OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Imenishangaza sana kusema suala la maji ni 'Kudra za Mungu'. Nimefikiria kama tuko serious na maendeleo. Labda nianze kwa kuwapa tafsiri ya maendeleo tofauti na ulizoea kuzisikia awali. Maendeleo ni uwezo wa mtu kuyadhibiti mazingira yake (Ability to command the environment). Hii inaenda sawa na maneno ya wenye dini "Nenda ukaitawale dunia".
Tafsiri ya maendeleo niliyoitoa ni ya Amartya Sen mwenye tuzo ya Nobel katika Uchumi. Kwa maana yake ni kuwa kama maji yapo Tegeta na wewe upo Mbagala, inabidi uyaamrishe maji kutoka Tegeta yafike Mbagala. Yeye anayetoka Mbagala kufuata maji Tegeta anakuwa hajaendelea ukilinganisha na yule ambaye maji yanamfuata Mbagala.
Hili ndio suala ambalo lipo kwa wenzetu kwenye kila sekta, mfano kilimo hawasubiri mvua nk. Kukubali kuwa vitu ni kudra unakuwa umekataa msingi wa kuendelea ambao ni kuamrisha maji. Just imagine kuna watu wanaishi majagwani na wanaamrisha maji yaliyo ardhini yaje juu wayatumie. Sisi hata kukinga maji yanayotiririka na tuyasafirishe kwenye maeneo stahiki hatutaki. Umasikini tunaupenda.
Kusema ni kudra za Mungu maana yake Wizara, Nchi, Mkoa, Mamlaka za Maji hazina mipango ya kufanya maji yapatikane muda wote ndio maana tunashindwa kudhibiti predictable risks.
I am sorry to say, wabongo tuna vichwa visivyo na ubongo.
Signed OLS