Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wakuu
Mwanamuziki maarufu wa dancehall kutoka Jamaica, Sean Paul, aliwasili Tanzania jana (Novemba 29) kwa ajili ya show yake inayotarajiwa kufanyika leo. Katika mahojiano na Bongo 5, alipoulizwa kuhusu Diamond Platnumz, Sean Paul alikiri kwamba hamfahamu msanii huyo lakini yuko tayari kukutana na kushirikiana na wasanii wa Kitanzania.
Kauli hii iliwashtua mashabiki wengi, kwani baada ya wapekuzi kufukunyua mambo ikajulikana kwamba msanii hao amem-follow Diamond kwenye mtandao wa Instagram.
Sean Paul amekuwa na ushirikiano na wasanii mbalimbali duniani, ikiwa ni pamoja na wimbo maarufu “Rockabye” alioshirikishwa na Clean Bandit na Anne-Marie.
Kauli yake ya kutowafahamu miamba wa muziki Bongo Simba na King Kiba, ina funzo kwa muziki wetu?