Uchaguzi 2020 Kauli ya Membe leo imedhihirisha kuwa Tundu Lissu hatunaye tena kwenye uchaguzi ujao

Uchaguzi 2020 Kauli ya Membe leo imedhihirisha kuwa Tundu Lissu hatunaye tena kwenye uchaguzi ujao

Obama alipokuja hapa baada ya kustaafu Watanzania wengi walijua ingawa wahusika walitaka iwe siri vivyo hivyo mtu mashughuri huwezi kumficha utafichika wewe ukijaribu. Mtu au watu wakitafuta makosa yoyote ya mtu yeyote kwa nia yoyote watayapata kwa njia mbalimbali. Mh. Lissu alikuwa mashughuri akiwa Mbunge kama Wabunge wengine, kilichompata kilimwongezea umashughuri, kukaa nje ya nchi miaka 3 kuliongeza umaarufu, kufukuzwa Ubunge na kumnyima haki zake kumeongeza mvuto, ujasiri wa kuamua kurudi kwenye pango la Simba na kutaka mnofu toka mdomo wa simba kumemfanya awe kipenzi cha wengi na muda mfupi wa kukamilisha matakwa ya Sheria asingepata wadhamini angekaa tu Singida. Utakuwa mjinga sana ukianza kucheza mchezo wowote kabla ya kipenga na kudai pointi.
Anakatwa tarehe 25/8 na kesho yake watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida na yeye atabaki na kesi zake kisutu
 
Na huku majimboni wagombea tunao waona wakichukua fomu kwa mbwembwe na na mapikipiki na hij tunaihitaje
 
Ni bora wamwache kwa sababu, ataungana na Membe sasa ndio itakuwa hali mbaya zaidi majukwaani
 
Sasa utasemaje ni kufanya kampeni kama hujateuliwa na tume kuwa mgombea?

Kampeni ni kujinadi kwa namna yoyote ile mara utakapokuwa umepitishwa kuwa mgombea wa uchaguzi. Kabla ya hapo ni siasa tu. Na kila mgombea wa urais mwaka huu amezifanya katika mtindo tofauti. Na hilo limekuwa likifanyika toka mwaka 1995.

Fomu ya uchaguzi hauchukuliwi kimya kimya na wadhamini hawatafutwi kimya kimya vile vile.
Mbona jambo lenyewe halina ugumu wa kitendawili cha ‘kuku na yai ni kipi kimetangulia’.

Tatizo labda ni tafsiri yako ya campaign.

Ni hivi: moja ya kitendo cha campaign ni kukusanya watu kwa lengo kuwashiwishi.

Hilo ndio jambo lililozuiwa na NEC kwa watu ambao wamechukua form za kugombea uraisi mpaka watakapoteuliwa na tarehe rasmi ya kufanya hayo ni 26 August.

It’s just common sense.
 
tuliwaambia mgombea ana tatizo la akili hawakuskia, sasa lissu achape lapa mapema tu
 
Anakatwa tarehe 25/8 na kesho yake watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida na yeye atabaki na kesi zake kisutu
Wewe mkate tu kwani atakuwa wa kwanza, wako wapi wasomi wale wakina Chenge, Wasira, Mwakyembe na wapenzi wenu akina Makonda na wengine wengi wa Chama chenu itakuwa huyu wa upinzani? Hata hilo la kukatwa likitokea, ujumbe utakuwa umefika.
 
Mkuu kama umefuatilia mikutano ya lisu HAKUNA alipojinadi wamchague KUWA raisi pia mikutano aliyokua anafanya ilikua anatafuta wadhamini huwezi kudhaminiwa bila kutema cheche kidogo huu mtego hawajategwa CHADEMA bali CCM we subiri uone lisu siyo mjinga hivyo alafu Membe yule yuko kazini hapo nadhani unamwelewa.......
 
Kampeni hata kama zingekuwa zinafanywa muda wote. Haina shida. Maana hata chama tawala kimekuwa kikfanya kampeni muda wote,wenyewe wanaita kuitekeleza ilani.

Labda tupate maana ya kampeni hasa ni nini?
 
Habari wadau,

Kwanza niwapongeze viongozi wote wa vyama vya kisiasa walio Tia Nia ya Kugombea Urais bila kuonyesha dalili zozote za kuchafua nchi

Nanukuu
Rais Magufuli alipoenda kuchukua form Alisema nimekuja peke yangu kwa sababu sitaki kuvunja sheria kwani hairuusiw Mgombea kuongozana na umati wa watu kwenye ofisi za kuchukulia form

Membe Leo kasema kua wametafuta wadhamin Ndani ya mikoa 10 kimia kimia ili kukwepa Mtego. Je, huo Mtego ni upi?

Juzi Tundu Lissu ameanza kutoa vitisho kuwa anasikia wanataka kumkata japo wahusika hawaja taja Jina mtu yeyote wala hawaja ongea habar za kumkata mtu ila wao wamejikita katika misingi ya kuendelea kuwakumbusha wagombea kufata sheria na kusema Atae junja sheria ya uchaguzi Basi wata mshuhulikia

Nacho jiuliza mimi ni haya maneno ya Membe na kwanini Tundu Lissu na chadema wajihisi ni Wao ndio walio Anza kampen kabla ya muda kwanin wajihisi ni wao ndio walio tukana kwann wajihisi ni wao ndio Wata katwa!?

Au wanajua walilo yatenda?
Tatizo ni kwamba kuna baadhi yetu tunachagua nini cha kukubaliana nacho na nini cha kukataa, hata kama kina ukweli ndani yake.
Kama tukichukulia ki mzuka mzuka suala la kuanza kampeni mapema, basi wabunge, mawaziri na hata raisi mwenyewe walishaanza kampeni siku nyingi sana.
Katika kufuatilia kwangu Lissu alilitolea ufafanuzi wa kisheria suala la kuanza kampeni mapema. Alisema kisheria yeye hajakuwa mgombea bado, ila ameteuliwa na chama chake kuwa mgombea. Kisheria unakuwa mgombea baada ya kupitishwa rasmi na tume ya uchaguzi, na tume ikisha kupitisha hapo sasa kisheria ndio unaweza kuingia katika mtego wakuanza kampeni mapema tofauti na terehe iliyo pangwa na tume ya uchaguzi.
Je, membe anaogopa mtego gani katika hilo? Ama hajui sheria? Ama anajua kuna watakao pindisha sheria na yeye asiweze kufanya lolote ili kujitetea kisheria?
 
Walikuwa 200 na magufuli akawapigia simu kwamba amefurahisgwa na nyimbo zinamtukana lissu chadema na wapinzani naamini hajuna sheria ya kumuenguwa Lissu Tume sidhani wanaweze kujishusha hadhi kiasi hicho

Tume haiko huru kwahiyo tutarajia lolote toka kwao na tusije kuwalaumu kwa kufuata maelekezo ya ‘aliye juu’!
 
Back
Top Bottom