Kauli ya Mkuu wa Majeshi kwa Rais ni ONYO, Turejee hii

"Kwamjibu wa mapendekezo ya makataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na uwezo wa kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badi ingekusanya gawio toka kwa chombo kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu" Hivi ni kwanini tukusanye gawio badala ya kodi yote kwa ujumla?kwanini tugawane mapato na watu wengine badala zote kua zetu?
Wewe hujatoa pesa ya ujenzi hata kidogo zaidi ya ardhi unategemea nini? . Kama ni hivyo jenga mwenyewe.
 
Viongozi wa kamati kuu ya chadema wamelia sana baada ya kupata taarifa za Upendo Peneza kujiunga na CCM. Mmoja ya kiongozi hao, Freeman Mbowe alisikia akitoa kilio cha kwikwi.

Tusisahau James Mbowe sio raia wa Tanzania lakini Chadema wanampa vyeo ndani ya chama chao.

Lissu, familia yake wote sio raia
Mkuu hapa hawashindanish upumbavu yan kwakuwa ccm wamewapa vyeo watu wasio kuwa raia na wewe kusema kuwa lisu sijui james sio raia unakuwa umelevel scores mkuu hii sio match ya mpira wa miguu, jaribu basi kutumia ubongo hata kidogo master, hatushindani kujua nan mpumbavu zaidi, aliesema hayo ni CDF tena mbele ya Samia na hatukumuona Rais akisema mbona james sio raia, ficha basi ujinga wa ccm kidogo tu, au wewe ni Bashite nini ? Mana lile halinaga akili na ni liropokaji,. Kuna watu wapo ccm wengine ni wakurugenz na wamezaliwa USA ila sio poa kuwataja hawahusiki hapa kwenye hii mada.
 
Bora CDF kasema tungesema Sisi huku uongozi mzima wa JF ungetulamba ban ya miezi sita
Kweli kabisa na alivyokuwa anasema anaeupiga mwingi alikaa kimya ila kuna jitu la namtumbo linakuja hapa kusema sijui lisu sio raia na james mbowe sio raia sasa wanarelate vipi na kitu alichosema CDF ? Matutusa ni wengi sana nchi hii
 
Nikiri wazi kutoka sakafu ya moyo wangu, nimefurahi sana kilio changu na kampeni yangu ya miaka mingi kuona leo imejibiwa na Mkuu wa Majeshi nchini. Nilionya kuwa nchi yetu tumeingiliwa, tunahujumiwa tena vya kutosha.

Nakumbuka 22 December 2019 niliandika makala hii hapa chini nikitilia mashaka kwamba taifa linahujumiwa na hawa walioko madarakani, walioko katika sekta za maamuzi mazito ya Taifa letu kuanzia ikulu hadi ofisi ya mtaa/kijiji. Naomba nikurejeshe katika makala hiyo kisha linganisha na alichosema Mkuu wa Majeshi.
__________

"Kuna mambo katika nchi yanahitaji uchunguzi kubaini pengine kuna hujuma katika taifa, hii inatokana na michakato mingi muhimu ya kichumi na kijamii imekuwa ikiishia njiani na kuliacha taifa katika hasara kubwa. Hii ni hujuma inahitaji mwarobaini kulitibu.

Mifano ya michakato ambayo kwamiaka mingi imekuwa ikiishia njiani ni kama vile sekta ya nishati ambapo uzalishaji wa umeme limekuwa jambo linalotumiwa kama mchakato wakuzuka na kufa kwa miaka mingi sana tangu mwaka 1994 ilipokuja kitu kinaitwa umeme wa dharula kuokoa taifa (IPTL), ikafata michakato mingi yenye kuumiza taifa na haikufanikiwa hadi tukafika kuchimba Gesi mtwara tukapoteza mabilioni, gesi hadi Kinyerezi, kufumba na kufumbua mradi umetelekezwa sasa tunaimba mradi wa Bonde la Rufiji. Twende tuendelee..

Serikali ya awamu ya nne ilianzisha mradi wa kimkakati kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara duniani, mradi huu ilikuwa ni kujenga bandari ya Bagamoyo kwa ubia kati ya China na Omani wenye thamani ya dola bilioni 10, Serikali ya Tanzania katika mradi huu ilikuwa haiweki pesa yoyote isipokuwa ardhi na raslimali zingine, huku Uchina na Omani wakiweka mtaji na utaalamu.

Kwamjibu wa mapendekezo ya makataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na uwezo wa kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badi ingekusanya gawio toka kwa chombo kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu.

Huu ni moja ya mradi ambo kimsingi ulikuwa umeitangazia dunia vita vya kiuchumi toka kwa washindani wetu ambao ni nchi jirani na zinazotuzunguka. Kwakuwa Afrika yote ingepokelea bidhaa zake toka ulimwenguni hadi Bagamoyo, sawa na ilivyo Dubai ambayo ndio mlango wa Afrika kupokelea bidhaa zake. Afrika inaingiza bidhaa toka Uchina kwa 88.8% na kiwango cha 98% ya bidhaa hizo zinapita Dubai. Hivyo kujengwa kwa Bandari ya Bagamoyo kungefunga nyia ya Dubai na bidhaa zote za Afrika kutoka China kupita Bagamoyo. Hii inamaana kwamba uchumi wa Dubai na Marekani ambayo ndio mdau mkuu ungemegwa. Mradi huu ulikuwa ndio msingi halisi wa kuanzisha mradi wa reli ya kisasa ya SGR, bila Bandari itakayozalisha mizigo kwa wingi SGR itakuwa ni kwakubeba abiria tu badala ya mizigo.

Serikali ya awamu ya tano katika hali ya kustaajabisha iliutupilia mbali mradi huo kwakutoa sababu ambazo hazina nguvu na zingine za kushangaza sana, mimi naitafsiri kama ni hujuma kwa taifa, izingatiwe kuwa tayari taifa lilishaingia gharama kubwa kuanzia kwenye upembuzi yakinifu, na kusaini mikataba ya awali. Kitendo cha kusitisha katika hatua hii ni kulitia hasara taifa.

Ajabu la dunia zaidi, Wale waliokuwa washindani wetu Dubai rasmi baada ya kutangaza mradi wa Bagamoyo, ndio wamekuja kuwekeza katika bandari ya Dar ambayo sisi tuliona ni ndogo kwa aina ya mipango yetu ya kiuchumi na Kimataifa, kuwekeza Bandari ya Dar kwa Dubai lilikuwa tangazo la kuua mradi wa Bagamoyo, hata kama mamlaka zinasema zitaanza mradi huo, ukweli haziwezi kujenga kama ilivyokusudiwa katika mipango ya awali. Na moja ya vipengele kwenye mikataba wa DP World ni kuwa tukitaka kuendeleza mradi wa Bagamoyo kipajmbele apewe yeye akishindwa ndio tutafute mwekezaji mwingine.

Katikati ya mvutano wetu na wabia hadi kusitisha, Rais wa Msumbiji Philip Nyusi kwakutumia majasusi wake waliotanda kila pembe ya Afrika na kwingineko, amefanya mageuzi makubwa, amechukua wazo lilelile ambalo limekataliwa Dar es Salaam na wajuvi, amekwenda kulisimika katika Bandari ya Nacala kwakuingia ubia na Wachina kwa Dola bilioni 5, hii ni Bandari inayotarajiwa kuwa lango kuu la kiuchumi Afrika.

Wakati hili halijapoa, Mwaka 2017 Tanzania tulipowazuia wazungu tuliowauzia wenyewe madinini yetu na kilichomo ndani yake kwamba wasisafirishe madini ghafi na makinikia yao, tuliimba nyimbo kwamba Tanzania itajenga vinu vya kuchenjulia madini hapahapa, na nyimbo ziliimbwa kisiasa zikaitikiwa kishabiki kwa beti za kinafiki kwelikweli. Leo nyimbo haziimbwi, hakuna anayejua kama viwanda vimeshajengwa au laa na hakuna anayehoji hilo, tulishazoe vimbunga kwamba vitavuma na kutulia.

Lakini huku sisi tukiwa tumebadili nyimbo sasa tunaimba nyimbo za Standard Gauge nk, Rwanda kwakutumia majasusi wao waliotanda kila pembe ya Dunia, ilichukua wazo lilelile la Tanzania imejenga vinu vya kuchenjulia madini na inatarajiwa kwamba mwaka huu 2024 Rwanda iwe ndio nchi ya kwanza barani Afrika inayosafirisha madini kwa wingi nje ya Afrika. Kumbuka na elewa Rwanda sio mzalishaji wa Dhabu, Almasi wala chochote kiitwacho madini isipokuwa kwenye kilimo cha chai na kahawa huko. Hivyo anategemea viwanda vyake vipokee madini ghafi toka Tanzania, Kongo, Zambia ikusanye kodi yake na kugonga muhuri wa madini unaotambulisha kuwa ni madini toka Rwanda nk. Sisi tumelala. Siasa inanguvu bana.

Ukitaka kujua kuwa tumeingiliwa katika nchi, Angalia Zanzibar, kwa miaka michache tu aliyoongoza Mwinyi michakato mingi mikubwa ya kiuchumi imefanikiwa na kufika mwisho, Mfano Mwinyi amejenga upya uwanja wa ndege wa hadhi ya Kimataifa, Amejenga uwanja wa mpira wa miguu wa hadhi ya kimataifa, amesaini mikataba ya ujenzi wa bandari ya abiria yenye hadhi ya kimataifa pengine itakuwa ndio bandari nzuri na kubwa barani Afrika. Kama hiyo haitoshi, Mwinyi anajenga bandari ya mizigo, amesaini ujenzi wa reli ya kisasa itakayoanza ujenzi hivi karibuni.

Kwa maoni yangu ninafiki kuna tatizo kubwa kwenye eneo la Ujasusi katika nchi yetu, hasa ujasusi wa Kiuchumi, na hili ndilo lilikuwa msingi wa kuandika Kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Michakato mingi ya kiuchumi katika nchi hii imekuwa haina mafaa ama inaliacha taifa katika makovu makubwa yasiyozibika. Hii inazaa uhalali wa kuhitaji mageuzi makubwa katika Idara ya Ujasusi nchini kuanzia kwenye ideology, sheria, misingi, kanuni, na mambo anuai ndani ya idara ya ujasusi nchini.

Ujasusi kwa nchi zilizoendelea kama China, Israel, Urusi na Marekani, unafanywa na watu ambao ni smart na wanajengwa kuwa smart ili kuweza kumudu ugumu wa kazi hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa. Majasusi katika nchi hizo hawapewi kazi kwasababu ya ujomba ujomba na kujuana.
Ni kweli asilimia kubwa ya information's zenye thamani katika kazi ya ujasusi huwa zinaletwa na "human intelligence" badala ya magazeti, TV na source nyingine za habari.

Kwa maana hiyo basi ni lazima kuwe na watu competent ambao wana uwezo wa kukusanya habari za kijasusi ili tuweze kupata information's za maana na kujenga uwezo wa kuzifanyia kazi informations hizo. Imagine wakati ule wa vita baridi jinsi Directorate 16 ya KGB ilivyoweza kufanya kazi ya kununua sensitive navy information za USA na kuweza kutengeneza balance ya navy fleet bila USA kugundua kwa miaka 17 kupitia kwa Johny Walker junior!

Nitoe rai kwa Mkuu wa Majeshi nchini, aanzishe Oparesheni ya kijasusi ya kulisafisha taifa kuanzia ngazi ya kaya, kijmtongoji, kijiji/mtaa, Kata, Wilaya, Mkoa, Taifa na Ikulu. Jeshi lifanye tathimini ya kina kuona Tanzania kwenye balozi zetu kuna majasusi wa aina gani. Wale wa kujua kuongea kifaransa na kireno na lugha nyingine za mataifa ya nje bila upeo wowote wa Technologia?. Kama kuna sehemu tunakosea zaidi basi ndio hapo kwenye balozi.

Majasusi wengi wa Tanzania au tunaoambiwa kuwa ni watu wa system wengi katika tafsiri ya kijasusi ni "informers". Ujasusi kama ujasusi hapa Tanzania ni kama hakuna. Usalama wa Taifa au TISS/UWT msingi wao uliounda chombo hiki ni "power defensive", yaani wajibu mkubwa unaelekezwa kwenye kumonitor mwelekeo wa kisiasa Tanzania hasa kuwadhibiti oppositions na elements zote za upinzani na assasinations za elements zozote zinazoonekana kuwa against himaya ya CCM. Hili nilitaraji kwenye mabadiliko ya kisheria na kimuundo lingebadilika kwenye marekebisho ya August 2023, Bahati mbaya wanasiasa waliingilia na kuzuia mabadiliko hayo tukabaki kulekule.

Nirudie kusema, Asante sana Mkuu wa Majeshi, Niwatakie Oparesheni njema ya kulijenga upya taifa letu kutuondolea majasusi wa kigeni walioko CCM na Serikalini wanaokwamisha maendeleo ya nchi yetu, Nihimize umakini na uangalifu katika Oparesheni nyingi huko nyuma zimeacha makovu makubwa yasiyofutika, Kwahakika Dunia inatuona, hii ichukue tahadhari zote za kiusalama bila kuumiza wananchi wasio na hatia.

Ok, In case umesahau au ulikuwa hujui, Mshindi wa Tuzo ya Mwandishi Bora wa Vitabu Barani AFRIKA ni YERICKO YOHANESY NYERERE kutoka TANZANIA.

Sifa na heshima ni za Watanzania!

Idumu Mizimu!

View attachment 2879795

View attachment 2879796
View attachment 2879797
Hiyo miradi ulitoitaja, haikuendelea sio kwa sababu kuna watu wamepandikizwa ma jasusi wanahujumu! Hizo ni conspiracy tu hazinna ushahidi, hapo ni rushwa tu na wizi, wa CCM, viongozi wote anateua Raisi!
Maraisi waliopita, Mkapa, Kikwete, Maghu!
Mkapa aliuza mashirika ya umma, akajiuzia mgodi na ikulu ndogo, unataka kusema ni "ma jasusi wa, Rwanda ndio, wlimfanya afsnye hivyo?
Ur fucking kidding me bro!
Kikwete kauza gesi,skendal za, Richmond, wizi wa meremeta, huo, wote umefanywa na ma jasusi!? Serious, bro!
Incompetence, na, wizi ndio balaa LA Nchi hii,
Haya, aliyetoa amri Wa Masai wahamishwe kwa lazima, bandsri ziuzwe kwa mwarabu, tundu lisu apigwe risasi, Imran kombe auliwe kama jambazi, watu wanyongwe na kutupwa coco beach ni majasusi waliopandikizwa?
Hizi, story zenu kawasimulie watoto wa day care
 
MWAMBA KABISA WEWE....
 
Viongozi wa kamati kuu ya chadema wamelia sana baada ya kupata taarifa za Upendo Peneza kujiunga na CCM. Mmoja ya kiongozi hao, Freeman Mbowe alisikia akitoa kilio cha kwikwi.

Tusisahau James Mbowe sio raia wa Tanzania lakini Chadema wanampa vyeo ndani ya chama chao.

Lissu, familia yake wote sio raia
Wa bongo mmefsnywa maskini, mpaka hamfurukuti! Manaona njia pekee ya kutoka kimaisha ni kujiunga na *chama", huyo binti, aliyeenda CCM, anajiunga na kundi kubwa LA vijana wenye njaa,aliondoka Kafurila, Nassari! Leo hii wapo wapi, "they are just the shells of their original self" Wamepewa, vijinafasi uchwara wasife njaa, CCM itawatumia tu, wakiisha utamu kama big j, watatupwa kule!
Ha kuna Jimbo wanaweza kupita kwa tiketi ya CCM, maana hata huko CCM wapo wenye njaa wengi tu,
Mtu alikuwa mbunge, miaka mitano,akalipwa milioni 250! Sasa hv ana njaa! Anataka aingie bungeni kuendelea"kuwasemea"wana Nchi!
Umalaya upo wa aina nyingi
 
Bora CDF kasema tungesema Sisi huku uongozi mzima wa JF ungetulamba ban ya miezi sita
Mbona mimi nimeandika sana tangu Jambo Forum 2006 mpaka leo na sijapigwa ban ndugu Mpetde !?
Uoga hata wa kuandika tukiwa na ID fake ni uoga wa kimaiti ndugu.
Tusitaje watu bila ya kuweka ushahidi usio na shaka.
 
Mpaka CDF kuamua kusema haya hadharani hali ni mbaya sana. Kwa utawala huu wa CCM nchi iko uchi kabisa dunia inatuchora sana. Wao kipaumbele chao ni kuendelea kutawala tu bila kujali mustakabali wa nchi.

Wakizungumzia usalama wa nchi wanamaanisha ustawi wa CCM madarakani. Hata ukisikiliza alert ya Rais kwa JW inalenga wao kuendelea kuwa madarakani na kuwaona Chadema kama adui wa nchi kiasi cha kuomba msaada wa JW kuwashughulikia Chadema.
Kiongozi akiwa dhaifu, kila kitu kitakuwa dhaifu.
 
Back
Top Bottom