Themagufulianz
JF-Expert Member
- Apr 15, 2017
- 4,548
- 1,988
kuhusisha matatizo ya chadema na ccm ni udhaifu mkubwa..
Tunategemea perfection kwa chadema sio kushughulikiwa wala kuonja sumu.
Tunategemea perfection kwa chadema sio kushughulikiwa wala kuonja sumu.
Sijawahi miliki kadi yoyote ya chama cha siasa, lakini cdm nimekuwa nikiipa support ya hali na mali, na watu Kibao wameikubali na kuipa cdm kura kwa ushawishi wangu. Lakini sihitaji kadi yao wala ya chama chochote cha siasa hasa ccm, narudia tena hasa kadi ya chama cha maibilisi ccm.
Ni hivi, Sumaye hawezi siasa za ushindani kwani alitoka ccm kwenye siasa za mbeleko ya vyombo vya dola na tume ya uchaguzi, hivyo anapokutana na ushindani halisi wa kisiasa hawezi kutoboa. Ingekuwa kwenye uchaguzi kulitokea vurugu ili kuhujumu box la kura hapo utetezi wake ungekuwa na mashiko. Au tungeona box la kura likitolewa nje ya chumba cha kura kisha kwenda kupunguza kura zake, hapo angekuwa na Utetezi wenye mashiko. Hilo neno kushughulikiwa analitumia kuficha aibu ya kushindwa.
Kama alitegemea atashinda kwa upendeleo basi ameumia, yeye arudi ccm ili arudishiwe mali zake za wizi alizopata akiwa madarakani. Mpigie simu kisha muulize alifungua matawi mangapi ya cdm toka alipojiunga, akikupa hiyo idadi uje umtetee. Anataka kuchuma kwenye shamba walilolima wanaume wenzake, aende ACT , ama arudi ccm, au aanzishe chama chake awe mwenyekiti kama Zito fullstop.