Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Tuache kukariri ndugu, tufahamu haya;Maelekezo ya Magu wakati anaahidi kuzijenga alielekeza waliopo wasiondolewe,
Alitaka maskini wakae nao nyumba nzuri za kisasa.
Nyumba hamkujenga ninyi, kwann mzitolee mate?
Kwann kujitafutia LAANA za kujitakia?
Jengeni zenu hata kule makueni au kule Kiembe samaki mzifanye apartment za biashara.
1. Aliyesema waendelee kukaa kwenye hizo nyumba ni Rais (wakati huo alikuwa Magufuli) chini ya tamko lake na sio chini ya kanuni na utaratibu. Hivyo Rais mwingine anaweza kutengua/kulipuuzia hilo tamko na hakuna popote pa kwenda kuhoji au kupinga.
2. Tamko la Magufuli lilisema wakazi wote wa hizo nyumba waendelee kukaa humo kwa kuuziwa apartment kabla ya watu wengine. Na hicho ndicho kinachoendelea sasa. Hakuna popote tamko limekiukwa.
Wakazi hao kwa sasa wanapaswa kujenga hoja (kama ipo kweli) kwenye bei ya hizo nyumba kuwa kubwa kuliko uhalisia wa soko. Waje na mifano halisi ya kuonyesha apartment kama hizo, maeneo muhimu hapo Dar zinauzwa kwa bei pungufu ya hiyo. Wasijifiche tena kwenye kivuli cha unyonge, umaskini na siasa, hiyo ni biashara (kuna wabia wamewekeza fedha zao ili kujenga hayo majengo na lazima warejeshe pesa za kwa wakati na faida).
NOTE:
Mimi binafsi naona hizo bei ziko chini zaidi ya soko na ulipaji wako ni nafuu sana, na ikitokea zikatangazwa kuuzwa kwa mtu yoyote kuweza kununua, haitachukua hata wiki moja zote zitakuwa zimeuzwa huenda hata kwa cash.