Nimekuwa nashuhudia kuwa utawala wa awamu hii wakijisifia kwamba Rais wetu ni Rais wa wanyonge.
Huwa najiuliza tafsiri ya neno mnyonge katika kamusi ya Kiswahili Sanifu. Mimi siyo miongoni kwa wanaostahili hiyo sifa na nakataa rasmi kuitwa mnyonge.
Kwa kuwa ni haki yangu, mtu yeyote asiniite mnyonge.
Hofu yangu ni moja tu. Nitakuwa sina Rais? Natamani kuomba Mh. Magufuli aache kujiita Rais wa Wanyonge maana ni utwezaji wa utu wetu Watanzania.
Unyonge ndani ya nchi huru kwa umri wa nusu karne, ikiwa na raslimali lukuki ni jambo lisilokubalika.
Mimi siyo miongoni mwenu, naomba mturuhusu tumtafute kiongozi wa Tanzania na siyo wa wanyonge, huu ni udhalilishaji.
Nawaomba ndugu zangu Watanzania, tukatae unyonge, siyo sifa njema.