Kauli ya Mkuu wa Majeshi kwa Rais ni ONYO, Turejee hii

Kauli ya Mkuu wa Majeshi kwa Rais ni ONYO, Turejee hii

"Kwamjibu wa mapendekezo ya makataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na uwezo wa kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badi ingekusanya gawio toka kwa chombo kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu" Hivi ni kwanini tukusanye gawio badala ya kodi yote kwa ujumla?kwanini tugawane mapato na watu wengine badala zote kua zetu?
Tunagawana kwa sababu sisi walioweka mtaji wa uwekezaji ni wengine. Hivyo, tungepaswa kugawana faida hadi pale gharama zao za uwekezaji zitakaporudi na kupata faida kwa kadiri tutakavyokuwa tumekubaliana.
 
Tunapojadili mambo ya maana jitahidi kuficha upumbavu wako ndugu
Ni aina ya watanzania waliokua moulded na ccm na madhara yake ni kutokuona sensitive issues zinazolikabili taifa na namna ya kukabiliana nazo wanaonesha upumbavu wao hadharani na kupoteza mada ya msingi na yenye maana. Huuu ndio mtaji wa watawala na hao aliosemq sidiefu katika kulihujumu taifa kwa kufanya maamuzi tata yanayoligharimu taifa! Hawaoni hata hizo kesi za kimataifa tunazodaiwa kama ni hasara kwa taifa? Mark my word ipo siku hata dp watatudai.
 
Wa bongo mmefsnywa maskini, mpaka hamfurukuti! Manaona njia pekee ya kutoka kimaisha ni kujiunga na *chama", huyo binti, aliyeenda CCM, anajiunga na kundi kubwa LA vijana wenye njaa,aliondoka Kafurila, Nassari! Leo hii wapo wapi, "they are just the shells of their original self" Wamepewa, vijinafasi uchwara wasife njaa, CCM itawatumia tu, wakiisha utamu kama big j, watatupwa kule!
Ha kuna Jimbo wanaweza kupita kwa tiketi ya CCM, maana hata huko CCM wapo wenye njaa wengi tu,
Mtu alikuwa mbunge, miaka mitano,akalipwa milioni 250! Sasa hv ana njaa! Anataka aingie bungeni kuendelea"kuwasemea"wana Nchi!
Umalaya upo wa aina nyingi
Huyu atapewa nafasi ya utendaji serikalini, hiyo ni ajira ya kudumu
 
Nikiri wazi kutoka sakafu ya moyo wangu, nimefurahi sana kilio changu na kampeni yangu ya miaka mingi kuona leo imejibiwa na Mkuu wa Majeshi nchini. Nilionya kuwa nchi yetu tumeingiliwa, tunahujumiwa tena vya kutosha.

Nakumbuka 22 December 2019 niliandika makala hii hapa chini nikitilia mashaka kwamba taifa linahujumiwa na hawa walioko madarakani, walioko katika sekta za maamuzi mazito ya Taifa letu kuanzia ikulu hadi ofisi ya mtaa/kijiji. Naomba nikurejeshe katika makala hiyo kisha linganisha na alichosema Mkuu wa Majeshi.
__________

"Kuna mambo katika nchi yanahitaji uchunguzi kubaini pengine kuna hujuma katika taifa, hii inatokana na michakato mingi muhimu ya kichumi na kijamii imekuwa ikiishia njiani na kuliacha taifa katika hasara kubwa. Hii ni hujuma inahitaji mwarobaini kulitibu.

Mifano ya michakato ambayo kwamiaka mingi imekuwa ikiishia njiani ni kama vile sekta ya nishati ambapo uzalishaji wa umeme limekuwa jambo linalotumiwa kama mchakato wakuzuka na kufa kwa miaka mingi sana tangu mwaka 1994 ilipokuja kitu kinaitwa umeme wa dharula kuokoa taifa (IPTL), ikafata michakato mingi yenye kuumiza taifa na haikufanikiwa hadi tukafika kuchimba Gesi mtwara tukapoteza mabilioni, gesi hadi Kinyerezi, kufumba na kufumbua mradi umetelekezwa sasa tunaimba mradi wa Bonde la Rufiji. Twende tuendelee..

Serikali ya awamu ya nne ilianzisha mradi wa kimkakati kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara duniani, mradi huu ilikuwa ni kujenga bandari ya Bagamoyo kwa ubia kati ya China na Omani wenye thamani ya dola bilioni 10, Serikali ya Tanzania katika mradi huu ilikuwa haiweki pesa yoyote isipokuwa ardhi na raslimali zingine, huku Uchina na Omani wakiweka mtaji na utaalamu.

Kwamjibu wa mapendekezo ya makataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na uwezo wa kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badi ingekusanya gawio toka kwa chombo kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu.

Huu ni moja ya mradi ambo kimsingi ulikuwa umeitangazia dunia vita vya kiuchumi toka kwa washindani wetu ambao ni nchi jirani na zinazotuzunguka. Kwakuwa Afrika yote ingepokelea bidhaa zake toka ulimwenguni hadi Bagamoyo, sawa na ilivyo Dubai ambayo ndio mlango wa Afrika kupokelea bidhaa zake. Afrika inaingiza bidhaa toka Uchina kwa 88.8% na kiwango cha 98% ya bidhaa hizo zinapita Dubai. Hivyo kujengwa kwa Bandari ya Bagamoyo kungefunga nyia ya Dubai na bidhaa zote za Afrika kutoka China kupita Bagamoyo. Hii inamaana kwamba uchumi wa Dubai na Marekani ambayo ndio mdau mkuu ungemegwa. Mradi huu ulikuwa ndio msingi halisi wa kuanzisha mradi wa reli ya kisasa ya SGR, bila Bandari itakayozalisha mizigo kwa wingi SGR itakuwa ni kwakubeba abiria tu badala ya mizigo.

Serikali ya awamu ya tano katika hali ya kustaajabisha iliutupilia mbali mradi huo kwakutoa sababu ambazo hazina nguvu na zingine za kushangaza sana, mimi naitafsiri kama ni hujuma kwa taifa, izingatiwe kuwa tayari taifa lilishaingia gharama kubwa kuanzia kwenye upembuzi yakinifu, na kusaini mikataba ya awali. Kitendo cha kusitisha katika hatua hii ni kulitia hasara taifa.

Ajabu la dunia zaidi, Wale waliokuwa washindani wetu Dubai rasmi baada ya kutangaza mradi wa Bagamoyo, ndio wamekuja kuwekeza katika bandari ya Dar ambayo sisi tuliona ni ndogo kwa aina ya mipango yetu ya kiuchumi na Kimataifa, kuwekeza Bandari ya Dar kwa Dubai lilikuwa tangazo la kuua mradi wa Bagamoyo, hata kama mamlaka zinasema zitaanza mradi huo, ukweli haziwezi kujenga kama ilivyokusudiwa katika mipango ya awali. Na moja ya vipengele kwenye mikataba wa DP World ni kuwa tukitaka kuendeleza mradi wa Bagamoyo kipajmbele apewe yeye akishindwa ndio tutafute mwekezaji mwingine.

Katikati ya mvutano wetu na wabia hadi kusitisha, Rais wa Msumbiji Philip Nyusi kwakutumia majasusi wake waliotanda kila pembe ya Afrika na kwingineko, amefanya mageuzi makubwa, amechukua wazo lilelile ambalo limekataliwa Dar es Salaam na wajuvi, amekwenda kulisimika katika Bandari ya Nacala kwakuingia ubia na Wachina kwa Dola bilioni 5, hii ni Bandari inayotarajiwa kuwa lango kuu la kiuchumi Afrika.

Wakati hili halijapoa, Mwaka 2017 Tanzania tulipowazuia wazungu tuliowauzia wenyewe madinini yetu na kilichomo ndani yake kwamba wasisafirishe madini ghafi na makinikia yao, tuliimba nyimbo kwamba Tanzania itajenga vinu vya kuchenjulia madini hapahapa, na nyimbo ziliimbwa kisiasa zikaitikiwa kishabiki kwa beti za kinafiki kwelikweli. Leo nyimbo haziimbwi, hakuna anayejua kama viwanda vimeshajengwa au laa na hakuna anayehoji hilo, tulishazoe vimbunga kwamba vitavuma na kutulia.

Lakini huku sisi tukiwa tumebadili nyimbo sasa tunaimba nyimbo za Standard Gauge nk, Rwanda kwakutumia majasusi wao waliotanda kila pembe ya Dunia, ilichukua wazo lilelile la Tanzania imejenga vinu vya kuchenjulia madini na inatarajiwa kwamba mwaka huu 2024 Rwanda iwe ndio nchi ya kwanza barani Afrika inayosafirisha madini kwa wingi nje ya Afrika. Kumbuka na elewa Rwanda sio mzalishaji wa Dhabu, Almasi wala chochote kiitwacho madini isipokuwa kwenye kilimo cha chai na kahawa huko. Hivyo anategemea viwanda vyake vipokee madini ghafi toka Tanzania, Kongo, Zambia ikusanye kodi yake na kugonga muhuri wa madini unaotambulisha kuwa ni madini toka Rwanda nk. Sisi tumelala. Siasa inanguvu bana.

Ukitaka kujua kuwa tumeingiliwa katika nchi, Angalia Zanzibar, kwa miaka michache tu aliyoongoza Mwinyi michakato mingi mikubwa ya kiuchumi imefanikiwa na kufika mwisho, Mfano Mwinyi amejenga upya uwanja wa ndege wa hadhi ya Kimataifa, Amejenga uwanja wa mpira wa miguu wa hadhi ya kimataifa, amesaini mikataba ya ujenzi wa bandari ya abiria yenye hadhi ya kimataifa pengine itakuwa ndio bandari nzuri na kubwa barani Afrika. Kama hiyo haitoshi, Mwinyi anajenga bandari ya mizigo, amesaini ujenzi wa reli ya kisasa itakayoanza ujenzi hivi karibuni.

Kwa maoni yangu ninafiki kuna tatizo kubwa kwenye eneo la Ujasusi katika nchi yetu, hasa ujasusi wa Kiuchumi, na hili ndilo lilikuwa msingi wa kuandika Kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Michakato mingi ya kiuchumi katika nchi hii imekuwa haina mafaa ama inaliacha taifa katika makovu makubwa yasiyozibika. Hii inazaa uhalali wa kuhitaji mageuzi makubwa katika Idara ya Ujasusi nchini kuanzia kwenye ideology, sheria, misingi, kanuni, na mambo anuai ndani ya idara ya ujasusi nchini.

Ujasusi kwa nchi zilizoendelea kama China, Israel, Urusi na Marekani, unafanywa na watu ambao ni smart na wanajengwa kuwa smart ili kuweza kumudu ugumu wa kazi hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa. Majasusi katika nchi hizo hawapewi kazi kwasababu ya ujomba ujomba na kujuana.
Ni kweli asilimia kubwa ya information's zenye thamani katika kazi ya ujasusi huwa zinaletwa na "human intelligence" badala ya magazeti, TV na source nyingine za habari.

Kwa maana hiyo basi ni lazima kuwe na watu competent ambao wana uwezo wa kukusanya habari za kijasusi ili tuweze kupata information's za maana na kujenga uwezo wa kuzifanyia kazi informations hizo. Imagine wakati ule wa vita baridi jinsi Directorate 16 ya KGB ilivyoweza kufanya kazi ya kununua sensitive navy information za USA na kuweza kutengeneza balance ya navy fleet bila USA kugundua kwa miaka 17 kupitia kwa Johny Walker junior!

Nitoe rai kwa Mkuu wa Majeshi nchini, aanzishe Oparesheni ya kijasusi ya kulisafisha taifa kuanzia ngazi ya kaya, kijmtongoji, kijiji/mtaa, Kata, Wilaya, Mkoa, Taifa na Ikulu. Jeshi lifanye tathimini ya kina kuona Tanzania kwenye balozi zetu kuna majasusi wa aina gani. Wale wa kujua kuongea kifaransa na kireno na lugha nyingine za mataifa ya nje bila upeo wowote wa Technologia?. Kama kuna sehemu tunakosea zaidi basi ndio hapo kwenye balozi.

Majasusi wengi wa Tanzania au tunaoambiwa kuwa ni watu wa system wengi katika tafsiri ya kijasusi ni "informers". Ujasusi kama ujasusi hapa Tanzania ni kama hakuna. Usalama wa Taifa au TISS/UWT msingi wao uliounda chombo hiki ni "power defensive", yaani wajibu mkubwa unaelekezwa kwenye kumonitor mwelekeo wa kisiasa Tanzania hasa kuwadhibiti oppositions na elements zote za upinzani na assasinations za elements zozote zinazoonekana kuwa against himaya ya CCM. Hili nilitaraji kwenye mabadiliko ya kisheria na kimuundo lingebadilika kwenye marekebisho ya August 2023, Bahati mbaya wanasiasa waliingilia na kuzuia mabadiliko hayo tukabaki kulekule.

Nirudie kusema, Asante sana Mkuu wa Majeshi, Niwatakie Oparesheni njema ya kulijenga upya taifa letu kutuondolea majasusi wa kigeni walioko CCM na Serikalini wanaokwamisha maendeleo ya nchi yetu, Nihimize umakini na uangalifu katika Oparesheni nyingi huko nyuma zimeacha makovu makubwa yasiyofutika, Kwahakika Dunia inatuona, hii ichukue tahadhari zote za kiusalama bila kuumiza wananchi wasio na hatia.

Ok, In case umesahau au ulikuwa hujui, Mshindi wa Tuzo ya Mwandishi Bora wa Vitabu Barani AFRIKA ni YERICKO YOHANESY NYERERE kutoka TANZANIA.

Sifa na heshima ni za Watanzania!

Idumu Mizimu!

View attachment 2879795

View attachment 2879796
View attachment 2879797
Hadi hasara inanitafuna sijui nijimalize???
Mhenga miye nilikuwepo RPF ilipochukua Nchi Rwanda.
  • Maafisa wa ngazi za juu waliosomeshwa na Tanzania na kujitanabaisha kuwa ni Watanzania wengi wakijiita wanyambo, waha na wahaya walinistua kupita kiasi.
  • Nilikuwa na marafiki katika idara nyeti za usalama na wengine jeshini.
Jeshini nilikuwa na rafiki yangu Luteni wa jeshi mtaalamu injinia wa vifaru.
- Serikalini nilikuwa na wataalam wakuwa wa Kilimo, Maji na ujenzi.
Katika mkoa mmoja Basi kubwa la abiria 60 lilikodishwa likaelekea Rwanda na wale niliowazoea kuwa watanzania.
  • Yule Mwanajeshi nilimtembelea Rwanda akiwa mkuu wa Kikosi cha mizinga wa Rwanda.
  • Yule wa Kilimo nilimkuta amekabidhiwa mradi mkubwa wa wizara ya kilimo huko Rwanda. Kwa vile alikuwa rafiki yangu nilikuta amebadilisha jina la ubini na kujiita majina ya kule Rwanda.

KIfupi damage iliyofanyika na inaendelea kufanyika ni kubwa kupita kiasi. Nilipouona mkataba wa DP world nilichanganyikiwa hadi leo.
General Mkunda tafadhali pindua hii nchi haraka ili ipone!
 
Hi Tundu lissu ni Mtanzania kweli ??

Jina lake tuu sio la kizalendo
Hili suala la CDF liangaliwe kwa mapana, kuna tetesi kwamba hata John Heche ni raia wa Kenya, alikuja Tanzania akiwa mkubwa tu.
IMG-20240119-WA0012.jpg
 
Yupo kwenye ngazi ipi ya maamuzi aliyoteuliwa na serikali?
Sio lazima awe serikalini, hata maandamano anayopanga, yanaathiri taifa kimaamuzi, na chama anachofanyia kibarua chake, kimesajiliwa na serikali, kwa hiyo na yeye ni mtumishi wa umma in a way
 
Inavyoonekana ni kwamba Yeriko ni Jasusi mbombezi(au mzoa taarifa tu: Informer)au ana vyanzo vyake vingi vya kiintelijensia kutoka kwa majasusi.

Swali, kwanini ana mumunya mumunya badala ya kutuambia tu ni wapi specifically, tumeingiliwa?

Ni nani huyo anayemufanya CDF kukosa usingizi?
Close information na open information unapokuw unadili na taarfa

Inawez kuw nataarfa sahihi ila zikazua taharuk
 
Viongozi wa kamati kuu ya chadema wamelia sana baada ya kupata taarifa za Upendo Peneza kujiunga na CCM. Mmoja ya kiongozi hao, Freeman Mbowe alisikia akitoa kilio cha kwikwi.

Tusisahau James Mbowe sio raia wa Tanzania lakini Chadema wanampa vyeo ndani ya chama chao.

Lissu, familia yake wote sio raia
Walichagua uraia wa Taifa gani
 
Sisi Kwa level ya viongozi wa nchi hatuko serious vyombo vyetu vyote vimeelekezwa kuthibiti wazalendo
Kudhibiti Wazalendo !
I wish i could not believe it !
Kama itakuwa ni hivyo je hiyo itakuwa ni kwa faida ya nani ??!!
 
Kuna ka uteja flani kapo mahali fulani nyeti sana, kwa hiyo arosto ikipanda wanadungwa kasindano fulani, kisha wateja wanakua watiifu kwa kusahau pakusimamia. Enewei kama sijaeleweka, minnimeelewa.
Duh 🙄 !
 
Sio lazima awe serikalini, hata maandamano anayopanga, yanaathiri taifa kimaamuzi, na chama anachofanyia kibarua chake, kimesajiliwa na serikali, kwa hiyo na yeye ni mtumishi wa umma in a way
Uwezo wako wa akili ni mdogo au umeamua kuchagua upande wa akili ndogo! Hebu rejea kauli ya cdf "wako serikalini na wameteuliwa katika ngazi za maamuzi"

By the way nimefuatilia comments zako nyingi wewe ni mpumbavu ashakum sio matusi kwani upumbavu ni kipaji kama ufupi na urefu according to Mwalimu Nyerrer
Biblia inasema umjibu mpumbavu sawa sawa na upumbavu wake asije akaerevuka. Adios
 
Uwezo wako wa akili ni mdogo au umeamua kuchagua upande wa akili ndogo! Hebu rejea kauli ya cdf "wako serikalini na wameteuliwa katika ngazi za maamuzi"

By the way nimefuatilia comments zako nyingi wewe ni mpumbavu ashakum sio matusi kwani upumbavu ni kipaji kama ufupi na urefu according to Mwalimu Nyerrer
Biblia inasema umjibu mpumbavu sawa sawa na upumbavu wake asije akaerevuka. Adios
Bahati mbaya huna akili,ufupi na urefu ni kipaji ?au ni maumbile? Jinga sana
 
Watoto wa Mbowe na Lissu ni raia wa Marekani na Uingereza
Therefore? Waziri mkuu wa uingereza unajua alizaliwa wapi ? TANZANIA-
BARAKA OBAMA ASILI YAKE KENYA (Luo)
Mtoto wa George Weah ni footballer wa US
Kule state kuna Mayor mwenye asili ya Somalia.
Rejea kauli ya cdf na utumie ubongo kufikiri kimantiki ndipo uongee. James Mbowe ameteuliwa serikalini katika ngazi ipi ya maamuzi? Kwanini mnakimbia vivuli? Tujadili threat iliyopo mbele yetu kwamba kuna refugees na immigrants wanaohujumu nchi yetu! We unazungumzia watu wenye uraia wa nchi nyumngine ambao walifaa kulalamikiwa huko waliko
 
Tatizo kuu ni pale vyombo vya usalama vinapowaza chaguzi zijazo na hatma ya CCM madarakani,hii imewa brainwash hadi maafisa usalama wanawaza ccm kuliko kuwaza hatma ya Taifa letu na ustawi wake!!

KOSA KUBWA SANA ALILOFANYA NYERERE NI KUWAAMINISHA WATz KWAMBA TANZANIA HAIWEZI SONGA MBELE BILA CCM KANA KWAMBA NCHI YA TANZANIA IKIONGOZWA NA VYAMA VINGINE ITABADILIKA JINA,Huo ndio mtego na zigo la misumari ambalo taifa limebebeshwa!!

Kama taifa tungekua na desturi ya vyama kupokezana vijiti nadhani tungejikita kwenye utaifa na sio uvyama Na ufia itikadi Kila chama kingejitahidi kiutendaji Ili kuweka historian ya kimaendeleo katika taifa!!!

Ujasusi uliojikita kuhakikisha chama kinashika dola ni ujasusi wa kijinga ambao binafsi najuta Saba kuzaliwa kwenye taifa ambalo wanalinda chama badala ya ustawi wa wananchi !!!


Lawama zangu zooooote ziende Kwa vyombo vya Dola kuanzia TISS,jwtz,polisi na vyombo vyoote!!

Hatuwezi endelea Kwa kulinda chama hata siku moja!!

Mimi ni mwanaccm ninaeamini ccm imeharibiwa na Dola kwa kulindwa,kuhakikishiwa kushika Dola na kulea ufisadi na uchama,dola ndio adui was CCM kama CCM ingekosa Dola hata kwa miaka kumi tungekua na ccm imara kuliko hii ya uchawa!!!
 
Hadi hasara inanitafuna sijui nijimalize???
Mhenga miye nilikuwepo RPF ilipochukua Nchi Rwanda.
  • Maafisa wa ngazi za juu waliosomeshwa na Tanzania na kujitanabaisha kuwa ni Watanzania wengi wakijiita wanyambo, waha na wahaya walinistua kupita kiasi.
  • Nilikuwa na marafiki katika idara nyeti za usalama na wengine jeshini.
Jeshini nilikuwa na rafiki yangu Luteni wa jeshi mtaalamu injinia wa vifaru.
- Serikalini nilikuwa na wataalam wakuwa wa Kilimo, Maji na ujenzi.
Katika mkoa mmoja Basi kubwa la abiria 60 lilikodishwa likaelekea Rwanda na wale niliowazoea kuwa watanzania.
  • Yule Mwanajeshi nilimtembelea Rwanda akiwa mkuu wa Kikosi cha mizinga wa Rwanda.
  • Yule wa Kilimo nilimkuta amekabidhiwa mradi mkubwa wa wizara ya kilimo huko Rwanda. Kwa vile alikuwa rafiki yangu nilikuta amebadilisha jina la ubini na kujiita majina ya kule Rwanda.

KIfupi damage iliyofanyika na inaendelea kufanyika ni kubwa kupita kiasi. Nilipouona mkataba wa DP world nilichanganyikiwa hadi leo.
General Mkunda tafadhali pindua hii nchi haraka ili ipone!
Daaah
 
Hawa aliwawakilisha wanawake na Samia anawawakilisha wanawake wote maana wote ni wanawake. Dunia ya wakubwa hawaamini katika kuongezea na wanawake anzia Washington hadi Piong yang
 
Back
Top Bottom