Kwa hiyo ukitoa wanyonge waliobaki hawana viongozi wa kuwatetea? au hawakupiga kura katika uchaguzi. ni lazima uwe kiongozi wa wote na utengeneze mazingira ili kila mtu apige hatua mbele yule mnyonge apate na aliyekuwa nacho apate zaidi ndio kukuwa kwa uchumi. lakini sio hawa uwapandishe na wengine uwashushe. uchumi imara haujengwi na kauli za kisiasa ili upate kuongoza ila ni policy nzuri kuwawezesha watu wote nafasi sawa kusonga mbele kwa kadri ya uwezo wa mtu. mfanya biashara mtaani atafanya zaidi biashara ikiwa kazungukwa na majirani ambao hali zao za kiuchumi zinaimarika kila siku ila kama watu ni maskini hausaidii kukua kwa biashara. sote tukiweza kusonga mbele kila mtu atafaidika sasa tuache kaulli hizi mimi kiongozi wa wanyonge je hawa wasio kuwa wanyonge nani kiongozi wao?