Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Mkuu moja ya silaha wanayoitumia kudhoofisha upinzani miaka yote ni pamoja na kupandikiza mamluki kwenye nyadhifa za juu za uongozi ili kuvuruga mambo hasa pale upinzani unapokuwa tishio..
Mbinu nyingine ya CCM ni kuhakikisha wanaitumia dola kutisha viongozi wa upinzani ikiwa ni pamoja na kukata mianya yao ya kuingiza fedha, kupandikiza kashfa ili kuwachafua kwenye jamii, kubambikiza kesi ili kuwanyima uhuru nk..
Kuwa kiongozi kwenye upinzani unahitaji uwe na uwezo kifedha kulisha familia na ndugu zako, kusomesha watoto wako, unahitajika pia kuwa na Afya njema kukabiliana na mikikimikiki, uwe unaakili za kimjini mjini, uwe mafia kiaina, usiwe mnafiki, usiwe mtu wa kuyumbayumba, uwe na elimu ya wastani, uwe jasiri.. SIASA ZA AFRICA ZINAHITAJI WATU WA HIVYO NA KWA MBOWE SINA SHAKA...
Sina tatizo na utetezi wako maana umeshiba utetezi wenye mashiko, ila mimi sijawahi kuamini kwenye uwezo wa mtu kukaa madarakani zaidi ya miaka 10 madarakani. Hivi akifa leo ndio chama basi? Siamini katika uimara wa mtu, bali naamini katika uimara wa taasisi.