Kauli ya Lissu ya Rais Mzanzibar ni matokeo ya kufumba masikio Tanganyika kuwa na Serikali yake na viongozi wake watakaoamua mambo yao, asilaumiwe!

Kwa sababu serikali 3, CCM hawataki. Na Serikali 1 imeshindikana. Hivyo serikali ya Muungano ndiyo serikali ya Tanganyika, basi iwe marufuku Mzanzibari kuwa Rais wa JMT, kwani haitakuwa sahihi mzanzibari kuwa Rais wa Tanganyika iliyojificha ndani ya JMT.
ha haa! yaani siku zote nyinyi muwe watawala sisi tuwe watawaliwa, unadhani hiyo ni sawa?
 
Mbona huyo Mwinyi amezikwa Zanzibar, na kijana wake ni Rais huko pia.
Inakuajee hapoo??
si ni CCM (Magu) ndiyo wamemuweka madarakani? Na huyu Mheshimiwa si aliwahi kuwa mbunge wa Mkuranga baadae ndiyo akaondoka na kwenda kupewa jimbo Zanzibar, au umesahau hiyo?

Wacha tunyamaze tu.
 
Kila marais wakitokea upande wa Zanzibar wanafanya maamuzi ya kuiumiza Tanganyika.
Sijawahi sikia rais Mtanganyika katoa ardhi ya Zanzibar kwa wawekezaji au kauza bandari au rasilimali yoyote kubwa ya Zanzibar kwa wageni.

Samia anafanya makosa makubwa sana
Huko kwenye ardhi ni mbali sana, hata ateue mtu wa bara akawe DC Unguja tu
 
Huu ndiyo udhaifu wenyewe wa Muungano. Aidha huu muungano uwe wa Serikali 3 ili kila mtu awe na maamuzi na mambo yake au Serikali moja au uvunjwe kabisa maana ni full unafiki kwa hali ilivyo sasa.

Unashangaa unaenda Wilaya za ndani ndani huko unakuta kuna watumishi Wazanzibar unajiuliza hivi mjini Magharibi unaweza kukuta Afisa Afya Mtanganyika?
Yeah,kuna maafisa afya wa kiunguja huku Tanganyika wakati huo afya si swala la muungano
 
Kwanza niombe moderators muiache hii thread ijitegemee, inaenda mbali zaidi ya kauli ya Lissu.

Kama una akili timamu na za kutosha, utakuwa umegundua kwamba suala la kusema kero za muungano zinatatuliwa limekuwa ni suala la kuzidi kuipa Zanzibar mamlaka yake kama nchi kamili na kuiondoa kwenye mambo yanayohusu muungano. Hii inatia ndani kuwapa zaidi nafasi waZanzibar kufanya kazi upande wa bara, si katika taasisi za muungano tu, bali hata maeneo ambayo sio ya muungano. Na tunajua ukweli suala hili limekua kubwa sana kipindi hiki cha Raisi Samia.

Sasa nyie watu mnaojiita viongozi wetu mkidhani kwamba watu wa bara hawaoni hili, basi mnajidanganya. In fact viongozi wa bara mnaoshupalia kumlaumu Lissu kwa kauli yake mnaonekana kama wasaliti wa Tanganyika, traitors. Kila mtu wa bara kwa sasa anaona ukweli kwamba katika suala la Muungano, Zanzibar ina mamlaka kamili kama nchi japo kuna kidanganyio cha muungano, wakati rasirimali za bara zinazidi kuibeba Zanzibar kila siku kwa kisingizio cha muungano. Zanzibar walipohisi kuna mafuta visiwani waliamua mafuta yaondolewe kwenye muungano. Mnafikiri watu wa bara hawaoni haya?

Angalia suala la umeme. Kimsingi, Zanzibar hawataki kulipia umeme. Wanakopa umeme wa Tanesco, deni linafikia mabilioni, wakiambiwa walipe wanakuja juu. Tanesco wanakatazwa kuwakatia umeme au hata kuwadai, wanaambiwa ni suala linashughulikiwa huko juu. Matokeo ni kwamba watumiaji wa umeme bara inabidi watozwe bei kubwa ya umeme ili kufidia umeme ambao Zanzibar wanatumia lakini kama serikali hawataki kuulipia! Hata wewe msomaji wa bara unalipia bili yako ya umeme kwa kuchangia kuwapa Zanzibar umeme wa bure! Sasa wao kulipia umeme hiyo nayo ni kero ya muungano?

Mfano mwingine. Zanzibar wanaruhusiwa kumiliki ardhi bara, lakini watu wa bara hawawezi kumiliki ardhi Zanzibar kwa kisingizio Zanzibar ni kisiwa kidogo. Sasa kama ni kisiwa kidogo, si ndio maana Wa Zanzibar wanaruhusiwa kuhamia bara? Ingekuwa sawa kusema ni kisiwa kidogo kama Wazanzibar wasingeruhusiwa kumiliki ardhi upande wa bara. Sasa unaruhusu waje bara kupunguza pressure ya population kule, lakini unasema watu wa bara msinunue ardhi Zanzibar. Unawahadaa nani kwa kisingizio hiki, watu wa bara? Kwa sababu tunajua sababu ya kuwanyima watu wa bara kununua ardhi Zanzibar sio upungufu wa ardhi. Kama ardhi ya kununua haipo basi haitawezekana kununua, na watu watajipatia ardhi bara. Sio rahisi kununua ardhi Moshi kwa sababu hakuna ardhi ya kununua, sasa leo utasema Wasukuma wasinunue ardhi Moshi kwa sababu Moshi kuna upungufu wa ardhi kwa ajili ya Wachaga, una akili sawasawa wewe?

Zanzibar sasa imekuwa ikifanya kitu kinaitwa "cherry picking" kuamua nini kiwe katika muungano, na inaonyesha wazi kwamba katika suala la wao kufanya hivyo, watu wa bara hawatakiwi kupinga lolote. Na tunajua kwamba kwa sasa Zanzibar wanatumia nafasi ya uwepo wa Rais Samia kwenye kiti cha Uraisi kama nafasi pekee ya kuvutia mambo mengi upande wao. Hilo sio siri.

Zanzibar wamejisahau sana katika kuvutia upande wao hadi imefikia watu wachache wameanza kudokeza kwamba suala la watu wa bara kwenda Zanzibar kwa passport lirudishwe! Ni wazi mapendekezo kama hayo ya kipumbavu yasingetokea katika kipindi cha raisi mwingine, bali kunakuwa na ujasiri wa kuyatoa chini ya Raisi Samia.

Sasa kumlaumu Tundu Lissu kwa kauli aliyotoa juu ya Raisi wa Zanzibar kufukuza Wamasai ni kumwonea. Tundu Lissu alichofanya ni kueleza hisia za Watanzania bara wenye akili timamu karibu wote. Ni wale tu ambao hawana uwezo wa kufikiri ulio sawa watapingana na Lissu, na sio kwa sababu kuna tatizo katika kauli ya Lissu, bali kwa sababu nafasi walizonazo katika uongozi wa serikali zinawataka wamkosoe Lissu. Ndani ya mioyo ya hawa watu wanajua Tundu Lissu anaongea ukweli.

Sasa, onyo langu kwa serikali ni kwamba inabidi iwe makini sana na suala hili la muungano. Hata Raisi Samia mwenyewe, japo ni raisi wa Tanzania, hapaswi kujisahau kwamba yeye ni Mzanzibar, na yapo mambo ambayo ni afadhali asiyafanyie uamuzi kwa sababu yana "political sensitivity" katika context ya kwamba yeye ni Mzanzibar. Hii ni pamoja na uamuzi ambao binafsi naona haukuwa wa busara wa mkataba wa bandari za bara, ajira za Wazanzibar upande wa bara, teuzi zake nk. Raisi Samia aliamua kupambana na watu wa bara katika hili, akijua yeye na Waziri wa Miundombinu, wenye maamuzi makubwa juu ya huu mkataba, walikuwa Wazanzibar. Hilo lilikuwa kosa (political blunder) hata kama mkataba unaweza uwe na manufaa.

Kuna maamuzi ambayo Raisi Samia anapaswa kutumia busara ya kuyaacha hadi raisi kutoka bara aje awe madarakani na ayashughulikie, pamoja na mikataba yenye impact kubwa upande wa bara. Raisi Samia, kama atatumia busara, atakuwa mwangalifu sana katika kufanya maamuzi ambayo yanaathiri watu wa bara na sio watu wa Zanzibar, japo yanafanyika katika kivuli cha muungano. Kama hatafanya hivyo, basi aelewe wazi kwamba vyama kama Chadema watatumia maamuzi hayo ili kujaribu kumwondoa madarakani, na watanzania bara wote wenye akili wanapaswa kuwaunga mkono. Raisi Samia asisahau kwamba ni Watanzania bara wanaomuweka raisi madarakani kwa sababu ya wingi wao. Lissu anajua hilo, na Chadema watakuwa hawajaiva kisiasa kama hawatalitumia hilo katika njia yenye akili kujaribu kuiondoa CCM madarakani.

Pia soma
Zanzibar imeunga na Tanganyika, katika porojo lako lote hili haukutaja neno Tanganyika hata mara moja. Sijajua unazungumzia muungano gani, laiti ungetumia akili kidogo tu basi ungelijua kutokuwepo Tanganyika hapo ndio shida zote zinaanzia. Mitano tena mama, mpaka waseme. Akili nyingi mbele kiza, Watanganyika tulieni acheni kujazana ujinga.
 
Ukiona hoja nzito kama za Tundu Lissu , tena za Kisheria zinajibiwa na Nape Mnauye .. ujue kitu kimegonga ! Nape Ndio Think Tank ya CCM kujibu hoja nzito za Kisheria ! Zingekuwa ni hoja nyepesi AG angejibu Kwa niaba ya Serikali!
 
Kwanza niombe moderators muiache hii thread ijitegemee, inaenda mbali zaidi ya kauli ya Lissu.

Kama una akili timamu na za kutosha, utakuwa umegundua kwamba suala la kusema kero za muungano zinatatuliwa limekuwa ni suala la kuzidi kuipa Zanzibar mamlaka yake kama nchi kamili na kuiondoa kwenye mambo yanayohusu muungano. Hii inatia ndani kuwapa zaidi nafasi waZanzibar kufanya kazi upande wa bara, si katika taasisi za muungano tu, bali hata maeneo ambayo sio ya muungano. Na tunajua ukweli suala hili limekua kubwa sana kipindi hiki cha Raisi Samia.

Sasa nyie watu mnaojiita viongozi wetu mkidhani kwamba watu wa bara hawaoni hili, basi mnajidanganya. In fact viongozi wa bara mnaoshupalia kumlaumu Lissu kwa kauli yake mnaonekana kama wasaliti wa Tanganyika, traitors. Kila mtu wa bara kwa sasa anaona ukweli kwamba katika suala la Muungano, Zanzibar ina mamlaka kamili kama nchi japo kuna kidanganyio cha muungano, wakati rasirimali za bara zinazidi kuibeba Zanzibar kila siku kwa kisingizio cha muungano. Zanzibar walipohisi kuna mafuta visiwani waliamua mafuta yaondolewe kwenye muungano. Mnafikiri watu wa bara hawaoni haya?

Angalia suala la umeme. Kimsingi, Zanzibar hawataki kulipia umeme. Wanakopa umeme wa Tanesco, deni linafikia mabilioni, wakiambiwa walipe wanakuja juu. Tanesco wanakatazwa kuwakatia umeme au hata kuwadai, wanaambiwa ni suala linashughulikiwa huko juu. Matokeo ni kwamba watumiaji wa umeme bara inabidi watozwe bei kubwa ya umeme ili kufidia umeme ambao Zanzibar wanatumia lakini kama serikali hawataki kuulipia! Hata wewe msomaji wa bara unalipia bili yako ya umeme kwa kuchangia kuwapa Zanzibar umeme wa bure! Sasa wao kulipia umeme hiyo nayo ni kero ya muungano?

Mfano mwingine. Zanzibar wanaruhusiwa kumiliki ardhi bara, lakini watu wa bara hawawezi kumiliki ardhi Zanzibar kwa kisingizio Zanzibar ni kisiwa kidogo. Sasa kama ni kisiwa kidogo, si ndio maana Wa Zanzibar wanaruhusiwa kuhamia bara? Ingekuwa sawa kusema ni kisiwa kidogo kama Wazanzibar wasingeruhusiwa kumiliki ardhi upande wa bara. Sasa unaruhusu waje bara kupunguza pressure ya population kule, lakini unasema watu wa bara msinunue ardhi Zanzibar. Unawahadaa nani kwa kisingizio hiki, watu wa bara? Kwa sababu tunajua sababu ya kuwanyima watu wa bara kununua ardhi Zanzibar sio upungufu wa ardhi. Kama ardhi ya kununua haipo basi haitawezekana kununua, na watu watajipatia ardhi bara. Sio rahisi kununua ardhi Moshi kwa sababu hakuna ardhi ya kununua, sasa leo utasema Wasukuma wasinunue ardhi Moshi kwa sababu Moshi kuna upungufu wa ardhi kwa ajili ya Wachaga, una akili sawasawa wewe?

Zanzibar sasa imekuwa ikifanya kitu kinaitwa "cherry picking" kuamua nini kiwe katika muungano, na inaonyesha wazi kwamba katika suala la wao kufanya hivyo, watu wa bara hawatakiwi kupinga lolote. Na tunajua kwamba kwa sasa Zanzibar wanatumia nafasi ya uwepo wa Rais Samia kwenye kiti cha Uraisi kama nafasi pekee ya kuvutia mambo mengi upande wao. Hilo sio siri.

Zanzibar wamejisahau sana katika kuvutia upande wao hadi imefikia watu wachache wameanza kudokeza kwamba suala la watu wa bara kwenda Zanzibar kwa passport lirudishwe! Ni wazi mapendekezo kama hayo ya kipumbavu yasingetokea katika kipindi cha raisi mwingine, bali kunakuwa na ujasiri wa kuyatoa chini ya Raisi Samia.

Sasa kumlaumu Tundu Lissu kwa kauli aliyotoa juu ya Raisi wa Zanzibar kufukuza Wamasai ni kumwonea. Tundu Lissu alichofanya ni kueleza hisia za Watanzania bara wenye akili timamu karibu wote. Ni wale tu ambao hawana uwezo wa kufikiri ulio sawa watapingana na Lissu, na sio kwa sababu kuna tatizo katika kauli ya Lissu, bali kwa sababu nafasi walizonazo katika uongozi wa serikali zinawataka wamkosoe Lissu. Ndani ya mioyo ya hawa watu wanajua Tundu Lissu anaongea ukweli.

Sasa, onyo langu kwa serikali ni kwamba inabidi iwe makini sana na suala hili la muungano. Hata Raisi Samia mwenyewe, japo ni raisi wa Tanzania, hapaswi kujisahau kwamba yeye ni Mzanzibar, na yapo mambo ambayo ni afadhali asiyafanyie uamuzi kwa sababu yana "political sensitivity" katika context ya kwamba yeye ni Mzanzibar. Hii ni pamoja na uamuzi ambao binafsi naona haukuwa wa busara wa mkataba wa bandari za bara, ajira za Wazanzibar upande wa bara, teuzi zake nk. Raisi Samia aliamua kupambana na watu wa bara katika hili, akijua yeye na Waziri wa Miundombinu, wenye maamuzi makubwa juu ya huu mkataba, walikuwa Wazanzibar. Hilo lilikuwa kosa (political blunder) hata kama mkataba unaweza uwe na manufaa.

Kuna maamuzi ambayo Raisi Samia anapaswa kutumia busara ya kuyaacha hadi raisi kutoka bara aje awe madarakani na ayashughulikie, pamoja na mikataba yenye impact kubwa upande wa bara. Raisi Samia, kama atatumia busara, atakuwa mwangalifu sana katika kufanya maamuzi ambayo yanaathiri watu wa bara na sio watu wa Zanzibar, japo yanafanyika katika kivuli cha muungano. Kama hatafanya hivyo, basi aelewe wazi kwamba vyama kama Chadema watatumia maamuzi hayo ili kujaribu kumwondoa madarakani, na watanzania bara wote wenye akili wanapaswa kuwaunga mkono. Raisi Samia asisahau kwamba ni Watanzania bara wanaomuweka raisi madarakani kwa sababu ya wingi wao. Lissu anajua hilo, na Chadema watakuwa hawajaiva kisiasa kama hawatalitumia hilo katika njia yenye akili kujaribu kuiondoa CCM madarakani.

Pia soma
Lissu anahitajika kushughulikiwa. Kuchochea ubaguzi haijawahi kuwa uhuru wa kujieleza. Lissu ni kirusi and should be treated as such!
 
Na amini nakuambia, kadiri unavyozidi kusikia kero za muungano zinapatiwa "ufumbuzi" ndivyo ambavyo Zanzibar inazidi kujiondoa kwenye muungano huku ikinufaika na muungano. Na naamini hakuna kipindi ambacho "kero za muungano" zimetatuliwa nyingi na kwa kasi kama kipindi cha Raisi Samia. Jiulize, ni kwa nini?
kama kuna kitu kinaitwa kero za muungano, ulishawahi kusikia wapi kuna kero ya watanganyika? yaani ni kama mchepuko vile, kero zote ni zao, sisi hakuna hata tunacholalamika, wakati hakuna hata tunachofaidika. wanini sasa hawa?
 
Hii kitu imeniuma sana
Nilikuwa timu Mama sana . Kitendo cha TPA NA WAMASAI, imebidi nirudi nyuma

Watoto Zake na jamaa zake kawaingiza sana kwenye UDC na UDED, anaamini watanganyika hatuoni na kujua
Bahati mbaya historia hiyo ya chifu Hagaya itabaki kwenye kumbukumbu kama historia ya chifu Mangungo.
 
Rais Samia aliisha sema yeye hana kabila bali ni Mzanzibar. Nape unapojibu hoja nenda na context ya mazingira ya sasa kipindi cha siasa za akina Malechela miaka ya 80 imebadilika mno
Kwani kuitwa mzanzibar ni dhambi?
 
Ni Muungano wa kipuuzi kabisa. Rais wa JMT ana mamlaka ya kila kitu kwa Tanganyika, hata yasiyo ya Muungano, ila kwa Zanzibar, Rais wa JMT hana chake, isipokuwa kwa mambo ya muungano tu!!
Tanganyika imevaa koti la muungano na Rais wa muungano ni mzenji poleni sana
 
Ukifanya jamba baya, ni vizuri kuambiwa, na ni sahihi kuchukiwa kwa machukizo uliyoyanya.

Wewe unaweza kuwa na sababu nzuri za kwa nini;
1) wahusika wakuu wote wa kuuza bandari za Tanganyika ni Wazanzibari?

2) Kama IGA iliyopoteza sovereignity ya nchi kwenye maamuzi yahusuyo bandari, bandari za Zanzibar hazimo?

3) Mbuga za wanyama na hifadhi za misitu zote walizopewa waarabu ni za Tanganyika, na hakuna japo fukwe moja ya Zanzibar waliyopewa waarabu?

Kama kweli uzanzibari wake ndio uliomfanya agawe bandari na mbuga kwa waarabu, wakati anafanya hayo
Kwanini Serikali ilimuachia? kuanzia Bunge mawaziri wakurugenzi amabao 95% ni watanganyika?
Kwa nini chama chake cha CCM kilimuachia ambacho zaidi ya 90% ya viongozi wake na wafuasi wake ni watanganyika?
Kwanini JWTZ ilimuachia wakati zaidi ya 90% ni watanganyika?
Na kwanini TISS walimuachia ambao nao zaidi ya 90% ni watanganyika?

Mkuu munachokifanya ni kueneza chuki, nchi nyingi ambazo leo hazikaliki kwa civil wars zilianza na chokochoko kama hizi.
 
Mimi sidhani ni tatizo tena kwa Chadema kutumia suala la U-Zanzibar wa Raisi Samia kuwaondoa CCM madarakani, kwa sababu huo ndio ukweli. Kwa hatua tuliyofikia kwa kile ambacho wanaita "wameondoa kero za Muungano"sioni kwa nini serikali ya muungano iwe na raisi kutoka Zanzobar, kwa sababu serikaliya muungano imebaki na mambo yanayohusu bara peke yake.

Nadhani hili suala linapaswa liende hadi ndani ya Katiba, kwamba kwa sababu serikali ya Zanzibar ina raisi wake na mamlaka yake, basi siku zote raisi wa muungano LAZIMA atoke bara, na makamu wake atoke visiwani. ISIPOKUWA, ikiwa Raisi wa muungano atakufa, basi makamu wa raisi kutoka Zanzibar atakaimu kiti cha uraisi kwa kipindi kisichozidi mwaka moja, ambapo ndani ya kipindi hicho uchaguzi wa raisi utaitishwa. Na atakapokuwa akikaimu kiti cha uraisi, atakuwa na limited powers of authority katika kufanya maamuzi.

Ukifanya jamba baya, ni vizuri kuambiwa, na ni sahihi kuchukiwa kwa machukizo uliyoyanya.

Wewe unaweza kuwa na sababu nzuri za kwa nini;
1) wahusika wakuu wote wa kuuza bandari za Tanganyika ni Wazanzibari?

2) Kama IGA iliyopoteza sovereignity ya nchi kwenye maamuzi yahusuyo bandari, bandari za Zanzibar hazimo?

3) Mbuga za wanyama na hifadhi za misitu zote walizopewa waarabu ni za Tanganyika, na hakuna japo fukwe moja ya Zanzibar waliyopewa waarabu?
Katika orodha ya mambo ya muungano Ardhi ya tanganyika hakuwemo ni nani aliengiza katika muungano? Na kwa nini Alifanya hivo?
 
Huu ndiyo udhaifu wenyewe wa Muungano. Aidha huu muungano uwe wa Serikali 3 ili kila mtu awe na maamuzi na mambo yake au Serikali moja au uvunjwe kabisa maana ni full unafiki kwa hali ilivyo sasa.

Unashangaa unaenda Wilaya za ndani ndani huko unakuta kuna watumishi Wazanzibar unajiuliza hivi mjini Magharibi unaweza kukuta Afisa Afya Mtanganyika?
Shaka Hamduni Shaka
 
Waimbaji wa mapambio hili pambio la Uzanzibar wa mkuu mbona kama hamlipendi vile. Ongezeni sauti, watanganyika wasikie vizuri 🤣🤣😂
 
marais wa zanzibar ni wangapi? Ali Hassan Mwinyi ni wa kwenu, na yeye mwenyewe alifafanua kwenye kitabu chake. Alikwenda Zanzibar kwa ajili ya kupata elimu akabakia kule, sasa tena hao marais wako wapi? Miaka 57 mumetutawala, bado tu munalalamika na hiyo mitatu ya Samia?
tumewatawalaje sasa? Rais mnae wa kwenu na serikali yenu, sisi tanganyika hatuna rais pia hatuna tulichonufaika kuungana na nyinyi zaidi ya kero makerere ulalamishi na pia sisi watanganyika kupata hasara kuungana na kainchi masikini kasiko na rasilimali yoyote kenye watu wavivu kufanya kazi wenye kupenda misaada.! Sisi tuna kila kitu kuanzia madini aina zote, tuna maziwa na mito na bahari, tuna misitu na mashamba makubwa kujitosheleza, tunawatu wenye nguvu ya kufanya kazi na pia bado tuna maadili na uvumilivu wa kiimani yani mkiristo muislamu na mpagani wote wanachangamana na hakuna shida, halafu imekua vema nyie kutawala ili tuwajue rangi zenu halisi. Ili akija rais mtanganyika jambo la kwanza n kuvunja muungano na kufukuza kila mzanzibari aliyeko tanganyika ili muishi kwa misaada ya hao warabu wenu. Sasa sijui warabu washindwe kupeleka misaada palestina halafu walete zanzibar inafikirisha sana. Yote kwa yote tumewachoka bandari zetu na wanyama wetu wanatuuma sanaa!
 
Nisha uliza swali,lakini mpaka sasa sijapata jawabu nadhani hapa naweza pata jibu la swali langu.

Ni nani aliye iuza Tanganyika na Mali zake zote kuwa za Muungano ?
 
Kwa sababu serikali 3, CCM hawataki. Na Serikali 1 imeshindikana. Hivyo serikali ya Muungano ndiyo serikali ya Tanganyika, basi iwe marufuku Mzanzibari kuwa Rais wa JMT, kwani haitakuwa sahihi mzanzibari kuwa Rais wa Tanganyika iliyojificha ndani ya JMT.
Mkuu heshima kwako.

Serikali ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania haiwezi kuwa serekali ya Tanganyika,kwa sababu Tanganyika haipo.Ndio maana ni ngumu kutetea kitu ambacho hakipo.Zanzibar ni rahisi kutetea maslahi yao sababu serikali ya MP ipo kwa ajili ya Zanzibar.

Mimi napenda kujua ni nani aliye iuza Tanganyika yetu na maslahi yetu ?
 
Back
Top Bottom