Kauli zako Rais zitalitesa Taifa kwa muda mrefu, jaribu kupunguza hisia weka busara zaidi

Kauli zako Rais zitalitesa Taifa kwa muda mrefu, jaribu kupunguza hisia weka busara zaidi

ILA KAULI ZA NDUGU ZAKO MABEBERU WANAZOZITOA KWENYE MITANDAO KWA KUWAWEKEA WATANZANIA TENA WATUMISHI WA UMA KWAMBA WASIKIKANYAGE INCHI ZAO BILA HATA YA KUJA KUJIRIDHISHA JUU YA TUHUMA ZAO, ILA KWAKUWA KIONGOZI WALIYE MTAKA ALIGARAGAZWA, WAO VITENDO HIVYO HUWA MNAWAPONGEZA, SI NDIO?? TULIENI WAAMBIWE UKWELIII.
Hivi ndugu yangu kwa akili hiyo hiyo kidogo uliyojaaliwa unaamini wazungu wakitaka jambo lao wanashindwa?Hujifunzi tu nchi ngapi ambazo wazungu wamewaondoa viongozi wao kwa nguvu hata kama wananchi bado wanawahitaji?

Kuamini kwamba Tz eti inaweza kutunishana misuli na mataifa yaliyoendelea katika kila nyanja ni kupoteza muda.
 
Hizi kauli za kujifanya sisi ni tajiri kuliko Ulaya ndio zinatutia umaskini jeuri.

Kwa kipi tulichonacho mpaka umUlaya watuogope? Kipi?
Kuna Mzungu alisema hatuwezi kutengeneza hata mswaki. Nikacheck nikaona ni kweli.
 
Kwa upande mmoja yupo sawa kwa upande mwingine hayuko sawa naomba maoni yangu yaeleweke hivyo.
Ukikosa ktk moja umekosa ktk yote.
Huezi sema eti kwakuwa siyo mzinzi Basi utaingia peponi wakati unaua.

Kuto mwambia binaadam mwenzako kuwa huko uendako Kuna simba usiende, wewe ni muuaji tu.
Eti ukimwambia utamtia hofu!
Hofu ya vipi wakati kweli Simba yupo?

Eti chukueni tahadhari, tuchukue tahadhari kwa lipi?
Kwanini usiwe mkweli kuwa korona ipo?
Eti kwasababu ya miradi watu wataacha kufanyakazi na hela itaakosekana.

MIRADI NI BORA KULIKO AFYA NA UHAI WETU?
AMA KWELI HUYU NI MCHUNGAJI WA MSHAHARA, HANA UCHUNGU NA KONDOO KWAKUWA SIYO MALI YAKE
 
Being positive in a negative situation is not naive, it’s Leadership.

Besides, a leader is a reflection of their people, he is a product of his people, the same people he is now leading!
There are democratically elected and self imposed leaders. Your narration above refers to the the first category.
 
Hivi ndugu yangu kwa akili hiyo hiyo kidogo uliyojaaliwa unaamini wazungu wakitaka jambo lao wanashindwa?Hujifunzi tu nchi ngapi ambazo wazungu wamewaondoa viongozi wao kwa nguvu hata kama wananchi bado wanawahitaji?

Kuamini kwamba Tz eti inaweza kutunishana misuli na mataifa yaliyoendelea katika kila nyanja ni kupoteza muda.
Kwahyo kwakuwa wananguvu na wewe unaungana nao watufanye kama misukule?? Hovyo kabisa, masikini naye anahaki zake, usimnyanyase kisa unamlisha. Wateteni hao mabeberu wenu hapo ufipani.
 
Kwahyo kwakuwa wananguvu na wewe unaungana nao watufanye kama misukule?? Hovyo kabisa, masikini naye anahaki zake, usimnyanyase kisa unamlisha. Wateteni hao mabeberu wenu hapo ufipani.
Huu nao ni upungufu wa hoja,kwahiyo kila anayekosoa serikali mnadhani ni CHADEMA tu?Wakati mwingine kujikakamua uonekane una nguvu haitasaidia chochote bora kukaa kimya tu kwani hatutapungukiwa kitu.

Kila siku tunajiita matajiri lakini hadi ujenzi wa matundu ya vyoo tunasaidiwa na hao mabeberu.Sasa sisi matajiri tumewahi kuwapa msaada gani hao wazungu?
 
Inakuja kadri mtu anavyostaarabika(siyo kuelimika) Yaan anavyozidi kuishi na kuyatawala mazingira yake ,umri unavyosonga mbele ndivyo busara inavyotakiwa kuongezeka.unajitofautisha.
Busara siyo matako ambayo kila mtu anayo
 
Mimi nakuomba utafakari hili uliponye taifa. Mungu akubariki wewe na Taifa letu amen.
Mbona hotuba ya Rais ipo wazi sana?
Umeumia kwa kuambiwa usikimbilie chanjo ama kwa kuambiwa matajiri hawaitakii mema Tanzania.
Wazungu wakati mwingine huwa wanajihoji si kwa kufuata moyo wako wewe.
Wazungu wanajihoji kwamba,Magufuli pamoja na kinachosemwa ni dikteta,lakini amebana wala rushwa,ameongeza mapato kikubwa zaidi Magufuli sio tishio kwa Mmarekani au Muingereza,kwa hiyo wanaishia kumtizama tu
 
Huu nao ni upungufu wa hoja,kwahiyo kila anayekosoa serikali mnadhani ni CHADEMA tu?Wakati mwingine kujikakamua uonekane una nguvu haitasaidia chochote bora kukaa kimya tu kwani hatutapungukiwa kitu.

Kila siku tunajiita matajiri lakini hadi ujenzi wa matundu ya vyoo tunasaidiwa na hao mabeberu.Sasa sisi matajiri tumewahi kuwapa msaada gani hao wazungu?
Wapi nimetaja chadema, mbona kama umechanganyikiwaa
 
Kinjeketile Ngware(Maji Maji rebellion)
Ambilikile Mwasapile(loliondo)
Jei Pea M (imani)

Yaani Risasi puuuu kutoka kwenye shortgun ghafla inakuwa maji ? Au kwenda loliondo kunywa kikombe ukiamini kupona ukimwi ? Au imani za kuamini kuwa gwajima anauwezo wa kufufua wafu?

Hivi kule uganda kulikuwa na yule askofu aliyewaaminisha waumini wake kwenda mbinguni baada ya kuwachoma moto kanisani yupo wapi?
 
Huu nao ni upungufu wa hoja,kwahiyo kila anayekosoa serikali mnadhani ni CHADEMA tu?Wakati mwingine kujikakamua uonekane una nguvu haitasaidia chochote bora kukaa kimya tu kwani hatutapungukiwa kitu.

Kila siku tunajiita matajiri lakini hadi ujenzi wa matundu ya vyoo tunasaidiwa na hao mabeberu.Sasa sisi matajiri tumewahi kuwapa msaada gani hao wazungu?
Wewe lofa kweli,matundu ya choo ilikuwa hawamu ya nne wakati wa Kikwete,leta ushaidi tokea hawamu ya tano ya Magufuli,imeisha pokea msaada gani wa choo au shule?selikali ya Magufuli haitegemei misaada kuombaomba tena inafanya yenyewe.
 
Pamoja kuwa wewe ndio Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya taifa letu. Huna budi kukumbuka miiko ya kiti chako, nakukumbuka kauli zako iwe ni kwa uzalendo au ni kwa upendo mkubwa kwa watanzania basi huna budi kuzichambua na kuzitafakari kwa kina kabla ya kuzitamka.

Mh Rais unaliumiza taifa silence na mwisho kilio kitasikika kwa sauti kubwa. Hawa watu tunawaita mabeberu wamewekeza sana kwenye intelligence zao kiasi wanajua kila neno na sera za mataifa yetu. Wanajadili kila neno linatoka kwa watawala, kiufupi they are smart than us and the can eliminate us within a second.

Rais wangu hakuna tajiri anajisifia tajiri na kama yupo huyo sio tajiri ni masikini. Tajiri anasifiwa na kamwe hajisifii, mataifa ya wenzetu wanatushangaa kila siku sisi matajiri sisi matajiri, utajiri huu upo kwenye makaratasi au upo kinadharia na sio kwa vitendo na hii ni kama hujuma kwako mwenyewe as u raise your voice we are reach wanazidi kutubana kiasi itafika mahali nakwambia uchumi huu uta collapse ghafla mimi nakwambia ukweli Mzee wangu maana kuwa Rais sio kuwa na hekima zote.

Yusuph mfungwa alitolewa gerezani kuja kutegua kitendawili cha Mfalme aliekuwa hajui afanye nini na ndoto yake. Yusuph akaiponya nchi na leo Wewe kama Rais wetu nakushauri punguza maneno ya kujisifu, sisi ni matajiri unatuweka kwenye shida ambayo hutaiona sasa ila watakao kuja kiti kitakuwa cha moto unless utatawala milele lakini japo kwa mwendo huu Zimbabwe inanukia Tz.

Mh Rais hivi ujiulizi Tz hatuna even a single vaccine na wewe tangu utoto mpaka leo umedungwa masindano ya kinga ya kutoka kwa hao mabeberu, why unatweza jitihada za watu wanaotumia pesa na mali zao kutafuta sisi tuweze ishi, hivi kweli mkuu unaona hii ipo sawa? Wewe ni mwanasayansi ila umezungukwa na vichwa vyenye akili kiasi even you unajua sasa why usijishushe kama Rais ukawasikiliza.

Kauli zako Mkuu zina athari kubwa kiuchumi na ustawi wa hili taifa kama hutokubali kutumia hekima ktk kauli au kusoma hotuba.

Hotuba zako zinakuwa analysis na big agency na zinakuwa published kwenye vyombo vyao, angalia kauli yako jana walichoandika na uone kile kitatokea.

Kwani tupo peke yetu hatujafunga uchumi mbona mataifa mengi yana endelea na kazi. Japan hawaja lock down ila taratibu zingine zina endelea kama kawaida shida hapa u hate protocol na kutushawishi tuone hizo protocol sio sahihi. Hapa mkuu unatuchanganya as a nation. Ukisema hawa mabeberu sio hawafai basi turudi kwenye zama mawe dini hatukuwa nazo na tamadun hizi lakin tusibeze kazi nzuri ya hawa wazungu kutustaarabisha so tusibeze kaz zao. Tupongeze kwa sauti kubwa tuwaponde kwa sauti ya chini huwo ndio ustaarabu.

Nani anatuonea wivu na kama anatuonea wivu anashindwa nini kututawala maana anajuwa siri zote na mipenyo yote ktk taifa Waingereza wamekaa hapa wakatupa Uhuru, wajeruman the same Mmarekan amesaidiana na sisi kupata uhuru pamoja na mataifa mengine kutusaidia kumbuka diploma sia ni kitu muhim ktk dunia ya sasa ndio maana wamarekani wakaona sera ya Rais wao alie toka sio nzuri wakamtoa.

Wakati unaitangazia dunia sisi matajiri nchi ya jirani wameongeza uwezo wao kivita nani tajiri mtu ameagiza magari ya billion of Usd kwa ajili ya kupambana na makaidi wewe Hapo Mkuranga na kusini unaona kunavyo tuchanganya. Sasa nani Tajiri?

Mimi nakuomba utafakari hili uliponye taifa. Mungu akubariki wewe na Taifa letu amen.
Busara aipate wapi sasa? Nacho kile ni kilema sawa na kuwa kiziwi au kipofu
 
Mwaandishi wa maada, unamdharau Rais wetu mpendwa JPM, rais wetu John, aliyeishinda COVID-19, Mwaka jana. Wew tubu zambi zako, lasivyo wew mwaandishi, ni Muasi wa taifa(mhaini) Rebel, na utashughurikiwa kwelikweli. Muasi hana nafasi.
 
Yaani Risasi puuuu kutoka kwenye shortgun ghafla inakuwa maji ? Au kwenda loliondo kunywa kikombe ukiamini kupona ukimwi ? Au imani za kuamini kuwa gwajima anauwezo wa kufufua wafu?

Hivi kule uganda kulikuwa na yule askofu aliyewaaminisha waumini wake kwenda mbinguni baada ya kuwachoma moto kanisani yupo wapi?

Hahahaha,mkuu umetoboa 🤣🤣
 
Back
Top Bottom