hii ikatengeneneza "wanyonge" kwa tafsiri sahihi ya kiswahili ni watu waliokosa msaada,
Kilichofanyika katika awamu ya tano ya rais Magufuli ni kulipa kipaumbele kundi hili la wanyonge kwa lengo la kuliinua .
Kuimalisha huduma za kijamii,kuhakikisha mfumo wa utoaji haki hauna upendeleo, kuwasikiliza kero zao na kuzitatua,kuwapa elimu bure,kwa sababu elimu iligeuka biashara badala ya huduma kwa jamii,na mengine mengi yenye lengo chanya kuwainua kiuchumi.
Hivyo kauli hii hua ni msistizo wa viongozi ya kua ipo na kundi hili kubwa pamoja nalo katika kuliinua kwa kuliwezeshea miundo mbinu bora,na wala si dhihaka,au tusi,