Pre GE2025 Kauli ya Nape na Mkuu wa Wilaya ya Longido kuwa serikali ya CCM inalazimisha ushindi katika uchaguzi zinahalalisha kuindoa CCM madarakani kwa nguvu

Pre GE2025 Kauli ya Nape na Mkuu wa Wilaya ya Longido kuwa serikali ya CCM inalazimisha ushindi katika uchaguzi zinahalalisha kuindoa CCM madarakani kwa nguvu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kawaida, chama cha siasa kilichopo madarakani kwa kuchaguliwa ki-demokrasia, hakipaswi kuondolewa madarakani kwa nguvu. Uhalali wa kuiondoa serikali madarakani unapaswa uwe kupitia sanduku la kura katika uchaguzi wa kidemokrasia, na kama kuna ukiukwaji wa haki za uchaguzi, mfumo wa sheria wa nchi unapaswa kurekebisha hilo.
Lakini pale inapothibitika kwamba chama kilicho madarakani kinatumia udanganyifu kuendelea kuwa madarakani, na haiwezekani kupata haki ya uchaguzi kupitia mfumo wa sheria au mahakama, ndipo inapokuwa halali kuiondoa serikali ya chama kilichopo madarakani kwa kutumia nguvu.
Uondoaji wowote wa serikali halali madarakani kinyume cha sanduku la kura ni kosa la uhaini na adhabu yake ni kifo kwa kunyongwa mpaka kufa!.

Suppose ni kweli Watanzania wakapata muujiza wa ajabu wa kupata uwezo wa ajabu wa kuiondoa serikali ya CCM madarakani by any means, nani ndie ataireplace CCM?.

Siasa ni sayansi ya siasa, political science hivyo inafuata kanuni za kisayansi, nothing can exist in a hollow, ili CCM iondoshwe there must be inertia to replace ili CCM iweze kuondoka au kuondoshwa there must be a replacement kwanza ndipo iwe replaced!.

Kwa vyama hivi vilivyopo bado hakuna chama cha kuireplace CCM, hivyo CCM is there to stay for a long long time to come kwasababu CCM sio tuu ni chama cha siasa, CCM ni chama Dola, CCM ni Dola! CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola!
P
 
Kuna taasisi nchini zikiamua tu watu wanaingia mitaani kusherehekea! Sababu za kufanya hivyo zipo.
Tatizo taasisi hizo zinaongozwa na machawa wa ccm ama wanachama wafia ccm.

Wakuu wa majeshi wanataka teuzi wakishastaafu (mfano Mabeyo) ama kugombea ubunge kupitia ccm (mfano Mbona).
 
Tatizo taasisi hizo zinaongozwa na machawa wa ccm ama wanachama wafia ccm.
Wapo watu ndani ya hizo taasisi, wanaona kinachoendelea na wanasubiri wakati muuafaka. NI jambo la muda tu. Wanajaribu kuwahonga sana viongozi wa taasisi hizo, waliopo madarakani na waliostaafu, lakini wapo wasiohongeka, na wapo wanaochukua vitu wanavyopewa lakini ndani ya mioyo yao wanajua siku za CCM zimekaribia kwisha. Taasisi hizi kuna chimbuko la vijana wameanza kujitokeza, kina Sankara, Traole wetu.
 
Wapo watu ndani ya hizo taasisi, wanaona kinachoendelea na wanasubiri wakati muuafaka. NI jambo la muda tu. Wanajaribu kuwahonga sana viongozi wa taasisi hizo, waliopo madarakani na waliostaafu,lakini wapo wasiohongeka, na wapo wanaochukua vitu wanavyopewa lakini ndani ya mioyo yao wanajua siku za CCM zimekaribia kwisha
Hili likiwezekana itakuwa ndiyo mwanzo wa ukombozi wa taifa letu.
 
Uondoaji wowote wa serikali halali madarakani kinyume cha sanduku la kura ni kosa la uhaini na adhabu yake ni kifo kwa kunyongwa mpaka kufa!.

Suppose ni kweli Watanzania wakapata muujiza wa ajabu wa kupata uwezo wa ajabu wa kuiondoa serikali ya CCM madarakani by any means, nani ndie ataireplace CCM?.
P
Mkuu Pascal, umenena vema. Uondoaji wa serikali halali madarakani kinyume cha sanduku la kura. Ndio maana tunasema, uhalali wa serikali ya CCM haupo, na hili sio Chadema wamesema, bali CCM wenyewe, na hiyo ndio basis ya thread hii! Kulikuwa na uhalali wa serikali ya CCM iliyotokana na uchaguzi wa 2020? Je litakuwa kosa kuiondoa hiyo serikali madarakani kwa kusingizio ni serikali ya kidemokrasia, kama kufanya hivyo kwa mfumo wa sheria haiwezekani?

Suala la kuiondoa CCM halafu nani ata-replace wala sio tatizo. Na wala hatusemi CCM ikiondoka Chadema au ACT wazalendo ndio wachuke nafasi, la hasha. Hata baadhi ya watu ndani ya CCM wapo walio wazalendo wa kweli, si CCM wote wamefisadika. Wewe Pascal ni mwana CCM, una ubaya kama wana CCM wengine tunaowajua? Tutajipanga upya, na kama ikibidi kuondokana na vyama vya kisiasa, basi tutafanya hivyo.

Kwani aliyesema lazima serikali ya nchi itokane na chama cha kiasi nani? Sisi hatuwezi kuwa na mfumo wetu ambao hata watu wengine wataiga? Traole wa Burkina Faso ametoka chama gani cha siasa? Nani amesema Burkina Faso mambo yao kwa sasa hayaendi kwa sababu hawana mfumo wa vyama vya siasa? Kwa hiyo basi, kuna ubaya gani tukawa na mfumo wa mawaziri ambao wanaomba kazi hiyo badala ya watu wachache kupewa kazi hiyo kwa sababu ambazo mara nyingi hazihusiani kabisa na uwezo wao wa kikazi bali ushabiki wao katika chama?

Siku ingetokea CCM wakaheshimu maamuzi ya kisheria tukawa na na raisi ambaye alikuwa independent candidate ingekuwaje? Kinachoendelea sasa nchini Kenya ni failure ya mfumo wa vyama vya kisiasa, na kujaribu kuweka serikali ambayo haijasimamia vyama vya siasa. Labda ni wakati mifumo ya uongozi wa nchi duniani ibadilike, na Tanzania can show the way.
 
Mkuu Pascal, umenena vema. Uondoaji wa serikali halali madarakani kinyume cha sanduku la kura. Ndio maana tunasema, uhalali wa serikali ya CCM haupo, na hili sio Chadema wamesema, bali CCM wenyewe, na hiyo ndio basis ya thread hii! Kulikuwa na uhalali wa serikali ya CCM iliyotokana na uchaguzi wa 2020? Je litakuwa kosa kuiondoa hiyo serikali madarakani kwa kusingizio ni serikali ya kidemokrasia, kama kufanya hivyo kwa mfumo wa sheria haiwezekani

Suala la kuiondoa CCM halafu nani ata-replace wala sio tatizo. Na wala hatusemi CCM ikiondoka Chadema au ACT wazalendo ndio wachuke nafasi, la hasha. Hata baadhi ya watu ndani ya CCM wapo, si CCM wote wamefisadika. Tutajipanga upya, na kama ikibidi kuondokana na vyama vya kisiasa, basi tutafanya hivyo.

Kwani aliyesema lazima serikali ya nchi itokane na chama cha kiasi nani? Sisi hatuwezi kuwa na mfumo wetu ambao hata watu wengine wataiga? Traole wa Burkina Faso ametoka chama gani cha siasa? Nani amesema Burkina Faso mambo yao kwa sasa hayaendi kwa sababu hawana mfumo wa vyama vya siasa? Kwa hiyo basi, kuna ubaya gani tukawa na mfumo wa mawaziri ambao wanaomba kazi hiyo badala ya watu wachache kupewa kazi hiyo kwa sababu ambazo mara nyingi hazihusiani kabisa na uwezo wao wa kikazi bali ushabiki wao katika chama?

Siku ingetokea CCM wakaheshimu maamuzi ya kisheria tukawa na na raisi ambaye alikuwa independent candidate ingekuwaje? Kinachoendelea sasa nchini Kenya ni failure ya mfumo wa vyama vya kisiasa, na kujaribu kuweka serikali ambayo haijasimamia vyama vya siasa. Labda ni wakati mifumo ya uongozi wa nchi duniani ibadilike, na Tanzania can show the way.
Naomba tuu kuheshimu mawazo yako ila kwa Tanzania hili haliwezekani, or at least not for now labda in future.
P
 
Naomba tuu kuheshimu mawazo yako ila kwa Tanzania hili haliwezekani, or at least not for now labda in future.
P
Exactly! Kwa sasa haliwezekani. Na sababu kwa nini haliwezekani kwa sasa tunazijua. Na kwamba in future labda litawezekana tuna matumaini.
 
Ingieni msituni
Na ukiingia msituni utakuwa unapigana na nani, CCM na Greenguard yao? Utalipua madaraja ya CCM au ya Tanzania? Huko ni kukosa busara kwa kiwango cha juu. Watu wasio na akili ndio wanafanya uamuzi wa kijinga wa kuingia msituni katika mazingira kama ya nchi kama yetu. Unachoma nyumba ya familia kwa sababu ndani kuna panya wanakula mahindi yaliyotunzwa kwa ajili ya chakula cha familia? Sasa huo ndio uhaini.

Mazingira ya Kabila wa DRC kuingia msituni yalieleweka, na Frelimo, na Museveni, na ZANU, na SWAPO, na MPLA. Lakini hayo sio mazingira ya hapa Tanzania. Tatizo letu ni jinsi gani tutawakamata hawa panya walafi na waharibifu na kuwafutilia mbali na kuharibu kabisa mazalio yao bila kuchoma nyumba ya familia. Sisi tuna akili kuliko wale waliofanya hivyo huko Liberia, Sudan, au Sierra Leone. Na mtu anaetaka kupandikiza ndani ya akili yetu tufanye yale yaliyofanywa katika nchi hizi ni mbaya kuliko ubaya tunaoona ukifanywa na CCM katika nchi yetu.
 
Basi acheni kulialia
 
Mwamko wa wananchi wengi kuliamini Sanduku la kura kupata viongozi wao umeshuka sana sababu ya RUSHWA na wizi wa kura.

Bomu litakaloripuka hapa kwetu siku za usoni, Kenya ikasome!!
 
Kura,ambayo ndio halali, wanauhujumu mfumo wake. Ukienda mahakamani kulalamika umehujumiwa wanaingilia maamuzi ya mahakama. Ukisema hadharani wanakuteka na kukupotezea. Sasa tufanyeje?
Machafuko tu.
 
Six5b0TZWlBbGx71.jpg
 
Back
Top Bottom