Kauli ya Mkuu wa Majeshi kwa Rais ni ONYO, Turejee hii

Nikiri wazi kutoka sakafu ya moyo wangu, nimefurahi sana kilio changu na kampeni yangu ya miaka mingi kuona leo imejibiwa na Mkuu wa Majeshi nchini. Nilionya kuwa nchi yetu tumeingiliwa, tunahujumiwa tena vya kutosha.

Nakumbuka 22 December 2019 niliandika makala hii hapa chini nikitilia mashaka kwamba taifa linahujumiwa na hawa walioko madarakani, walioko katika sekta za maamuzi mazito ya Taifa letu kuanzia ikulu hadi ofisi ya mtaa/kijiji. Naomba nikurejeshe katika makala hiyo kisha linganisha na alichosema Mkuu wa Majeshi.
__________

"Kuna mambo katika nchi yanahitaji uchunguzi kubaini pengine kuna hujuma katika taifa, hii inatokana na michakato mingi muhimu ya kichumi na kijamii imekuwa ikiishia njiani na kuliacha taifa katika hasara kubwa. Hii ni hujuma inahitaji mwarobaini kulitibu.

Mifano ya michakato ambayo kwamiaka mingi imekuwa ikiishia njiani ni kama vile sekta ya nishati ambapo uzalishaji wa umeme limekuwa jambo linalotumiwa kama mchakato wakuzuka na kufa kwa miaka mingi sana tangu mwaka 1994 ilipokuja kitu kinaitwa umeme wa dharula kuokoa taifa (IPTL), ikafata michakato mingi yenye kuumiza taifa na haikufanikiwa hadi tukafika kuchimba Gesi mtwara tukapoteza mabilioni, gesi hadi Kinyerezi, kufumba na kufumbua mradi umetelekezwa sasa tunaimba mradi wa Bonde la Rufiji. Twende tuendelee..

Serikali ya awamu ya nne ilianzisha mradi wa kimkakati kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara duniani, mradi huu ilikuwa ni kujenga bandari ya Bagamoyo kwa ubia kati ya China na Omani wenye thamani ya dola bilioni 10, Serikali ya Tanzania katika mradi huu ilikuwa haiweki pesa yoyote isipokuwa ardhi na raslimali zingine, huku Uchina na Omani wakiweka mtaji na utaalamu.

Kwamjibu wa mapendekezo ya makataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na uwezo wa kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badi ingekusanya gawio toka kwa chombo kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu.

Huu ni moja ya mradi ambo kimsingi ulikuwa umeitangazia dunia vita vya kiuchumi toka kwa washindani wetu ambao ni nchi jirani na zinazotuzunguka. Kwakuwa Afrika yote ingepokelea bidhaa zake toka ulimwenguni hadi Bagamoyo, sawa na ilivyo Dubai ambayo ndio mlango wa Afrika kupokelea bidhaa zake. Afrika inaingiza bidhaa toka Uchina kwa 88.8% na kiwango cha 98% ya bidhaa hizo zinapita Dubai. Hivyo kujengwa kwa Bandari ya Bagamoyo kungefunga nyia ya Dubai na bidhaa zote za Afrika kutoka China kupita Bagamoyo. Hii inamaana kwamba uchumi wa Dubai na Marekani ambayo ndio mdau mkuu ungemegwa. Mradi huu ulikuwa ndio msingi halisi wa kuanzisha mradi wa reli ya kisasa ya SGR, bila Bandari itakayozalisha mizigo kwa wingi SGR itakuwa ni kwakubeba abiria tu badala ya mizigo.

Serikali ya awamu ya tano katika hali ya kustaajabisha iliutupilia mbali mradi huo kwakutoa sababu ambazo hazina nguvu na zingine za kushangaza sana, mimi naitafsiri kama ni hujuma kwa taifa, izingatiwe kuwa tayari taifa lilishaingia gharama kubwa kuanzia kwenye upembuzi yakinifu, na kusaini mikataba ya awali. Kitendo cha kusitisha katika hatua hii ni kulitia hasara taifa.

Ajabu la dunia zaidi, Wale waliokuwa washindani wetu Dubai rasmi baada ya kutangaza mradi wa Bagamoyo, ndio wamekuja kuwekeza katika bandari ya Dar ambayo sisi tuliona ni ndogo kwa aina ya mipango yetu ya kiuchumi na Kimataifa, kuwekeza Bandari ya Dar kwa Dubai lilikuwa tangazo la kuua mradi wa Bagamoyo, hata kama mamlaka zinasema zitaanza mradi huo, ukweli haziwezi kujenga kama ilivyokusudiwa katika mipango ya awali. Na moja ya vipengele kwenye mikataba wa DP World ni kuwa tukitaka kuendeleza mradi wa Bagamoyo kipajmbele apewe yeye akishindwa ndio tutafute mwekezaji mwingine.

Katikati ya mvutano wetu na wabia hadi kusitisha, Rais wa Msumbiji Philip Nyusi kwakutumia majasusi wake waliotanda kila pembe ya Afrika na kwingineko, amefanya mageuzi makubwa, amechukua wazo lilelile ambalo limekataliwa Dar es Salaam na wajuvi, amekwenda kulisimika katika Bandari ya Nacala kwakuingia ubia na Wachina kwa Dola bilioni 5, hii ni Bandari inayotarajiwa kuwa lango kuu la kiuchumi Afrika.

Wakati hili halijapoa, Mwaka 2017 Tanzania tulipowazuia wazungu tuliowauzia wenyewe madinini yetu na kilichomo ndani yake kwamba wasisafirishe madini ghafi na makinikia yao, tuliimba nyimbo kwamba Tanzania itajenga vinu vya kuchenjulia madini hapahapa, na nyimbo ziliimbwa kisiasa zikaitikiwa kishabiki kwa beti za kinafiki kwelikweli. Leo nyimbo haziimbwi, hakuna anayejua kama viwanda vimeshajengwa au laa na hakuna anayehoji hilo, tulishazoe vimbunga kwamba vitavuma na kutulia.

Lakini huku sisi tukiwa tumebadili nyimbo sasa tunaimba nyimbo za Standard Gauge nk, Rwanda kwakutumia majasusi wao waliotanda kila pembe ya Dunia, ilichukua wazo lilelile la Tanzania imejenga vinu vya kuchenjulia madini na inatarajiwa kwamba mwaka huu 2024 Rwanda iwe ndio nchi ya kwanza barani Afrika inayosafirisha madini kwa wingi nje ya Afrika. Kumbuka na elewa Rwanda sio mzalishaji wa Dhabu, Almasi wala chochote kiitwacho madini isipokuwa kwenye kilimo cha chai na kahawa huko. Hivyo anategemea viwanda vyake vipokee madini ghafi toka Tanzania, Kongo, Zambia ikusanye kodi yake na kugonga muhuri wa madini unaotambulisha kuwa ni madini toka Rwanda nk. Sisi tumelala. Siasa inanguvu bana.

Ukitaka kujua kuwa tumeingiliwa katika nchi, Angalia Zanzibar, kwa miaka michache tu aliyoongoza Mwinyi michakato mingi mikubwa ya kiuchumi imefanikiwa na kufika mwisho, Mfano Mwinyi amejenga upya uwanja wa ndege wa hadhi ya Kimataifa, Amejenga uwanja wa mpira wa miguu wa hadhi ya kimataifa, amesaini mikataba ya ujenzi wa bandari ya abiria yenye hadhi ya kimataifa pengine itakuwa ndio bandari nzuri na kubwa barani Afrika. Kama hiyo haitoshi, Mwinyi anajenga bandari ya mizigo, amesaini ujenzi wa reli ya kisasa itakayoanza ujenzi hivi karibuni.

Kwa maoni yangu ninafiki kuna tatizo kubwa kwenye eneo la Ujasusi katika nchi yetu, hasa ujasusi wa Kiuchumi, na hili ndilo lilikuwa msingi wa kuandika Kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Michakato mingi ya kiuchumi katika nchi hii imekuwa haina mafaa ama inaliacha taifa katika makovu makubwa yasiyozibika. Hii inazaa uhalali wa kuhitaji mageuzi makubwa katika Idara ya Ujasusi nchini kuanzia kwenye ideology, sheria, misingi, kanuni, na mambo anuai ndani ya idara ya ujasusi nchini.

Ujasusi kwa nchi zilizoendelea kama China, Israel, Urusi na Marekani, unafanywa na watu ambao ni smart na wanajengwa kuwa smart ili kuweza kumudu ugumu wa kazi hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa. Majasusi katika nchi hizo hawapewi kazi kwasababu ya ujomba ujomba na kujuana.
Ni kweli asilimia kubwa ya information's zenye thamani katika kazi ya ujasusi huwa zinaletwa na "human intelligence" badala ya magazeti, TV na source nyingine za habari.

Kwa maana hiyo basi ni lazima kuwe na watu competent ambao wana uwezo wa kukusanya habari za kijasusi ili tuweze kupata information's za maana na kujenga uwezo wa kuzifanyia kazi informations hizo. Imagine wakati ule wa vita baridi jinsi Directorate 16 ya KGB ilivyoweza kufanya kazi ya kununua sensitive navy information za USA na kuweza kutengeneza balance ya navy fleet bila USA kugundua kwa miaka 17 kupitia kwa Johny Walker junior!

Nitoe rai kwa Mkuu wa Majeshi nchini, aanzishe Oparesheni ya kijasusi ya kulisafisha taifa kuanzia ngazi ya kaya, kijmtongoji, kijiji/mtaa, Kata, Wilaya, Mkoa, Taifa na Ikulu. Jeshi lifanye tathimini ya kina kuona Tanzania kwenye balozi zetu kuna majasusi wa aina gani. Wale wa kujua kuongea kifaransa na kireno na lugha nyingine za mataifa ya nje bila upeo wowote wa Technologia?. Kama kuna sehemu tunakosea zaidi basi ndio hapo kwenye balozi.

Majasusi wengi wa Tanzania au tunaoambiwa kuwa ni watu wa system wengi katika tafsiri ya kijasusi ni "informers". Ujasusi kama ujasusi hapa Tanzania ni kama hakuna. Usalama wa Taifa au TISS/UWT msingi wao uliounda chombo hiki ni "power defensive", yaani wajibu mkubwa unaelekezwa kwenye kumonitor mwelekeo wa kisiasa Tanzania hasa kuwadhibiti oppositions na elements zote za upinzani na assasinations za elements zozote zinazoonekana kuwa against himaya ya CCM. Hili nilitaraji kwenye mabadiliko ya kisheria na kimuundo lingebadilika kwenye marekebisho ya August 2023, Bahati mbaya wanasiasa waliingilia na kuzuia mabadiliko hayo tukabaki kulekule.

Nirudie kusema, Asante sana Mkuu wa Majeshi, Niwatakie Oparesheni njema ya kulijenga upya taifa letu kutuondolea majasusi wa kigeni walioko CCM na Serikalini wanaokwamisha maendeleo ya nchi yetu, Nihimize umakini na uangalifu katika Oparesheni nyingi huko nyuma zimeacha makovu makubwa yasiyofutika, Kwahakika Dunia inatuona, hii ichukue tahadhari zote za kiusalama bila kuumiza wananchi wasio na hatia.

Ok, In case umesahau au ulikuwa hujui, Mshindi wa Tuzo ya Mwandishi Bora wa Vitabu Barani AFRIKA ni YERICKO YOHANESY NYERERE kutoka TANZANIA.

Sifa na heshima ni za Watanzania!

Idumu Mizimu!

View attachment 2879795

View attachment 2879796
View attachment 2879797
Tatizo tulilo nalo kubwa ni CCM tu basi.
 
Naam n kweli yaan hizo taarifa sidiefu amezitoa tatizo wataenda kuzijadili kiupande upande.......

Hao wanyarwanda walivyojaa mpaka wengine wapo humo kwenye majeshi na wanavyojipenyeza kwa mgongo wa rushwa n hatariiii[emoji23][emoji23][emoji23].

Kaka Yericko ukisoma kitabu cha oparesheni moja ya mosadi kuwatoa wayahudi wa ethiopia (red sea spies) unaweza pata mwangaza mapandikizi yanavyoweza kujipenyeza kwenye nchi na kwa kuiakisi tanzania unaweza waona kina bongo zozo,calito n.k sio wa kuaminiwa kizembe zembe.

Idara wanaleta uyuvisisiemu ngoja kitulambe sasa[emoji23][emoji23][emoji23]
Uyo bongo zozo tangu mara ya kwanza namuona mtandaoni na ile interview yake ya fujo zisizoumiza kuna machale yalinicheza akilini kuhusu yule jamaa. Kama kuna kitu kinaniambia jamaa ni spy
 
ungependelea wamaanishe ustawi wa CHADEMA kua upinzani sio, right?[emoji205]
ulitamani arlet ya raisi iwe ni kutoka madarakani sio, right? [emoji205]

so ulitaka waione chadema kama miungu watu sio, right?[emoji205]
Hujaelewa kitu chukua kopo wahi maliwatoni ukatoe janaba msubiri mumeo, hii mada iko juu saaaaana ya ufahamu wako.
 
Yaan, ulichoandika hakika hakieleweki kabisa. Bandari ya Bagamoyo ilizuiliwa,, kujengwa, ina uhusiano gani na watu wa, nje au majasusi. Mwinyi amejenga, viwanja na kuleta, maendeleo Zanzibar ina uhusiano upi na ujasusi ? Haueleweki kabisa unachoandika.
Mbona kaeleza vizuri tena kwa lugha nyepesi kama hujaelewa hapa wewe ni ngumbaru. Ukiona huelewi ujue mada imekuzidi uwezo wa ufahamu.
 
Nikiri wazi kutoka sakafu ya moyo wangu, nimefurahi sana kilio changu na kampeni yangu ya miaka mingi kuona leo imejibiwa na Mkuu wa Majeshi nchini. Nilionya kuwa nchi yetu tumeingiliwa, tunahujumiwa tena vya kutosha.

Nakumbuka 22 December 2019 niliandika makala hii hapa chini nikitilia mashaka kwamba taifa linahujumiwa na hawa walioko madarakani, walioko katika sekta za maamuzi mazito ya Taifa letu kuanzia ikulu hadi ofisi ya mtaa/kijiji. Naomba nikurejeshe katika makala hiyo kisha linganisha na alichosema Mkuu wa Majeshi.
__________

"Kuna mambo katika nchi yanahitaji uchunguzi kubaini pengine kuna hujuma katika taifa, hii inatokana na michakato mingi muhimu ya kichumi na kijamii imekuwa ikiishia njiani na kuliacha taifa katika hasara kubwa. Hii ni hujuma inahitaji mwarobaini kulitibu.

Mifano ya michakato ambayo kwamiaka mingi imekuwa ikiishia njiani ni kama vile sekta ya nishati ambapo uzalishaji wa umeme limekuwa jambo linalotumiwa kama mchakato wakuzuka na kufa kwa miaka mingi sana tangu mwaka 1994 ilipokuja kitu kinaitwa umeme wa dharula kuokoa taifa (IPTL), ikafata michakato mingi yenye kuumiza taifa na haikufanikiwa hadi tukafika kuchimba Gesi mtwara tukapoteza mabilioni, gesi hadi Kinyerezi, kufumba na kufumbua mradi umetelekezwa sasa tunaimba mradi wa Bonde la Rufiji. Twende tuendelee..

Serikali ya awamu ya nne ilianzisha mradi wa kimkakati kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara duniani, mradi huu ilikuwa ni kujenga bandari ya Bagamoyo kwa ubia kati ya China na Omani wenye thamani ya dola bilioni 10, Serikali ya Tanzania katika mradi huu ilikuwa haiweki pesa yoyote isipokuwa ardhi na raslimali zingine, huku Uchina na Omani wakiweka mtaji na utaalamu.

Kwamjibu wa mapendekezo ya makataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na uwezo wa kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badi ingekusanya gawio toka kwa chombo kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu.

Huu ni moja ya mradi ambo kimsingi ulikuwa umeitangazia dunia vita vya kiuchumi toka kwa washindani wetu ambao ni nchi jirani na zinazotuzunguka. Kwakuwa Afrika yote ingepokelea bidhaa zake toka ulimwenguni hadi Bagamoyo, sawa na ilivyo Dubai ambayo ndio mlango wa Afrika kupokelea bidhaa zake. Afrika inaingiza bidhaa toka Uchina kwa 88.8% na kiwango cha 98% ya bidhaa hizo zinapita Dubai. Hivyo kujengwa kwa Bandari ya Bagamoyo kungefunga nyia ya Dubai na bidhaa zote za Afrika kutoka China kupita Bagamoyo. Hii inamaana kwamba uchumi wa Dubai na Marekani ambayo ndio mdau mkuu ungemegwa. Mradi huu ulikuwa ndio msingi halisi wa kuanzisha mradi wa reli ya kisasa ya SGR, bila Bandari itakayozalisha mizigo kwa wingi SGR itakuwa ni kwakubeba abiria tu badala ya mizigo.

Serikali ya awamu ya tano katika hali ya kustaajabisha iliutupilia mbali mradi huo kwakutoa sababu ambazo hazina nguvu na zingine za kushangaza sana, mimi naitafsiri kama ni hujuma kwa taifa, izingatiwe kuwa tayari taifa lilishaingia gharama kubwa kuanzia kwenye upembuzi yakinifu, na kusaini mikataba ya awali. Kitendo cha kusitisha katika hatua hii ni kulitia hasara taifa.

Ajabu la dunia zaidi, Wale waliokuwa washindani wetu Dubai rasmi baada ya kutangaza mradi wa Bagamoyo, ndio wamekuja kuwekeza katika bandari ya Dar ambayo sisi tuliona ni ndogo kwa aina ya mipango yetu ya kiuchumi na Kimataifa, kuwekeza Bandari ya Dar kwa Dubai lilikuwa tangazo la kuua mradi wa Bagamoyo, hata kama mamlaka zinasema zitaanza mradi huo, ukweli haziwezi kujenga kama ilivyokusudiwa katika mipango ya awali. Na moja ya vipengele kwenye mikataba wa DP World ni kuwa tukitaka kuendeleza mradi wa Bagamoyo kipajmbele apewe yeye akishindwa ndio tutafute mwekezaji mwingine.

Katikati ya mvutano wetu na wabia hadi kusitisha, Rais wa Msumbiji Philip Nyusi kwakutumia majasusi wake waliotanda kila pembe ya Afrika na kwingineko, amefanya mageuzi makubwa, amechukua wazo lilelile ambalo limekataliwa Dar es Salaam na wajuvi, amekwenda kulisimika katika Bandari ya Nacala kwakuingia ubia na Wachina kwa Dola bilioni 5, hii ni Bandari inayotarajiwa kuwa lango kuu la kiuchumi Afrika.

Wakati hili halijapoa, Mwaka 2017 Tanzania tulipowazuia wazungu tuliowauzia wenyewe madinini yetu na kilichomo ndani yake kwamba wasisafirishe madini ghafi na makinikia yao, tuliimba nyimbo kwamba Tanzania itajenga vinu vya kuchenjulia madini hapahapa, na nyimbo ziliimbwa kisiasa zikaitikiwa kishabiki kwa beti za kinafiki kwelikweli. Leo nyimbo haziimbwi, hakuna anayejua kama viwanda vimeshajengwa au laa na hakuna anayehoji hilo, tulishazoe vimbunga kwamba vitavuma na kutulia.

Lakini huku sisi tukiwa tumebadili nyimbo sasa tunaimba nyimbo za Standard Gauge nk, Rwanda kwakutumia majasusi wao waliotanda kila pembe ya Dunia, ilichukua wazo lilelile la Tanzania imejenga vinu vya kuchenjulia madini na inatarajiwa kwamba mwaka huu 2024 Rwanda iwe ndio nchi ya kwanza barani Afrika inayosafirisha madini kwa wingi nje ya Afrika. Kumbuka na elewa Rwanda sio mzalishaji wa Dhabu, Almasi wala chochote kiitwacho madini isipokuwa kwenye kilimo cha chai na kahawa huko. Hivyo anategemea viwanda vyake vipokee madini ghafi toka Tanzania, Kongo, Zambia ikusanye kodi yake na kugonga muhuri wa madini unaotambulisha kuwa ni madini toka Rwanda nk. Sisi tumelala. Siasa inanguvu bana.

Ukitaka kujua kuwa tumeingiliwa katika nchi, Angalia Zanzibar, kwa miaka michache tu aliyoongoza Mwinyi michakato mingi mikubwa ya kiuchumi imefanikiwa na kufika mwisho, Mfano Mwinyi amejenga upya uwanja wa ndege wa hadhi ya Kimataifa, Amejenga uwanja wa mpira wa miguu wa hadhi ya kimataifa, amesaini mikataba ya ujenzi wa bandari ya abiria yenye hadhi ya kimataifa pengine itakuwa ndio bandari nzuri na kubwa barani Afrika. Kama hiyo haitoshi, Mwinyi anajenga bandari ya mizigo, amesaini ujenzi wa reli ya kisasa itakayoanza ujenzi hivi karibuni.

Kwa maoni yangu ninafiki kuna tatizo kubwa kwenye eneo la Ujasusi katika nchi yetu, hasa ujasusi wa Kiuchumi, na hili ndilo lilikuwa msingi wa kuandika Kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Michakato mingi ya kiuchumi katika nchi hii imekuwa haina mafaa ama inaliacha taifa katika makovu makubwa yasiyozibika. Hii inazaa uhalali wa kuhitaji mageuzi makubwa katika Idara ya Ujasusi nchini kuanzia kwenye ideology, sheria, misingi, kanuni, na mambo anuai ndani ya idara ya ujasusi nchini.

Ujasusi kwa nchi zilizoendelea kama China, Israel, Urusi na Marekani, unafanywa na watu ambao ni smart na wanajengwa kuwa smart ili kuweza kumudu ugumu wa kazi hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa. Majasusi katika nchi hizo hawapewi kazi kwasababu ya ujomba ujomba na kujuana.
Ni kweli asilimia kubwa ya information's zenye thamani katika kazi ya ujasusi huwa zinaletwa na "human intelligence" badala ya magazeti, TV na source nyingine za habari.

Kwa maana hiyo basi ni lazima kuwe na watu competent ambao wana uwezo wa kukusanya habari za kijasusi ili tuweze kupata information's za maana na kujenga uwezo wa kuzifanyia kazi informations hizo. Imagine wakati ule wa vita baridi jinsi Directorate 16 ya KGB ilivyoweza kufanya kazi ya kununua sensitive navy information za USA na kuweza kutengeneza balance ya navy fleet bila USA kugundua kwa miaka 17 kupitia kwa Johny Walker junior!

Nitoe rai kwa Mkuu wa Majeshi nchini, aanzishe Oparesheni ya kijasusi ya kulisafisha taifa kuanzia ngazi ya kaya, kijmtongoji, kijiji/mtaa, Kata, Wilaya, Mkoa, Taifa na Ikulu. Jeshi lifanye tathimini ya kina kuona Tanzania kwenye balozi zetu kuna majasusi wa aina gani. Wale wa kujua kuongea kifaransa na kireno na lugha nyingine za mataifa ya nje bila upeo wowote wa Technologia?. Kama kuna sehemu tunakosea zaidi basi ndio hapo kwenye balozi.

Majasusi wengi wa Tanzania au tunaoambiwa kuwa ni watu wa system wengi katika tafsiri ya kijasusi ni "informers". Ujasusi kama ujasusi hapa Tanzania ni kama hakuna. Usalama wa Taifa au TISS/UWT msingi wao uliounda chombo hiki ni "power defensive", yaani wajibu mkubwa unaelekezwa kwenye kumonitor mwelekeo wa kisiasa Tanzania hasa kuwadhibiti oppositions na elements zote za upinzani na assasinations za elements zozote zinazoonekana kuwa against himaya ya CCM. Hili nilitaraji kwenye mabadiliko ya kisheria na kimuundo lingebadilika kwenye marekebisho ya August 2023, Bahati mbaya wanasiasa waliingilia na kuzuia mabadiliko hayo tukabaki kulekule.

Nirudie kusema, Asante sana Mkuu wa Majeshi, Niwatakie Oparesheni njema ya kulijenga upya taifa letu kutuondolea majasusi wa kigeni walioko CCM na Serikalini wanaokwamisha maendeleo ya nchi yetu, Nihimize umakini na uangalifu katika Oparesheni nyingi huko nyuma zimeacha makovu makubwa yasiyofutika, Kwahakika Dunia inatuona, hii ichukue tahadhari zote za kiusalama bila kuumiza wananchi wasio na hatia.

Ok, In case umesahau au ulikuwa hujui, Mshindi wa Tuzo ya Mwandishi Bora wa Vitabu Barani AFRIKA ni YERICKO YOHANESY NYERERE kutoka TANZANIA.

Sifa na heshima ni za Watanzania!

Idumu Mizimu!

View attachment 2879795

View attachment 2879796
View attachment 2879797
Tuanze na Mama. Yeye mwenyewe na baadhi ya washauri wake si Watanzania
 
Kwenye umeme pia nilishawahi kuandika hapa kuwa tunahujumiwa tena na mataifa makubwa tu.

Hawataki kabisa tuwe na nishati ya kueleweka.

Bandari ya bagamoyo ingeua nchi na kuifutilia mbali kama angepewa mchina
Mnahujumiwa na nani?.wewe sema uwezo wakuongoza nakusimamia wa chama cha mapinduzi umefika kikomo.
 
Sijaelewa inawezekanaje usalama wa Taifa upo na mamluki wanapata nafasi kiasi hicho. Kwamba hao wageni ni smat kuliko watz? Wanarumia ushawishi gani kupata hizo nafasi?
 
Usalama hii iliyojaza vijana wa ovyo toka uvccm, wanachoweza ni kuratibu wizi wa kura tu
 
Naanza kuwa na wasiwasi hata na Hawa nyelele,mkapa,mwinyi,kikwete,magufuri,samia,
Huenda si watanzania ina weza kuwa nimbegu za nje zilizo kuwa zimeanda liwa kwa Siri saana miaka mingi nyuma

Na Nina Imani hata wanao kuja wameandaliwa tayari uchaguzi ni fix tu kwani ukiwa chunguza vizuri utagundua hakili zao woote Zina fanana

Nina wasiwasi pia chadema/mbowe ni ccm na vyama vingine vyote vya upinzani nimatawi ya ccm Tanzania hakuna upinzani bado

Ujasusi ni kitu kipana Sana mkuu 🙏🙏
 
Yaan, ulichoandika hakika hakieleweki kabisa. Bandari ya Bagamoyo ilizuiliwa,, kujengwa, ina uhusiano gani na watu wa, nje au majasusi. Mwinyi amejenga, viwanja na kuleta, maendeleo Zanzibar ina uhusiano upi na ujasusi ? Haueleweki kabisa unachoandika.
Uimara au uduni wa taifa una uhusiano gani na uchumi? Watu wa nje? Bandari na miundombinu mingine? Siasa za ndani? Maamuzi serikalini?
Kwa ujumla wake, usalama wa taifa lenyewe?
Think out of the box.
 
Mpaka CDF kuamua kusema haya hadharani hali ni mbaya sana. Kwa utawala huu wa CCM nchi iko uchi kabisa dunia inatuchora sana. Wao kipaumbele chao ni kuendelea kutawala tu bila kujali mustakabali wa nchi.

Wakizungumzia usalama wa nchi wanamaanisha ustawi wa CCM madarakani. Hata ukisikiliza alert ya Rais kwa JW inalenga wao kuendelea kuwa madarakani na kuwaona Chadema kama adui wa nchi kiasi cha kuomba msaada wa JW kuwashughulikia Chadema.
Inasikitisha sana kwa kweli. Mi nikiwa kama Mtanzania inaniumiza kuona zaidi ya miaka 62 sasa toka uhuru kama nchi haina cha kujivunia. Miaka 62 sasa nchi haina umeme wa uhakika, wananchi wake hawana uhakika wa matibabu huku gharama za maisha zinazidi kupaa.
 
Watawala muda wote wanawaza uchaguzi ujao wataiba vipi kura ili waendelee kutawala.
 
Back
Top Bottom