Kaya 644 Magomeni kota zagomea kusaini mkataba kununua nyumba

Kaya 644 Magomeni kota zagomea kusaini mkataba kununua nyumba

Ndugu jitafakari upya, umeandika vitu vya ajabu ajabu tupu.
Hapa tunazungumzia mustakabari wa nchi yetu na sio matamko ya Marehemu (Magufuli).

Zile nyumba hazikuwa mali ya Magufuli, hivyo rejea ya matamko yake haina maana yoyote.

Zile nyumba zimejengwa kwa kodi za watanzania wote, na sio kwa pesa binafsi za Magufuli au pesa za wakazi wa Magomeni Kota.

Kanuni, taratibu na masharti ya serikali kuzingatia soko na biashara za upangishaji lazima zifuatwe.
Hali ya kiuchumi ya wapangaji hao ukilinganisha na mwaka 2015 imeporomoka mara dufu.

Hizo gharama walizoomba wauziwe ml 17 zilitakiwa zishuke Hadi ml 12 na walipe Kwa miaka Hadi 20.

Narudia, mkitaka faida, Serikali haipo Kwa ajili ya kumake PROFIT, IPO kusaidia raia.

Jengeni nyumba zenu binafsi ndo mpange faida,

Ukipewa nafasi ktk kuutumikia Umma wa Watanzania, tanguliza maslah ya umma mbele.

Aaamen
 
View attachment 2508191

Dar es Salaam. Wakazi 644 wa Magomeni Kota wamegomea kusaini mkataba wa kuanza kununua nyumba hizo, kwa madai kwamba bei waliyoletewa sio rafiki na haiendani na hali ya uchumi wao.

Aidha wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan aingilie kati kwa kuwa bei ya Serikali iliyowasilishwa ni kati ya Sh48 milioni na Sh56 milioni ni kiwango kikubwa wanachochukulia kama mtego wa kutaka kuwafukuza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa juzi na serikali kupitia kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambaye ni msimamizi wa mradi huo, mkataba huo unaanza kutumika kuanzia Februari 8 mwaka huu hivyo Kaya hizo zinapaswa kusaini kwa bei waliyoletewa.

Mwanasheria wa wakazi hao, Twaha Taslima akisoma barua iliyoandikwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Daud Kandoro, kwenda kwa wakazi hao, jana siku ambayo walifanya kikao mkoani Dar es Salaam, alisema bei iliyowasilishwa na serikali awali ilikuwa ndogo.

“Bei ambayo ilipendekezwa na Serikali awali ilikuwa ni Sh12 milioni hadi Sh17 milioni, iliyotolewa Juni mwaka jana, haikukidhi thamani ya eneo, haikujumuisha faida wala huduma za maeneo yanayozunguka makazi hayo ambayo ni jumuishi,” amesema.

Taslima amesema, "Njia mojawapo ya kuchukua ni kuiomba Serikali au kwenda mahakamani. Bei ya chumba na sebule kwa Sh48. 5 milioni na vyumba viwili na sebule Sh56.8 milioni inaweza isiwe rafiki na mnunuzu asimudu," alisema Taslima.

Mwenyekiti wa Wakazi wa Magoneni Koti, George Abel, amesema kwamba bei zilizokokotolewa siyo rafiki kwa wakazi hao, licha ya Serikali kuongezewa mkataba wa kulipa na kuishi kutoka miaka 10 hadi 15.

Amesema kuwa bei hiyo inatakiwa kila mkazi alipie Sh300,000 kwa mwezi hivyo kwa mwaka ni Sh3.6 milioni akisema kiasi hicho ni kikubwa ikizingatiwa baadhi ya wakazi tayari ni wazee na wastaafu.

"Tumepokea barua hii ikiwa zimebaki siku tatu tu kwamba tusaini mkataba wa manunuzi, tukutane tujadiliane kabla ya tarehe 8, Februari, mwaka huu, hizi bei si rafiki haziendani na hali za wakazi walio wengi," amesema Abel.

Mmoja wa wakazi wa nyumba hizo, Salama Goronga (65), amesema barua hiyo iliyosomwa kwao, ikionyesha bei hiyo imewahuzunisha kwa kuwa haiendani na hali zao kimaisha.

"Mimi nina wajukuu, na iliposomwa barua machozi tu yameanza kunitoka hiyo pesa nitatoa wapi, nitaondoka hapa niende wapi," amesema Salama.

Mkazi mwingine, Mwajuma Hamisi (82), amesema ana watoto wawili wa walioolewa ndio wanaomtunza kwa kumnunulia chakula na mahitaji mengine, hivyo itawawia vigumu leo hii waanze kumtafutia kodi mara atakapoondoka kwenye makazi hayo kutokana na kushindwa kulipia.

"TBA wanaotaka hizo nyumba, leo bei hii, kesho hii, tutalipaje mimi mzee, wanitoe hapa si aibu kwangu, mamilioni hayo nitayatoa wapi," amesema Mwajuma.

Alipoulizwa Kaimu Mkurugenzi kutoka idara ya miliki TBA, Said Mndeme amesema “Masuala hayo aulizwe mkuu wa taasisi ndiye anayejua,” amesema.

Mwananchi
Nashauri bei iongezwe ili hao masikini wakajengewe nje ya mji huko kimbiji, chekeni mwasonga, kimanzichana ama mohoro.

Hapo mjini wacha wakae matajiri wenye pesa ili mji uzidi kupendeza.

Unamuuziaje mtu city center kwa m50?
Hizo nyimba wapewe wenye uwezo nazo. Wakiwapa watu wasio na uwezo kesho hapatamaniki hapo maana maisha waliyozoea kuishi ya kiswahiliswahili uchafu mtupu.

Hizo nyumba sio za msaada bali biashara, asieweza kulipa aende kuishi kimanzichana.

Huna kipato unataka ukae city center ili usumbue watu? Si uende kijijini ukalime huko

Hakuna kuoneana huruma kwenye biashara.

Wazee wengi wa hapo kota walikuwa watumishi wa serikali ambao maisha yao yote ilikuwa ni kula bata mpaka kiinua mgongo wakalia bata, wachache sana walikuwa na akili ya kujenga.

Kuna mzee mmoja ni jamaa yangu alikuwa mtumishi serikalini ye maisha yake ilikuwa ni bata tu mpaka kiinua mgongo. hakuwahi jenga kwa sababu kota ilikuwa kodi sawa na bure.
 
Angalizo:

Mahusiano ya Serikali na wananchi ni kama ya mtu na bosi wake,

Wananchi ni Bosses na Serikali ni watumishi wa wananchi.

Viongozi wamegeuza ionekane Serikali ni bosses wa raia, NO, NO NO!!!

Hatukuiweka Serikali madarakani Ili ifanye Biashara na kuwafanya raia kuwa wateja, HAPANA.

Serikali KAZI kuu ni kuhudumia raia, imetumwa na wananchi KAZI Fulani Fulani Kwa maslah ya wananchi.

Aaamen
 
Magomeni mjini kati,kota za ghorofa alafu wakae malofa kizembe zembe tu iyo aipo nilijua tu ipo namna hao malofa wenzetu watapigwa chini kiaina flani.
Kama wananchi wengi ni malofa, Serikali pia ni Malofa.

Kila siku wanatembeza bakuli kukopa, iweje wawadharau wananchi malofa, wao Si wanatokana na wananchi malofa?

Viongozi Wachache ndo wanahusika na uhuni huu.
 
Wahame wakatafute sehemu nyingine ya kununua kwa bei wanayoitaka wao hakuna mtu anaweza kukuuzia nyumba yake eti kwa bei inayoendana na uchumi wako bali atauza kwa bei inayomlipa, hivyo kama hali zao za kiuchumi haziendani na hapo wakatafute sehemu itakayoendana na uchumi wao.
 
Hali ya kiuchumi ya wapangaji hao ukilinganisha na mwaka 2015 imeporomoka mara dufu.

Hizo gharama walizoomba wauziwe ml 17 zilitakiwa zishuke Hadi ml 12 na walipe Kwa miaka Hadi 20.

Narudia, mkitaka faida, Serikali haipo Kwa ajili ya kumake PROFIT, IPO kusaidia raia.

Jengeni nyumba zenu binafsi ndo mpange faida,

Ukipewa nafasi ktk kuutumikia Umma wa Watanzania, tanguliza maslah ya umma mbele.

Aaamen
Hoja zako ni dhaifu sana.
Serikali haikujenga zile nyumba pale magomeni ili kutoa huduma, wamejenga kufanya biashara. Lengo ni kuzalisha faida.

Wale wakazi wa Magomeni ni wapangaji tu, na mpangaji hawezi kumpangia mwenye nyumba kiasi cha kulipa.
 
Maelekezo ya Magu wakati anaahidi kuzijenga alielekeza waliopo wasiondolewe,

Alitaka maskini wakae nao nyumba nzuri za kisasa.

Nyumba hamkujenga ninyi, kwann mzitolee mate?

Kwann kujitafutia LAANA za kujitakia?

Jengeni zenu hata kule makueni au kule Kiembe samaki mzifanye apartment za biashara.
Nyumba zimejengwa na serikali na wala si ngedere yeyote yule.
 
Kama wananchi wengi ni malofa, Serikali pia ni Malofa.

Kila siku wanatembeza bakuli kukopa, iweje wawadharau wananchi malofa, wao Si wanatokana na wananchi malofa?

Viongozi Wachache ndo wanahusika na uhuni huu.
naibu waziri wa ardhi na makazi ajawekwa pale kwa kubahatisha.
madili yatafunguliwa kusini na kaskazini.malofa awana chao ni kulalama tu.
 
Walioishi hapo ni mababu na mabibi zao ambao pia walikuwa wamepangishwa na halmashauri!! Sikujua huu utaratibu WA kuwafidia wajukuu wa wapangaji pesa na nyumba bila Mkataba ulitoka wapi!? Just politics!! Eneo ni strategical Kwa biashara na Sio kujenga na kugawa Bure!! Majengo ya biashara Malls zingezaa ajira nyingi, my country!! Makazi wangejenga chanika na Mabwe Pande
Nyumba za makazi zikijengwa Chanika hizo biashara kwenye hayo maeneo zitafanywa na wanyama au wadudu?
 
Kwani ni lazima hao wakazi wakae hapo hapo Magomeni kwenye hizo nyumba?
Kwani ni wao tu wenye uhuhitaji wa nyumba bora hapa Tz?
Wanazing'ang'ania kwani ni mali yao?

Kama wanaona gharama ya kuzinunua ni kubwa, basi waende wakanunue huko kwenye gharama nafuu au wajenge nyumba zao.
 
Hivi hao wakazi wa Kota walikuwa Ni wapangaji au wemye nyumba?

Vitu vingine havihitaji elimu kubwa kujielewa.

Mlikuwa mnaishi bure pale Kota,
Mkalipwa na pesa za kwenda kupanga vyumba,

Bado mmepewa offer mkae bure miezi kadhaa ili baadae mnunuwe nyumba hizo.


Mnagomea kununuwa mnasema pesa kubwa,,,

Mnagomea mwenye nyumba zake?

Nyumba za serikali sio za wapangaji wa Kota.,
Serikali itoe bei elekezi kwa anayetaka kununuwa tujitose kununuwa,,

Vitu vingine hovyo kabisa...

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom