Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Uondoaji wowote wa serikali halali madarakani kinyume cha sanduku la kura ni kosa la uhaini na adhabu yake ni kifo kwa kunyongwa mpaka kufa!.Kawaida, chama cha siasa kilichopo madarakani kwa kuchaguliwa ki-demokrasia, hakipaswi kuondolewa madarakani kwa nguvu. Uhalali wa kuiondoa serikali madarakani unapaswa uwe kupitia sanduku la kura katika uchaguzi wa kidemokrasia, na kama kuna ukiukwaji wa haki za uchaguzi, mfumo wa sheria wa nchi unapaswa kurekebisha hilo.
Lakini pale inapothibitika kwamba chama kilicho madarakani kinatumia udanganyifu kuendelea kuwa madarakani, na haiwezekani kupata haki ya uchaguzi kupitia mfumo wa sheria au mahakama, ndipo inapokuwa halali kuiondoa serikali ya chama kilichopo madarakani kwa kutumia nguvu.
Suppose ni kweli Watanzania wakapata muujiza wa ajabu wa kupata uwezo wa ajabu wa kuiondoa serikali ya CCM madarakani by any means, nani ndie ataireplace CCM?.
Siasa ni sayansi ya siasa, political science hivyo inafuata kanuni za kisayansi, nothing can exist in a hollow, ili CCM iondoshwe there must be inertia to replace ili CCM iweze kuondoka au kuondoshwa there must be a replacement kwanza ndipo iwe replaced!.
Kwa vyama hivi vilivyopo bado hakuna chama cha kuireplace CCM, hivyo CCM is there to stay for a long long time to come kwasababu CCM sio tuu ni chama cha siasa, CCM ni chama Dola, CCM ni Dola! CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola!
P