Kauli ya Magufuli kuwa Kabudi na Lukuvi hawatagombea Urais haikuwa ya ghafla, ilipangwa siku nyingi na ndio mwanzo wa mgogoro ndani ya CCM

Hapana Mkuu. Hata Mkapa ambaye alikuwa ni rafiki mKubwa wa Magufuli, labda aliona mapungufu fulani ndani ya Magufuli hivyo hakumpa support yote ili kwenye mio za uraisi. Labda pia Mkapa hakutaka kugombana na Kikwete. Ndio maana Magufuli alisema wazi siku zote - hakuna anaemdai katika kuwa kwake raisi, ni juhudi zake peke yake.

Na labda kwa hasira ya Mkapa kutokuwa nae kwenye harakati a kumrithi Kikwete, Magufuli alipokuwa rahisi alikuwa hasikilizi chochote Mkapa alichomshauri. Na wala alikuwa ham-consult. Watu walianza kumlaumu Mkapa kuwa mtu wako Magufuli haambiliki, uwe unamshauri. Mkapa aliweka bayana kwamba hata yeye Magufuli hataki kabisa kumsikiliza, japo ni kweli yeye ndio aliyemfanya afike alipofika.

Ilifikia wakati Mkapa alikasirika akawa hahudhurii function yeyote ya kitaifa.Aliamua kukaa kando kabisa na mambo ya serikali, kama amesusa. Watu wenye busara wakamwambia Magufuli kwamba umeenda mbali sana na Mkapa, mwombe msamaha, huwezi kusahau mlikotoka. Nadhani katika maisha yake Magufuli ya uraisi, ni ushauri huo tu aliowahi kupokea, maana ni kweli alimalizana na Mkapa na Mkapa akawa anashiriki dhifa za kitaifa baada ya hapo.
 
Safu ya CCM 2025
1st preference =Majaliwa
2nd = Jafo
3rd= none
4th= none
Ni zamu ya Rais Muislamu.
Mkuu uraisi wa Tanzania sio uimamu au uaskofu. Sio jambo la zamu kwa mkristo au mwislamu. Tukianza hivyo hatutaishia hapo, tutasema ni zamu ya mwanamke, au Kanda ya Nyanda za juu, au Mchaga, au mwanasheria, nk
 
Swali aliandaliwa na nani?

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
Mkuu Matola katika kuandaliwa kuna yafuatayo:
Kwanza kunaandaliwa mazingira ya kisheria na kitaasisi ya mtu anayetarajiwa.. haya yalifanyika kabla ya uchaguzi wa 2015
Pili ni sarakasi na minyukano ya ndani ya chama ambaya yalifuatia - kumbuka idadi kubwa ya wagombea wa Urais 2015.
Tatu ni mazingira yaliyoandaliwa kumwangukia aliyeamuliwa..
Kuhusu nani alimwandaa.. jiulize maswali yafuatayo?
Nani walikuwa vyanzo vya haya mazingira? kisheria,kitaasisi.. 'definitely' siyo Rais aliyeko madarakani.. yeye alipewa tu sababu za kawaida za kuwepo kwa sheria zenyewe.. lakini 'central theme'.. asingeijua..
 
Kwa jinsi navyoona kuna uwezekano mkubwa Rais ajaye akawa ni Mwanamama. La hasha Rais atatokea Zanzibar, iwapo rais atatokea CCM.

Kuhusu Rais kutokea Zanzibar, ni suala la Legacy. Ukiangalia mfumo wa uongozi na utawala anaotumia Magufuli unaendana na maono ya mzee Nyerere.

Wakati Nyerere anang'atuka alituachia Mzee Mwinyi wa Zanzibar. Hivyo bila shaka na huyu mtawala atatuachia Mzanzibar Mwengine.

Ikishindikana na kukawa na vita kali kati ya vijana wafuatao CCM, Makamba, Jafo, Mwigulu, Kigwangala, Bashe, na Ndugai. Basi maajabu ya mwanamama kupitishwa na mkutano mkuu wa CCM kwa shinikizo la Mwenyekiti wao.

Above all, Tunaweza kuwa na Rais ambaye hatokani na Baraza la mawaziri kwa mara ya kwanza. Mheshimiwa anaweza kuamka na kuleta jina la mfukoni. Hapa tunaweza kuletewa Mkuu wa mkoa au Katibu wa wizara kama mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM.

Kama hujanielewa. Ki ufupi namaanisha Magufuli hasomeki.
 
Ina maana hao wajanja waliomwondoa Sokoine kimaajabu April 1984 walishajua mapema kwamba Nyerere alikuwa na mpango wa kung'atuka Novemba 1985?
 
Kabudi amehojiwa na Zuhura Yunusi yule mwandishi wa BBC swahili kwe tv inaitwa tanzanite online

ameonyesha hawezi kumudu jaziba yake anashindwa interview mara ya pili huyu hajamasta kwenye wizara yake anabebwa tuu

Hulka yake ya ubabe, maneno yasiyona busara na kuendekeza jazba kunamwonyesha jinsi anavyopwaya.
 
si bora hata lukuvi, huyo kabugi na mimacho yake hata akigombea nani atampigia kura?
 
Kumfananisha Magufuli na salakasi za Mzee wetu wa Msoga wakati wa kumtosa Mwandosya ni kituko ainasafu zao kiuongozi hazishabihiani.

Wakati JK alikuwa mnafiki kwa kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa asiowataka. JPM hamung'unyi maneno wala kukupa matumaini makubwa ili hali anajua sio chaguo lake. Wasio mfahamu wanadhani huu ni udhaifu au "ushamba" la! hasha hiyo ndio namna yake aliyojipambanua nayo na ikampa kura 12m.
Siasa za Magufuli amezipambanua kiuwazi kila mahali ili asikupotezee muda kuunda makundi au mkururo unaweza kuundwa na viongozi aliowataja ingawa nashawishika kuamini target ya ujumbe alikuwa Kabudi, maana ndio alishaanza kuwashawishi baadhi ya makatibu wakuu... (Wizara nazihifadhi) kuwa anachokishauri kwa mheshimiwa hakipingi! Huu ndio udhaifu wa Kabudi pia anapenda madaraka kwa njia za kubebwa na kulaghai.

JPM kama Mwenyekiti wao wa chama kusema kwake ni kufikisha ujumbe kwenye kambi zote zinazoanza kujiuunda.

Pia fitina zilizokuwepo kwenye baraza lililopita zimesababisha JPM kuwaambia wazi mawaziri waliopita kwa wasiende kwa waganga ilikupata uwaziri maana yake ni moja tu ndani yake kuna wezi na wabadhirifu, kuna waroho wa madaraka na wahudumu uchumi.

Haki ya kikatiba ya raia wa Tanzania mwenye sifa kuomba ridhaa na kuchaguliwa ipo ila ikiwa haki hiyo inatishia utulivu na amani ndani ya chama... Ni wajibu wa chama kutupia mwenyekiti kutuliza hali.

Kabudi na Lukuvi wakiona wamebanwa ili hali uwezo na uhitaji wa wananchi upo kwao sio lazima wabaki CCM ili kuweza wa marais.
 
Acha waambiwe maana hawana msaada wowote kwa taifa
Acha kudaganya umma

Wewe hujui faida na misaada tunayopata kwa wafadhilo, wahisani na wawezeshaji wabia wa maendeleo.

Labda haujui mifumo ya uendeshaji wa nchi maskini
 
Kwa hiyo alichosema Magufuli dhidi ya Lukuvi na Kabudi ndio msimamo wa CCM yote? Au ni kwamba unachosema ni kuwa anachosema Magufuli CCM lazima wafuate wapende wasipende?
 
Nakubali kabisa. Tena Kabudi ni aina ya watu ambao akiwa raisi atajua kwamba yeye ni raisi kwa kuwa anawazidi Watanzania wote akili!
 
Ina maana hao wajanja waliomwondoa Sokoine kimaajabu April 1984 walishajua mapema kwamba Nyerere alikuwa na mpango wa kung'atuka Novemba 1985?
Hewaaa! Actually, kuna watu walimfuata Nyerere kumwambia Sokoine alikuwa hajafa bado, na alikuwa ameuwawa "kimazingira". Hata walimwambia wangeweza kumrudisha na itabidi wafanye haraka kabla waliomchukua hawajamzuru zaidi au kumwondoa akili.

Kuna watu wenye dawa sijui, siku ya kuangalia maiti walisema walikuwa wanamwona yuko hai na wanashituka sana - kama unaweza kuupata huo mkanda utafute!

Wakamwambia kuwa waliofanya hivyo wanajulikana, na kwamba walimfuata Nyerere kumwambia Sokoine alikuwa anavuka mipaka, alitaka kuwaweka ndani mawaziri, na hivyo walihitaji kumdhibiti. Nyerere akawaambia kama mnaweza kumdhibiti mdhibitini, na wao wakaelewa aliwapa go ahead kumwondoa. Sasa aliyesema Sokoine alihitaji kudhibitiwa alikuwa mtu wa karibu sana na Nyerere. Nyerere akauliza, ina maana so and so anahusika pia? Wakajibu ndio. Nyerere akakasirika mno. Huyo so and so alipoenda kujieleza kwa Nyerere alifukuzwa kama mbwa!

Nyerere akawauliza, na tukimrudisha, baada ya kuitangazia dunia kuwa Waziri wetu Mkuu amekufa kwa ajali na tukapokea na salamu za rambirambi, tutaiambia nini dunia, na watatuoana sisi ni taifa la watu wa aina gani?

Akawaambia kama hajafa kabisa basi mmalizieni ili asiumizwe zaidi.
 
Hii chai tamu. Mhudumu aniongezee vitumbua viwili.
 
Kwa hiyo alichosema Magufuli dhidi ya Lukuvi na Kabudi ndio msimamo wa CCM yote? Au ni kwamba unachosema ni kuwa anachosema Magufuli CCM lazima wafuate wapende wasipende?
Sina hakika kama msimamo wa mwenyekiti ndio wa chama... ila nililo na uhakika nalo mwenyekiti akisema wajumbe hawana utamaduni wa kumpinga. Muda ni jibu zuri utayaona.
 
Thubutu yao...kwani hawapendi kutangulia kwa malaika?
 
Hichi kisa kina chekesha sana
 
hiiiii (in magu voice) kutatokea surprise kubwa sana hadi watu watashangaa,majina yapo mfukoni bado wanabodi ngojeni kidogo vuteni subra mtajionea wenyew tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…