Kauli ya Magufuli kuwa Kabudi na Lukuvi hawatagombea Urais haikuwa ya ghafla, ilipangwa siku nyingi na ndio mwanzo wa mgogoro ndani ya CCM

Kwa taaluma ya urais (kama ipo) anayekidhi ni Lukuvi, ni mtu anayeweza kusimamia kitu chochote hata kama hajakisomea, alimradi aweze kuzitawala vema rasilimali zilizoko mbele yake kufanikisha malengo yaliyokusudiwa. Hao wa PhD wanaweza kurudi kwenye taaluma za hizo PhDs ndiko wana nafasi ya kung'ara zaidi katika kutengeneza wataalamu wengi wa fani zao.
 
Good point. Ila sasa tatizo la Lukuvi ni kwamba hana confidence, na inawezekana ni kutokana na exposure ndogo. Atakuwa mtu wa kukaa ndani tu kama Magufuli.

By the way, katika hizi nchi zetu, kitu kimoja kinachowapa viongozi wetu confidence ya kuwakabili viongozi wa nchi tajiri ni uwezo wa kuongea lugha ya Kiingereza. Upende usipende huo ndio ukweli.

Wewe fikiria, wewe ndio raisi, una wasaidizi wako na Joe Bidden amewatembelea ikulu, kila sentensi Bidden akiongea unamuuliza msaidizi wako jamaa kasema nini? Na kumjibu Bidden unaogopa maana wasaidizi wako wengine wanaongea kiingereza vizuri kukuzidi, unaogopa ku-break mbele yao. Kuomba uongee Kiswahili utafsiriwe unaona aibu maana watu wanajua una PhD kwa hiyo wanategemea lugha ya Malkia ipande. Ni tatizo!

Sasa huyu Lukuvi mzee wa watu kazoea Kihehe kusema tantalizing hawezi anasema tendalizing, pantoni anaita pandoni, tutafika kweli?
 
Most likely ni Hussein Mwinyi.
Jafo atakuwa Waziri Mkuu, na atafaa sana.
CCM wataweka mgombea wa uraisi kutoka visiwani wakijua kwa uhakika kwamba wamekubuhu katika namna mbalimbali za kuiba kura hata washindwe vipi watageuza matokeo. La sivyo siku wanaweka mgombea wa visiwani kuwania uraisi ndio siku upinzani watachukua nchi, maana hata Zanzibar watampigia mpinzani ili akipita avunje muungano
 
Kabudi ni useless, ana vimaneno vya kiji.nga utadhani si mwanasheria, mara heshima ambayo sikustahili, mara umenitoa jalalani!none sense!
 
Lukuvi hana PhD lakini anaongea English vizuri. Nilishamsikia mara kadhaa.
 
Kuna memba humu alishaambia akaandika na uzi huu , Mahesabu makali ya Mzee Ally Hassan Mwinyi , mmesahau , alisema wakati wa kikao cha mkutano mkuu kuchagua mgombea urais ccm kuwa rais Magufuri aongeze muda wa miaka mitano , ili mwanae Hussein Mwinyi atimize miaka kumi Zanzibar ili baadaye aje amrithi Magufuri . Haya Sasa mnaiona hii coincidence ?
 

Kabudi hana akili hiyo, labda kama unacheza mind games.
 
Very sad. Wamekosa sifa gani? Kwani katiba inasema anayezidi umri gani ndio asigombee urais?
Inasikitisha sana rais wa nchi badala ya kuchaguliwa na wananchi, tunachaguliwa na Mwenyekiti wa CCM

Magufuli ni mtu wa ajabu sana.

Anahimiza watu kwamba uchaguzi umekwisha, tuchape kazi sasa.

Halafu hapo hapo anaanzisha habari za nani atakuwa rais wa kumrithi na nani hawezi kuwa rais, kimsingi anaanza kampeni za urais tena hata kabla ya kufanya kazi ya urais kwa mwezi tu!

CCM huwa wana tabia ya kuanzisha vigezo ambavyo havipo katika katiba ili kumkata mtu fulani.

Kwa mfano, walipotaka kumkata marehemu Samwel Sitta kwenye Uspika wa Bunge, walileta kigezo ambacho hakipo kwenye katiba yoyote, kwamba wanataka Spika mwanamke.

Walipotaka kumkata Lowassa, walileta kigezo cha umri.

Na sasa Magufuli anaendeleza tu kigezo hiki cha umri ambacho hakipo katika katiba yoyote.

Mimi si mtetezi wa Kabudi wala Lukuvi, lakini, nchi hii marais hawachagui rais ajaye.

Ndiyo maana Nyerere hakumpata rais aliyemtaka, Salim Ahmed Salim.

Ndiyo maana Mkapa hakumpata Dr. Omar Ali Juma wala Abdallah Kigoda.

Ndiyo maana Kikwete hakumpata Membe.

Na zaidi, Magufuli akijifanya kuanza kumtangaza mgombea anayemtaka na kulazimisha awe rais ajaye, kama watu hawamtaki, watu wanaweza kumfanyia kitu mbaya kama alivyofanyiwa Dr. Omar Ali Juma.

Nakumbuka nilikaa na mtoto mmoja wa familia ya Mkapa, aliniambia "huyu Dr. Omar ndiye rais anayefuatia wa Tanzania". Hizo habari zilikuwa za kutoka nyumbani kwa Mkapa kabisa.

Kilichofuatia ni historia.
 
Singida labda?.
 
Kumbe kabudi pia nae ni chizi ,kwa kulopoka na kutuchonganisha na wahisani wetu

wadau wa maendeleo wakisusa wawekezaji , watalii na wafadhili wa miradi ya jamii watatoka wapi kama si do haohao anaowatukana

Jeuri zitamtokea puani mwendawazimu huyu
 
Hotuba ya Kabudi aliyotoa kwa wafanya kazi wa mambo ya ndani ina kila namna ya viashiria kwamba ameanza kujitofautisha ili watu waone anaweza kuwa raisi wa namna gani
 
Kumbe kabudi pia nae ni chizi ,kwa kulopoka na kutuchonganisha na wahisani wetu

wadau wa maendeleo wakisusa wawekezaji , watalii na wafadhili wa miradi ya jamii watatoka wapi kama si do haohao anaowatukana

Jeuri zitamtokea puani mwendawazimu huyu
Kama unaongelea aliyosema kwa wafanya kazi wake wa wizara ya mambo ya ndani, lengo lilikuwa ni mbali zaidi. Amejionyesha wazi jinsi gani yeye ni kiongozi bora zaidi hasa katika kushughulika na mambo ya kimataifa, kuifanya Tanzania iheshime nk. Huyu sio yule mtu anaesema nimeokotwa jalalani, ndio maana nikasema huwa anaamua kujishusha ili akwezwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…