Rais Samia aliisha sema yeye hana kabila bali ni Mzanzibar. Nape unapojibu hoja nenda na context ya mazingira ya sasa kipindi cha siasa za akina Malechela miaka ya 80 imebadilika mnoHiyo kauli inashida gani kwani siyo mzanzibar kweli? mbona Magu aliitwa msukuma na hakuna mtu alilalamika?
Hiyo kauli inashida gani kwani siyo mzanzibar kweli? mbona Magu aliitwa msukuma na hakuna mtu alilalamika?
wazanzibar wametuchezea na kudeka kwa miaka mingi sana. ifike mahali tumwage tu mboga na ugali.
hana kabila, ila yeye ni "mzanzibari", mbona anataja kabila sasa? sisi wabara ukijiita wewe mzanzibar tunaokuona unataja kabila lako la uzanzibari, kama yeye asingekuwa mkabila, si angesema yeye ni "Mtanzania". hivi mnamwelewa?Rais Samia aliisha sema yeye hana kabila bali ni Mzanzibar. Nape unapojibu hoja nenda na context ya mazingira ya sasa kipindi cha siasa za akina Malechela miaka ya 80 imebadilika mno
Baba yenu wa taifa aliwahi kumteu mzanzibari kuwa waziri mkuu wakati mamlaka ya waziri mkuu mwisho chumbe pole sanaUongozi wa Samia ndio tumeona wazanzibari kuteuliwa kuwa maDC upande wa bara. Je mTanganyika anaweza kuwa DC Zanzibar?
Mbona huyo Mwinyi amezikwa Zanzibar, na kijana wake ni Rais huko pia.marais wa zanzibar ni wangapi? Ali Hassan Mwinyi ni wa kwenu, na yeye mwenyewe alifafanua kwenye kitabu chake. Alikwenda Zanzibar kwa ajili ya kupata elimu akabakia kule, sasa tena hao marais wako wapi? Miaka 57 mumetutawala, bado tu munalalamika na hiyo mitatu ya Samia?
Kwanza niombe moderators muiache hii thread ijitegemee, inaenda mbali zaidi ya kauli ya Lissu.
Kama una akili timamu na za kutosha, utakuwa umegundua kwamba suala la kusema kero za muungano zinatatuliwa limekuwa ni suala la kuzidi kuipa Zanzibar mamlaka yake kama nchi kamili na kuiondoa kwenye mambo yanayohusu muungano. Hii inatia ndani kuwapa zaidi nafasi waZanzibar kufanya kazi upande wa bara, si katika taasisi za muungano tu, bali hata maeneo ambayo sio ya muungano. Na tunajua ukweli suala hili limekua kubwa sana kipindi hiki cha Raisi Samia.
Sasa nyie watu mnaojiita viongozi wetu mkidhani kwamba watu wa bara hawaoni hili, basi mnajidanganya. In fact viongozi wa bara mnaoshupalia kumlaumu Lissu kwa kauli yake mnaonekana kama wasaliti wa Tanganyika, traitors. Kila mtu wa bara kwa sasa anaona ukweli kwamba katika suala la Muungano, Zanzibar ina mamlaka kamili kama nchi japo kuna kidanganyio cha muungano, wakati rasirimali za bara zinazidi kuibeba Zanzibar kila siku kwa kisingizio cha muungano. Zanzibar walipohisi kuna mafuta visiwani waliamua mafuta yaondolewe kwenye muungano. Mnafikiri watu wa bara hawaoni haya?
Kwa mfano, Zanzibar wanaruhusiwa kumiliki ardhi bara, lakini watu wa bara hawawezi kumiliki ardhi Zanzibar kwa kisingizio Zanzibar ni kisiwa kidogo. Sasa kama ni kisiwa kidogo, si ndio maana Wa Zanzibar wanaruhusiwa kuhamia bara? Ingekuwa sawa kusema ni kisiwa kidogo kama Wazanzibar wasingeruhusiwa kumiliki ardhi upande wa bara. Sasa unaruhusu waje bara kupunguza pressure ya population kule, lakini unasema watu wa bara msinunue ardhi Zanzibar. Unawahadaa nani kwa kisingizio hiki, watu wa bara? Kwa sababu tunajua sababu ya kuwanyima watu wa bara kununua ardhi Zanzibar sio upungufu wa ardhi. Kama ardhi ya kununua haipo basi haitawezekana kununua, na watu watajipatia ardhi bara. Sio rahisi kununua ardhi Moshi kwa sababu hakuna ardhi ya kununua, sasa leo utasema Wasukuma wasinunue ardhi Moshi kwa sababu Moshi kuna upungufu wa ardhi kwa ajili ya Wachaga, una akili sawasawa wewe?
Zanzibar sasa imekuwa ikifanya kitu kinaitwa "cherry picking" kuamua nini kiwe katika muungano, na inaonyesha wazi kwamba katika suala la wao kufanya hivyo, watu wa bara hawatakiwi kupinga lolote. Na tunajua kwamba kwa sasa Zanzibar wanatumia nafasi ya uwepo wa Rais Samia kwenye kiti cha Uraisi kama nafasi pekee ya kuvutia mambo mengi upande wao. Hilo sio siri.
Zanzibar wamejisahau sana katika kuvutia upande wao hadi imefikia watu wachache wameanza kudokeza kwamba suala la watu wa bara kwenda Zanzibar kwa passport lirudishwe! Ni wazi mapendekezo kama hayo ya kipumbavu yasingetokea katika kipindi cha raisi mwingine, bali kunakuwa na ujasiri wa kuyatoa chini ya Raisi Samia.
Sasa kumlaumu Tundu Lissu kwa kauli aliyotoa juu ya Raisi wa Zanzibar kufukuza Wamasai ni kumwonea. Tundu Lissu alichofanya ni kueleza hisia za Watanzania bara wenye akili timamu karibu wote. Ni wale tu ambao hawana uwezo wa kufikiri ulio sawa watapingana na Lissu, na sio kwa sababu kuna tatizo katika kauli ya Lissu, bali kwa sababu nafasi walizonazo katika uongozi wa serikali zinawataka wamkosoe Lissu. Ndani ya mioyo ya hawa watu wanajua Tundu Lissu anaongea ukweli.
Sasa, onyo langu kwa serikali ni kwamba inabidi iwe makini sana na suala hili la muungano. Hata Raisi Samia mwenyewe, japo ni raisi wa Tanzania, hapaswi kujisahau kwamba yeye ni Mzanzibar, na yapo mambo ambayo ni afadhali asiyafanyie uamuzi kwa sababu yana "political sensitivity" katika context ya kwamba yeye ni Mzanzibar. Hii ni pamoja na uamuzi ambao binafsi naona haukuwa wa busara wa mkataba wa bandari za bara, ajira za Wazanzibar upande wa bara, teuzi zake nk. Raisi Samia aliamua kupambana na watu wa bara katika hili, akijua yeye na Waziri wa Miundombinu, wenye maamuzi makubwa juu ya huu mkataba, walikuwa Wazanzibar. Hilo lilikuwa kosa (political blunder) hata kama mkataba unaweza uwe na manufaa.
Kuna maamuzi ambayo Raisi Samia anapaswa kutumia busara ya kuyaacha hadi raisi kutoka bara aje awe madarakani na ayashughulikie, pamoja na mikataba yenye impact kubwa upande wa bara. Raisi Samia, kama atatumia busara, atakuwa mwangalifu sana katika kufanya maamuzi ambayo yanaathiri watu wa bara na sio watu wa Zanzibar, japo yanafanyika katika kivuli cha muungano. Kama hatafanya hivyo, basi aelewe wazi kwamba vyama kama Chadema watatumia maamuzi hayo ili kujaribu kumwondoa madarakani. Asisahau kwamba ni Watanzania bara wanaomuweka raisi madarakani kwa sababu ya wingi wao. Lissu anajua hilo, na Chadema hawatakuwa hawajaiva kisiasa kama hawatalitumia hilo katika njia yenye akili kujaribu kuiondoa CCM madarakani.
Pia soma
Rais Mzanzibari amezitoa bandari zetu watanganyika kwa waarabu amewahamisha ndugu zetu Wamasai toka ngorongoro na loliondo.
Na amini nakuambia, kadiri unavyozidi kusikia kero za muungano zinapatiwa "ufumbuzi" ndivyo ambavyo Zanzibar inazidi kujiondoa kwenye muungano huku ikinufaika na muungano. Na naamini hakuna kipindi ambacho "kero za muungano" zimetatuliwa nyingi na kwa kasi kama kipindi cha Raisi Samia. Jiulize, ni kwa nini?wazanzibar wametuchezea na kudeka kwa miaka mingi sana. ifike mahali tumwage tu mboga na ugali.
Kwamba Rais wa Tanzania anamipaka yake kwa nchi ya Tanzania? Kwahiyo ni Rais wa nchi gani?
Mimi sidhani ni tatizo tena kwa Chadema kutumia suala la U-Zanzibar wa Raisi Samia kuwaondoa CCM madarakani, kwa sababu huo ndio ukweli. Kwa hatua tuliyofikia kwa kile ambacho wanaita "wameondoa kero za Muungano"sioni kwa nini serikali ya muungano iwe na raisi kutoka Zanzobar, kwa sababu serikaliya muungano imebaki na mambo yanayohusu bara peke yake.Hii inshu ingekua nchi nyingine tyr kingekuwa kimewaka. Watz ni wapole kwa kweli. Nchi ya amani hii
Na sasa mambo ya muungano hayaihusu Zanzibar, isipokuwa pale Zanzibar inapokuwa na maslahi. Halafu Tundu akisema analaumiwa?Ni Muungano wa kipuuzi kabisa. Rais wa JMT ana mamlaka ya kila kitu kwa Tanganyika, hata yasiyo ya Muungano, ila kwa Zanzibar, Rais wa JMT hana chake, isipokuwa kwa mambo ya muungano tu!!
marais wa zanzibar ni wangapi? Ali Hassan Mwinyi ni wa kwenu, na yeye mwenyewe alifafanua kwenye kitabu chake. Alikwenda Zanzibar kwa ajili ya kupata elimu akabakia kule, sasa tena hao marais wako wapi? Miaka 57 mumetutawala, bado tu munalalamika na hiyo mitatu ya Samia?
Hii inshu ingekua nchi nyingine tyr kingekuwa kimewaka. Watz ni wapole kwa kweli. Nchi ya amani hii
Hivi wasiotaka serikali 3 ndani ya CCM ni nani hasa? Tusisahau Zanzibar wameshawatambua baadhi ya viongozi wa bara ndani ya CCM ambao hawana uwezo wa kufikiri zaidi ya kufurahia nafasi zao, ambao wameamua kuwatumia kiawswasa. Hao watu ni wasaliti wa watu wa bara, wanatumika wakijua wanatumika lakini wakiona ni sawa kutumika kwa maslahi yao binafsi.Kwa sababu serikali 3, CCM hawataki. Na Serikali 1 imeshindikana. Hivyo serikali ya Muungano ndiyo serikali ya Tanganyika, basi iwe marufuku Mzanzibari kuwa Rais wa JMT, kwani haitakuwa sahihi mzanzibari kuwa Rais wa Tanganyika iliyojificha ndani ya JMT.
Mimi sidhani ni tatizo tena kwa Chadema kutumia suala la U-Zanzibar wa Raisi Samia kuwaondoa CCM madarakani, kwa sababu huo ndio ukweli. Kwa hatua tuliyofikia kwa kile ambacho wanaita "wameondoa kero za Muungano"sioni kwa nini serikali ya muungano iwe na raisi kutoka Zanzobar, kwa sababu serikaliya muungano imebaki na mambo yanayohusu bara peke yake.
Nadhani hili suala linapaswa liende hadi ndani ya Katiba, kwamba kwa sababu serikali ya Zanzibar ina raisi wake na mamlaka yake, basi siku zote raisi wa muungano LAZIMA atoke bara, na makamu wake atoke visiwani. ISIPOKUWA, ikiwa Raisi wa muungano atakufa, basi makamu wa raisi kutoka Zanzibar atakaimu kiti cha uraisi kwa kipindi kisichozidi mwaka moja, ambapo ndani ya kipindi hicho uchaguzi wa raisi utaitishwa. Na atakapokuwa akikaimu kiti cha uraisi, atakuwa na limited powers of authority katika kufanya maamuzi.
Ukifanya jamba baya, ni vizuri kuambiwa, na ni sahihi kuchukiwa kwa machukizo uliyoyanya.Tatizo sio kuitwa mzanzibari,Hoja ni kunasibisha matendo au shutuma zao kwake na uzanzibari wake, ni lugha ya uchochozi kabisa inayeeneza chuki.
Hii kitu imeniuma sana
Nilikuwa timu Mama sana . Kitendo cha TPA NA WAMASAI, imebidi nirudi nyuma
Watoto Zake na jamaa zake kawaingiza sana kwenye UDC na UDED, anaamini watanganyika hatuoni na kujua