Hivi Tundu Lisu amemtukana tusi gani Rais Magufuli?
Kuna mambo ambayo wengi, hata baadhi ya wanaCCM hawafurahishwi nayo, tena yanabomoa misingi ya umoja wetu, lazima yasemwe tena kwa ukali kabisa.
Ujenzi wa uwanja mkubwa Chato, hakuna mwenye akili timamu anayeweza kutetea hilo. Uwanja mdogo wa ndege wa kawaida, hakuna ambaye angeshangaa. Ule ni uharibifu wa fedha ya umma. Lakini naambiwa siyo uwanja tu bali taasisi mbalimbali wamelazimishwa kujenga Chato. Hii haileti picha nzuri hata kidogo. Kama kuna watu wanafanya hivyo kwa kutaka kumfurahisha Rais, wajue wanamharibia sana.
Kuna mambo ambayo Rais Magufuli itabidi ayafafanue:
1) Uwanja mkubwa wa ndege Chato
2) Taasisi nyingi za serikali kulazimika kujrnga Chato na siyo Geita au Bukoba
3) Wateule wengi kutoka kanda moja
4) Wanafamilia au ndugu wa karibu kupewa nafasi kubwa za serikali
Pengine ana sababu za msingi. Kama ndivyo, afanye ufafanuzi. Bila kufanya hivyo, tuhuma za upendeleo, visasi na ubaguzi, zitaendelea kumwandama.
Mfahamu kuwa kuna mikoa mingi, tena yenye maendeleo binafsi mazuri kwa miaka mingi, hakuna kitu chochote kikubwa cha maana kikichofanyika awamu hii.
Sent using
Jamii Forums mobile app