Soka Ndio Maisha Yangu
Member
- Nov 27, 2024
- 43
- 127
Tangu mwanzo wanasiasa hawa walikuwa wakiongea maneno ya hovyo, kwenye mikutano ya TCD, mikutano ya kutoa maoni ya dira ya Taifa, mikutano yoyote yenye mikusanyiko ya watu, walikuwa wakitoa kauli za kibabe sana.
Mfano Boni Yai anawaambia wana chadema msinipigie simu nataka mtu akinipigia simu aniambie amechukua hatua gani kwa msimamizi wa uchaguzi au msimamizi wa kituo, huyo Mwaipaya akawa akienda hadi kwenye vipimajoto vya ITV anasimama kwa mbwembwe akisema kuwa wasimamizi wa vituo tunaishi nao, wakurugenzi tunaishi nao, migambo tunaishi nao, Polisi tunaishi nao, kwanza polisi wako wachache nchi hii sisi tuko wengi, tutasema nao.
Lissu naye ndio usiseme kila mtu anajua hadi anamkashifu Rais wa nchi, huyo Sativa daah hana adabu hata kidogo, kule kwa Mdude Nyagali yeye ndio anajiona mwamba kuliko wote ndani ya Chadema.
Sasa vitisho vya namna hii utadhani nchi hii haina vyombo vya usalama unamtishia nani? Uchaguzi umefanyika jana Boni Yai kapiga kura karudi zake home anatweet tu kwenye mtandao wa X sijui amekutana na kiongozi mstaafu wa Serikali amemwambia hivi hivi, huku vijana wa chama hicho wakila virungu na kutaabika.Huyo Mwaipaya kakaa pembeni, hakuna yeyote aliyeonekana akipambana zaidi ya kutumia mitandao kulalamika lalamika tu.
Kama sio kauli zao naamini uchaguzi ungefanyika katika mazingira ya amani na utulivu kuliko hivi sasa ambapo vijana wengi sidhani kama mwakani watakwenda kupiga kura.