Dhambi maana yake ni tendo baya ambalo mtu hufanya kwa kujua ni tendo baya, na anaamua kulifanya kweli. Dhambi Ina vipengele vitatu: kukusaidia, kuamua na kufanya/tenda. Katika mahusiano dhambi hutokea kama wahusika wanalenga kutumiana (exploitation of each other). Kumbuka hapo juu nimesema (dhambi ina madhara kwa mtu mwenyewe, mtu mwingine au jamii). Katika mahusiano ambayo wahusika hawana intention ya kuwa pamoja maisha yao yote, dhambi hutokea kwa sababu wanajihusisha kwenye mahusiano yasiyo ya kweli/yasiyo na kibali machoni pa Mungu/ya kudanganyana na kutumiana kama vyombo vya anasa (fornication, adultery). Kuna athari kwa wahusika na kwa jamii (yaani kutumia viungo vya wahusika kinyume na makusudio yake). Ni kama mtu asiye na madaraka/mamlaka ya kufanya jambo fulani alifanye kama mwenye madaraka/mamlaka nalo. Anayefanya hivyo anatenda kosa (hata kama kufanya hivyo kunamfurahisha au kunawafurahisha baadhi ya watu au hata watu wote maana if one person can make a wrong, even all people can do so). Lazima tujifunze kufanya mambo ambayo tuko authorised/tuna kibali nayo na tukifanya hivi tunafanya ndani ya utaratibu. Kufanya mambo nje ya utaratibu hata kama kufanya hivyo kunamfurahisha mtu, kuna matokeo hasi kwetu wenyewe au kwa watu wengine. Lazima kwenye mahusiano tuji'envolve' kwenye 'genuine relationships' (mahusiano yenye kibali machoni pa Mungu). Hapo tutakuwa tumeepuka dhambi. Hivyo, kabla ya kufanya jambo lolote tujiulize: je, jambo hili lina kibali machoni pa Mungu? Kama jibu ni ndiyo endelea nalo, na kama jibu ni hapana, achana nalo.